Kama kuna kitu hatari katika dunia ya sasa ni kuwa na chanzo kimoja tu cha kipato. Ni hatari sana kwani chanzo hiki kitakapopotea, unajikuta kwenye wakati mgumu sana. Lakini watu wengi, hasa walioajiriwa huwa hawalioni hili. Wengi wakishaaminishwa kwamba kupata ajira ndio njia salama ya kutengeneza kipato, hawajisumbui tena kuangalia uwezekano wa kutengeneza kipato kwa njia nyingine.
Hatari nyingine iliyopo kwenye kutengeneza kipato, hasa kwa kupitia ajira ni kwamba watu huwa wanajisahau haraka sana. Mtu akishapata mshahara anazoea kwamba mwezi ujao pia utaingia tena na hivyo kuona kama ni chemchem ya milele. Ni mpaka pale chemchem hii inapokauka ndio watu wanapoamka usingizini na kujikuta kwamba wameshapotea kwenye ulimwengu huu wa kutengeneza kipato.
Sasa leo nataka nikupe njia moja mbadala ya kutengeneza kipato ukiwa unaendelea kufanya hicho unachofanya sasa. Iwe ni kazi au biashara au hata kama huna chochote unachofanya, kuna njia nzuri sana ya wewe kutengeneza kipato. Njia hii haitakuhitaji uwekeze fedha nyingi ili kupata mavuno, bali itakuhitaji uweke juhudi na maarifa uliyonayo ili kuweza kutengeneza kipato.
Kabla sijakuambia njia hii ni ipi, ngoja tukubaliane kitu kimoja hapa. Kwanza kabisa hapo ulipo kuna kitu au vitu fulani ambavyo unavipenda sana, kweli? Ndio ni kweli, kuna vitu fulani ambavyo unapenda kuvifanya au kuvifuatilia kila siku na kila mara. Vitu hivi vinaweza kuwa vinaendana na kazi au biashara unayofanya au vinatokana tu na vipaji ambavyo unavyo. Inawezekana unapenda kufuatilia michezo, inawezekana unapenda kufuatilia mitindo, inawezekana unapenda kufuatilia mambo ya afya, upishi, teknolojia na kadhalika.
Pia hapo ulipo una ujumbe ambao unatamani sana kila mtu angeupata na kuufanyia kazi. Labda kuna kitu ambacho uliwahi kufanya na kikakusaidia sana kwenye maisha. Labda kuna mbinu fulani unazijua ambazo mtu yeyote akizitumia hatabaki kama alivyokuwa. Labda kuna vitu watu wanadanganywa kuhusu kazi au biashara unayofanya na ungetamani uweze kuwaambia watu ukweli. Nakumbuka siku moja mtu aliniambia, siku nikipata nafasi ya kuongea kwenye chombo cha habari, nitawachana sana hawa watu wanaodanganya watu kupitia biashara fulani, mimi nikamuuliza kwa nini usifanye hivyo leo? nilimpa njia ambayo na wewe nitakupa leo.
Jambo la tatu na la mwisho ninalotaka tukubaliane hapa ni kwamba wewe una kitabu ndani yako. Ndio, inasemekana kwamba kila binadamu anayeishi ana kitabu ndani yake. Kuna wengi ambao wanalitambua hili na kweli wanatamani wangeweza kuandika kitabu ila wanajikuta wanashindwa kufanya hivyo, labda kwa kuona wamekosa muda au kwa kuona uandishi wa kitabu ni kitu kigumu sana hivyo kuogopa kuanza kuandika. Wewe una kitabu ndani yako, na mimi nataka nikusaidie kuandika kitabu hicho. Haijalishi ni nani atakisoma kitabu hicho hata kama hakitasomwa na wengi lakini angalau wewe utakuwa umekiandika na itakuwa ni moja ya vitu utakavyojivunia sana kwenye maisha yako. Kuna vitu vingi sana umejifunza mpaka hapo ulipofika sasa ambapo kama utaweza kuviandika na kuwashirikisha wengine, utakuwa umewasaidia wengi.
