Kujifunza kila siku ndio hitaji la msingi kabisa la kuwa na maisha bora na mafanikio kwenye jambo lolote unalofanya. Na kujifunza tunakozungumzia hapa ni kujifunza kweli mambo ambayo ni ya msingi na sio kupata tu taarifa.
Naamini uko vizuri sana mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, najua kadiri siku zinavyokwenda maisha yako yanakuwa bora kutokana na kuweza kutumia maarifa mbalimbali unayopata kupitia AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Kazi yetu kubwa ni kuhakikisha wewe unapata maarifa bora sana yatakayofanya maisha yako yawe bora pia.
Kama wote tunavyojua na tulivyokumbushana hapo juu, kujifunza kila siku ni hitaji la msingi sana la kufikia mafanikio makubwa. Na sisi ambao tunaishi katika zama hizi tuna nafasi kubwa sana ya kujifunza kuliko nyakati zote kuwahi kutokea duniani. Kwa kuwa na simu yako tu, unaweza kujifunza mambo mengi mno kwa kusoma vitabu, kusoma mitandao na hata kuhudhuria mikutano kwa kutumia simu yako. Ni nafasi ya kipekee sana ambayo hatupaswi kuiacha ipite bila ya kuitumia.

KUTUMIA MAKUNDI YA WASAP KUJIFUNZA

 
Teknolojia imekuja na faida kubwa.
Simu yako ya mkononi, hasa hizi simu za kisasa zinazoitwa smartphone, ni kifaa chenye nguvu sana. Kifaa hiki kinaweza kukusaidia mambo makubwa sana. Simu hizi zimekuja na teknolojia mpya na nzuri sana za kuweza kuboresha maisha yetu.
Moja ya vitu vizuri sana vinavyopatikana kwenye smartphone ni mtandao wa WASAP au WHATS APP. Huu ni mtandao ambao watu wanaweza kutumia kwa ajili ya mawasiliano. Unaweza kutuma na kupokea ujumbe, wimbo, picha na hata simu. Na hapa huhitaji kuwa na dakika za maongezi au meseji bali unahitaji kuwa na kifurushi cha kuingia kwenye mtandao.
Na kitu bora kabisa kuhusu mtandao huu ni kwamba mnaweza kuwa kwenye kikundi ambapo mnawasiliana kwa pamoja. Ndani ya vikundi hivi taarifa inaweza kuwafikia watu wengi kwa wakati mmoja.
Wakati mtandao huu mpya unaingia na watu kuweza kuwa kwenye vikundi, watu walikuwa wakitumia vikundi hivi kuchekeshana, kutaniana, kupeana habari na mengine mengi.
Lakini kwa siku za hivi karibuni mambo yamebadilika sana. Vikundi hivi vimeanza kuwa sehemu kubwa ya kujifunza na kuhamasika. Ni vigumu sana kuendelea kufurahia vichekesho wakati maisha ni magumu. Hivyo watu wameanza kutumia makundi haya kujifunza.
Siku za hivi karibuni nimekuwa napokea maombi ya watu wakiomba nitoe mafunzo kwenye vikundi vyao. Wao tayari wana kikundi lakini wanakosa maarifa ya muhimu ya kuwaletea mafanikio. Na hivyo wanakuwa wanahitaji mtu wa kuwapatia mafunzo hayo.
Mara nyingi wanaonitafuta anakuwa mtu mmoja kwenye kikundi ambaye anaona kuna mafunzo yatawaa wote kama kikundi. Ni hatua nzuri sana hii ya kujifunza na ninaona watu wanaweza kunufaika kwa hili.
Kutokana na hitaji hili la watu kupata maarifa na mwongozo, ninatoa nafasi kwa kikundi chochote ambacho kinahitaji mtu wa kuwafundisha na kuwaongoza.
Kikundi hiko kiwe na mrengo wa kibiashara au shughuli zozote za uzalishaji ambapo kila mwanakikundi anakuwa na shughuli fulani anayofanya.
Kila mwanachama wa kikundi hiko awe amejitoa kweli na ana kiu kubwa ya kufanikiwa kwa kile anachofanya.
