Habari za siku ndugu msomaji wa mtandao huu wa AMKA MTANZANIA ni matumaini yangu unaendelea vizuri katika harakati zako za kutafuta mafanikio na uhuru wako wa kifedha. Katika kona yetu ya Ujasiriamali na biashara, tutajifunza Jinsi mawazo hasi yanavyoihua biashara yako. Mamilioni ya watu wamekuwa wakikabiliana na changamoto mbalimbali katika dunia hii tunayoishi. Mbali na misukosuko katika maisha au katika mahusiano , hali inayochangia kutokuelewana, msongo wa mawazo, magonjwa, hata wengine hufikia hatua ya kujinyonga. Kadhia nyingine kubwa ni kuhusu kushindwa au kufilisika kwa biashara aliyonayo mtu.

Kutokufanikiwa kwa biashara kunatokana na mipango katika biashara, masoko na suala la kifedha. Pia inakuwa si rahisi kujua kwa undani ni kwanini biashara ndogo zinakufa. Haitoshi kusema kuwa ni kutokana na ushindani wa kibiashara uliopo, ama mabadiliko ya teknolojia, madeni, mauzo madogo, ama huduma mbaya kwa wateja.

Yote hayo ni ugonjwa unaosababishwa na usimamizi mbovu katika biashara husika. Tambua kuwa, ujuzi binafsi, elimu, kujituma na ari ya kazi ndivyo vinavyohitajika katika utawala wa biashara.

Biashara nyingi hushindwa kuendelea kutokana na ukosefu wa mawazo mazuri. Zinaweza kufa kutokana na muundo mbaya wa uwekezaji katika biashara. Mara zote kumbuka kuwa, mpango mzuri wa biashara ni mwongozo wa kufikia malengo ya kibiashara unayoyatarajia, hata kama kutakuwepo na baadhi ya vikwazo katika biashara ile unayoifanya. Kumbuka kuwa kama huna mpango mzuri katika biashara uliyonayo, ni sawa na kuwa na silaha ambayo huwezi kuitumia wakati wa mapambano. Kama hauna ujuzi wa kuendesha biashara yako, unajiweka kwenye nafasi mbaya ya kushindwa kuiendesha sio kwa sababu biashara hiyo haina faida, bali ni kwa kuwa unashindwa kuisimamia katika misingi inayotakiwa, kwa kuona ufahari kuwa na biashara ambayo haisongi mbele.

Jambo muhimu unapochagua kufanya biashara ni vema ukachagua ile ambayo una ujuzi nayo pia unaielewa kwa undani. Unaweza kuwatumia wale watu wenye vipaji ama wenye uaminifu katika biashara ambao wataweza kukusaidia kwa kile unachotaka kukifanya. Wape nafasi ya kukuongoza na kukufanyia tathmini au kukueleza kuwa hawakubaliani nawe pale unapokwenda tofauti katika biashara.

Ikumbukwe kuwa biashara nyingi zinaanza vizuri, lakini mwisho wake unakuwa mbaya, kwa kuwa biashara inaendelea kukua na wale wasimamizi wake wanashindwa kuisimamia vizuri kutokana na mahitaji yaliyopo kwa wakati huo au kutokuweka wafanyakazi wazuri wanaoweza kuleta ushindani kwenye soko.

Mfano mzuri katika hili, ni pale mfanyabiashara anapoanzisha kampuni na baadaye inakuwa kampuni kuu. Hapa utaona kuwa wale wafanyakazi aliokuwa nao katika ile kampuni akiwemo yeye mwenyewe, hawawezi kuwa na ushindani katika kuiendesha hiyo kampuni. Kwa kuwa kampuni inafanikiwa kwa kuwaweka watu wenye uzoefu na ujuzi, ambao kiwango chao cha elimu kinaridhisha.

Hata mfanyabiashara mkubwa, Bill Gate ambaye ni mwanzilishi wa Microsoft, amefikia hapo alipo kutokana na kuwa na timu imara ya watu wanaomzunguka. Kama mwanzilishi wa biashara yako inakubidi kujua ni wakati gani wa kuchukua watendaji wenye ujuzi katika biashara unayoifanya. Kwa upande mwingine katika siku hizi , suala la masoko linaonekana kuwa muhimu kuliko bidhaa husika. Mlaji analundikiwa bidhaa nyingi zenye matumizi yanayofanana. Hivyo inabidi kuwe na kampeni kubwa kwenye timu ya masoko ili kuweza kuuza bidhaa hizo.