Sasa kwa njia hizi tatu tulizojadili hapo juu unaweza kutengeneza kipato cha ziada wakati unaendelea na kazi yako au biashara yako. Unaweza kutengeneza kipato cha ziada kupitia kile ambacho unapenda kufanya, au kupitia ujumbe unaotamani sana kutoa kwa wengine au kupitia kitabu ambacho unapenda kuandika. Yote haya yanawezekana ukianza na kitu kimoja tu…. BLOG.
Ndio ukianzisha blog yako unaweza kuandika kitu chochote ambacho kinaweza kuwaelimisha wengine na wakati huo huo ukatengeneza kipato. Unaweza kuwa unaandika kuhusu kitu ambacho unapenda kufuatilia, ukakichambua vizuri na mtu akifika kwenye blog yako anajua ataondoka na maarifa ya kutosha. Unaweza kuandika kuhusu ukweli ambao unapindishwa kwenye kazi au biashara unayofanya na hapa ukapata watu wengi ambao wanataka kupata ukweli kabla hawajafanya maamuzi muhimu kwenye maisha yao. Na pia unaweza kutumia blog yako kama sehemu ya kuandika kitabu.
Makirita, maelezo yako nimeyapenda, lakini sasa mimi sio mtaalamu wa kutengeneza blog na sijawahi kuandika kwenye maisha yangu yote, hii hainifai mimi. Sasa kama hili ndio tatizo lako naomba nikueleze kwamba kama umeweza kusoma hiki nilichoandika hapa, basi una utaalamu mara mia ya unaohitaji ili kuanzisha blog. Na kuhusu gharama, ni gharama sifuri unahitaji ili kuanzisha na kuendesha blog yako. Na kuhusu kwamba hujawahi kuandika, hivi ulishawahi kutuma meseji yoyote kwa mtu, hata ya simu tu, kama jibu ni ndio, tayari wewe ni mwandishi mzuri.
Sasa ili kukusaidia wewe uweze kutengeneza blog yako na kuweza kuandika makala nzuri zinazosaidia wengine na wewe kuweza kutengeneza kipato kupitia blog yako, niliandika kitabu kinachokupa elimu yote muhimu. Kitabu hiko kinaitwa JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Hiki ni kitabu ambacho kina mbinu zote muhimu unazotakiwa kuwa nazo ili kuweza kutengeneza kipato kwa kufanya kile ambacho unapenda kufanya na bila ya kuharibu ratiba zako za sasa. Katika kitabu hiki kuna siri zote ambazo nazitumia mimi katika kuendesha biashara kwa njia ya mtandao wa intaneti.
Ni hatua gani uchukue?
Jipatie kitabu hiki ambacho kitakuwezesha wewe kufungua blog yako(kina maelekezo ya picha na mtu yeyote anaweza kufuatisha na kukamilisha blog yake ndani ya nusu saa), pia kitakuwezesha kuandika makala nzuri na zinazotoa maarifa kwa wengine. Gharama ya kitabu hiki ni tsh elfu kumi(huu ndio uwekezaji pekee utakaoweka kwenye blog yako, kuanzisha na kuendesha itakuwa bure kabisa). Kitabu hiki kipo kwenye mfumo wa soft copy, pdf na kinatumwa kwa email.
Kupata kitabu hiki tuma fedha tsh elfu kumi(10,000/=) kwenye namba 0717396253 au 0755953887 na kisha tuma ujumbe wenye email yako kwenye moja ya namba hizo na utatumiwa kitabu hiki.
Chukua hatua hii leo ya kujipatia kitabu hiki na utabadili maisha yako kwa kiasi kikubwa sana. Kwani wakati wengine wanapoteza muda wao kulalamikia vitu ambavyo hawawezi kuvibadili, wewe utakuwa unafanya mambo ambayo yanaweza kuwasaidia wengine.
Usikubali siku ya leo ipite bila ya kupata kitabu hiki, utakuwa umeidhulumu nafsi yako kwa kiasi kikubwa sana.
Nakutakia kila la kheri katika kuboresha maisha yako na kuweza kufikia mafanikio makubwa.
TUPO PAMOJA.

N;B USISAHAU KUJIPATIA KITABU CHAKO CHA BLOG LEO.