Kila mwanakikundi awe tayari kufanyia kazi yale anayofundishwa na kuleta mrejesho kwamba amefikia wapi, na changamoto ni nini.
Kwa kuwa mimi ni Kocha, siishii tu kufundisha, bali ninafuatilia utekelezaji wa yale ninayofundisha, hivyo wanakikundi wasiwe wa kufurahia tu mafunzo, bali wawe tayari kuyafanyia kazi na atatoa taarifa amefikia wapi.
Hii ni nafasi nzuri sana ya kila mwanakikundi kujifunza na kuchukua hatua, na kila mwanakikundi atasukumwa kufanya hata kama anapata sababu ambazo zinaweza kumfanya arudi nyuma.
Ni rahisi sana kuweka mipango, ila kama hakuna anayekuangalia kama kweli unaitekeleza ni rahisi kukata tamaa. Ila unapofanya kazi na kocha utalazimika kufanya hata kama hujisikii kufanya, na hapo ndio mafanikio yanapoanzia.
Tunawezaje kufanya kazi pamoja?
Kwanza muwe na kikundi, ambacho watu wapo tayari kujifunza na kufanyia kazi.
Pili kutakuwa na ada ya mafunzo na muongozo huu kwa mwezi, kwa kuanzia natoa ada ya punguzo kubwa sana ambalo halijawahi kutokea, na halitakuja kutokea tena. Ada kwa kuanzia itakuwa tsh laki tatu(300,000/=) kwa mwezi kwa kikundi kizima. Hii ni ada ndogo sana ukilinganisha na thamani ambayo kila mwanakikundi ataipata. Kama kikundi kina watu 100, maana yake kila mtu anatoa elfu 3 kwa mwezi, kama mpo 60 kila mtu anatoa elfu 5 na kama mpo 30 maana yake kila mtu analipa elfu 10 kwa mwezi.
Narudia tena hii ni ada ndogo sana kulipa kama kikundi, kwa kumkochi mtu mmoja kwa mwezi gharama ndio sawa na hiyo ya kikundi. Hivyo kama mna kikundi chenu, hebu chukueni nafasi hii kwa haraka sana, maana haitakuja kutokea tena.
Na kwa kutoa ada hiyo, wanakikundi wanakuwa wamejituma kweli kujifunza.
Kitu kingine muhimu ni kwamba fedha hizi atakusanya kiongozi wa kikundi mwenyewe au kwa utaratibu wenu wenyewe na mimi nitapatiwa hiko kiasi kwa ajili ya kuanza kutoa mafunzo na mwongozo.
Faida kubwa mtakayiopata kama kikundi kwenye program hii.
Kila mwanakikundi ataweza kupata maarifa sahihi ya kufanya biashara yake au kufanya kazi zake.
Kila mwanakikundi ataweza kuweka malengo yake ya kikazi au kibiashara yatakayomfikisha kwenye mafanikio.
Kila mwanakikundi ataweza kujijengea nidhamu ya kutekeleza mipango yake hata pale anapokutana na changamoto kwa sababu anajua kuna watu wanamfuatilia.
Na mengine mengi…….
Ufanye nini sasa?
Kama wewe ni mwanachama wa kikundi, au kiongozi wa kikundi nakili makala hii na nenda ukaiweke kwenye kikundi chenu na wahamasishe wanakikundi wote kusoma. Na kama wataona inafaa mchukue hatua mapema. Kama wataona haifai na wewe unaona inafaa unaweza kuangalia njia nyingine za kufaidika na hili.
Mwisho kabisa niseme ya kwamba kadiri mnavyokuwa na kikundi kidogo na cha watu waliojitoa kweli, ndivyo itakuwa rahisi kwenu kujifunza na kufanyia kazi yale ambayo mnajifunza.
Niwakaribishe sana wale wote ambao mpo tayari kujifunza na kuboresha maisha yenu tufanye kazi kwa pamoja. Nafasi hii ni ya kipekee na haitapatikana tena hapo baadae, chukua hatua sasa.
Nakutakia kila la kheri katika kufanyia kazi haya ambayo unajifunza. Kama utahitaji kuwafinyiwa coaching wewe binafsi karibu tuwasiliane.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
wasap; +255 717 396 253