Kumbuka kipindi ambacho bidhaa zilikuwa zikijiuza zenyewe kimekwishapita. Hivyo wajasiriamali wengi wanashindwa kujua ukweli huu katika kipindi hiki cha ushindani. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakifanya jitihada kubwa na kutumia muda mwingi kutengeneza bidhaa bora na kuziweka sokoni bila kujihangaisha kuhusu kutafuta masoko. Matokeo yake, hutumia pesa nyingi kwenye kuendeleza bidhaa na pesa kidogo kwenye kutafuta masoko ya bidhaa hizo, mwisho wa siku, mapato hupungua na wanafilisika na kuondolewa sokoni na wapinzani wao ambao wanajua mikakati ya kupata masoko kwenye biashara walizonazo. Endelea kutembelea mtandao huu wa Amka Mtanzania kwa makala bora zaidi za kujielimisha na kujihamasisha. TUNAKUTAKIA MAFANIKIO MEMA KATIKA BIASHARA YAKO NA TUPO PAMOJA.

Makala hii imeandikwa na Geofrey Mwakatika, Unaweza kutembelea blog yake Geofrey Mwakatika kujifunza zaidi.

kitabu-kava-tangazo4323

Habari njema kwako!!!

AMKA CONSULTANTS imekuandalia semina itakayoendeshwa kwa njia ya mtandao. Semina hii inajulikana kama SIKU 21 ZA MAFANIKIO MWAKA 2015. Kupitia semina hii utajifunza mambo mengi sana, baadhi ya mambo hayo ni jinsi ya kuweka malengo makubwa utakayoweza kuyafikia, jinsi ya kushika hatamu ya maisha yako, jinsi ya kuwa bora kwenye kile unachofanya, jinsi ya kutumia muda wako vizuri, jinsi ya kuongeza ubunifu wako na jinsi ya kuifanya kila siku kuwa ya maana kwako.

Mambo yote haya utakayojifunza ni muhimu sana ili kuweza kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa.

Semina hii itaendeshwa kwa siku 21 ambapo kila siku utatumiwa email yenye somo husika lililoelezwa vizuri na kukupa hatua ya kuchukua. Utaweza kuuliza swali au kuomba ufafanuzi katika wakati huo wa semina. Pia kama zoezi la kuweka malengo ni gumu kwako tutasaidiana hatua kwa hatua jinsi ya kufanya zoezi hilo.

Semina hii itaanza Jumatatu ya tarehe 05/01/2015 mpaka Jumapili ya tarehe 25/01/2015. Gharama za semina hii ni tsh elfu kumi(10,000/=). Siku ya mwishoya kulipia kujiunga na semina hii ni tarehe 31/12/2014. Ili kuweza kuwa na ushiriki mzuri wa kila atakayetaka kushiriki semina hii, nafasi zitakuwa chache sana, hivyo atakayewahi kulipa ndiye atakayepata nafasi. Nafasi zikijaa utakuwa umekosa nafasi hii muhimu sana kwenye maisha yako. Hivyo fanya malipo mapema ili kujihakikishia nafasi yako katika mafunzo haya muhimu.

Kufanya malipo, tuma fedha ya mafunzo, tsh elfu kumi kwenye namba 0717396253 au 0755953887 na kisha tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo ukiambatanisha jina lako na email yako.

Usikose nafasi hii muhimu ya kuuanza mwaka 2015 kwa mtazamo mpya na utakaoweza kukufikisha kwenye mafanikio makubwa unayotamani kila siku.

tunakukaribisha sana kwenye mafunzo haya ya siku 21, usipange kuyakosa, hutayapata tena wakati mwingine na wala hutaweza kuyapata sehemu nyingine. Fanya malipo leo ili kujihakikishia nafasi yako ya kushiriki mafunzo haya.Tunakutakia kila la kheri katika siku chache zilizobaki ili kumaliza mwaka huu 2014.TUPO PAMOJA