Habari msomaji wetu wa makala za uchambuzi wa vitabu. Karibu sana katika wiki nyingine ya uchambuzi wa kitabu. Wiki hii tunajifunza kwenye kitabu kinachoitwa Critical Thinking ama kwa Kiswahili waweza kusema Tafakuri tunduizi au fikra tundulizi. Kitabu hiki kimeandikwa na Harvey Segler . Mwandishi anafundisha dhana nzima ya fikra tunduizi, faida zake, jinsi gani unaweza kuwa critical thinker pamoja na mambo mengine yahusianayo na fikra tunduizi. Fikra tunduizi au Critical thinking inaweza kutafsiriwa kama ni uchambuzi na tathimini ya jambo kwa kusudio la kutengeneza hukumu, ila pia yaweza kutafsiriwa kama fikra huru, kule kutengeneza ukweli wako binafsi. Katika fikra tunduizi mambo mawili makuu yanayohusika ni upataji wa taarifa na pili ni kuziweka zile taarifa kwenye matumizi sahihi.

 
Karibu sana tujifunze
1. Fikra tunduizi inaenda bega kwa bega na fikra huru (independent thinking). Kama wewe ni critical thinker ni kwamba unaweza kufikiri wewe mwenyewe na kutengeneza mtazamo maoni/ mawazo yako binafsi kuhusu jambo fulani. Yaani unakua sio mtu wa kufuata mkumbo kwa vile fulani kawa na maoni haya, na wewe unaungana naye. Hapana lazima uweze kutengeneza mawazo au maoni yako yaliyo huru. Unakua na uwezo wa kuichukua hali au jambo fulani na kuthamini facts zake na kutengeneza hitimisho lako.
2. Ili kua mtu wa fikra tunduizi, unahitaji kuifundisha akili yako kufikiri yenyewe, bila kuangalia nani kasema nini. Kuwa Critical thinker Sio kitu kinachotokea tu utahitaji kuweka juhudi kuifunza akili yako iweze kufikiri kwa uhuru. Kwa bahati mbaya bila kutarajia hua tunapenda kwenda kwenye njia rahisi zaidi ambapo tunafanya kile ambacho kinafanywa na kila mtu, bila kujali ni kitu gani hicho wanafanya. Yaani hata kama ni kitu cha kipuuzi, kwa vile kinafanywa na kila mtu (au watu wengi) basi na wewe unafanya maana, huna fikra huru. You need to train your mind to think for itself.
3. Ili uweze kuondoka kwenye hilo duara, lazima ujifunze kuchuja taarifa unazopokea na kuchukua kile cha muhimu. Maana kutakua na maoni mengi, na ushauri tofauti tofauti, ambayo yote hayo yanarushwa usoni mwako kila siku, hutaweza kuzichakata (process) zote. Hii ina maana unahitaji kujifunza sanaa ya uchujaji wa taarifa ambazo unazipata, na kisha kuchukua kile cha muhimu tu. Weka umakini wako kwenye zile taarifa zenye kujalisha tu kwako na kuachana na hizo nyingine. Kama hilo jambo halina athari kwako, au kwenye kile unachofanya hiyo ni ishara ya kwanza kwamba hilo jambo lapaswa kuwekwa mwishoni kwenye orodha yako ya vipaumbele. Pay attention to the details that matter in your day, and forget about the rest.
Lakini je ni jinsi gani utaweza kutafahamu kwamba taarifa ipi uipe usikivu na ipi uitupilie mbali? Kuna njia au hatua tatu muhimu.
4. HATUA YA KWANZA: Zingatia Nia ya mzungumzaji. Huyo mzungumzaji ni nini hasa kinamsukuma kusema, hayo anayosema. Mtu anaposema kitu fulani, kuna uwezekano kuna watu wananufaika kwa njia fulani. Wanaweza kuwa kuna kitu wanataka kukuuzia au wanataka kitu fulani kutoka kwako. Kwa mtazamo huu sasa chukulia kila kitu unachokisikia au kukisoma kina chembechembe ya chumvi. Ndio panaweza kua na ukweli kwenye hicho anachokisema, lakini ukweli huo unaweza kua umechezewa kiasi fulani. Mfano unakutana na mzungumzaji wa anatoa taarifa za tiba asili, na kusema wanatibu magonjwa yote, sasa wewe jiulize huyo msemaji ana nia gani haswa? Kama tu Hospitali kubwa ya Taifa kama Muhimbili haiwezi kutibu magonjwa yote pamoja na vifaa na teknolojia waliyo nayo iweje, mtu mmoja tu akwambie anatibu magonjwa yote kwa miti shamba alafu unaamini na kuichukua hiyo taarifa kufanyia maamuzi na kuwashirikisha wengine. Consider the motive of the speaker.
5. HATUA YA PILI: Zingatia Chanzo cha Taarifa. Watu wengi sana wanatoa mawazo akilini mwao na kuyaweka kama ndio ukweli. Kitu hichi kimekua kikifanyika miaka mingi, ndio asili ya mwanadamu. Taarifa hizo zimejaa kila kona ya dunia, na kwa ujio wa intaneti kumesababisha ongezeko kubwa la taarifa. Wapaswa kukumbuka kwamba, kwa vile mtu kasema kitu fulani, hiyo haifanyi kile kitu kua kweli. Kanuni hii pia inakwenda kwa taarifa tunazozipata kwenye mitandao. Umesoma kitu kwenye intaneti usihitimishe kwamba ni kweli. Mpaka umeona chanzo chenye kuaminika au kuna ushahidi wa kuaminika endelea kua na mashaka nayo, usiiamini moja kwa moja. Never just blindly believe anything. Consider the source of the information.
SOMA; KITABU; Kurasa Za Maisha Ya Mafanikio, Nidhamu Uadilifu Na Kujituma.
6. HATUA YA TATU: Jilinde na vitu ambavyo viko wazi/dhahiri
Hila au mtego ambao unatumika mara nyingi na Wazungumzaji (speakers) ni kupata confidence yako kwa kusema vitu vilivyo wazi unavyovifahamu. Kinachotokea ni kwamba huyo mzungumzaji anataka ukubaliane na mtazamo wake/wao, na wanajaribu kufanya mtazamo wao uwe matazamo wako. Na kufanya hivyo hua wanaanza kusema vile vitu ambavyo viko wazi hata wewe unakubaliana navyo, kisha sasa ndio wanahamia kwenye vile vitu wanavyotaka kukushawishi ukubaliane navyo. Wanaanza na vile vitu unavyokubaliana navyo, ili imani yako ijengeke kwao, kwa vile umeamini vile vya mwanzo ni kweli basi utaona hata maoni yao ya mwisho ni kweli pia. Hii inaweza kua kwenye mazungumzo ya watu wawili, mijadala/midahalo au hata katika makala mbalimbali kwenye mitandao. Mfano Mzungumzaji anaweza kusema, “Tunafahamu unafanya kazi kwa bidii sana, na unathamini fedha yako. Na ndio maana bidhaa yetu ndio kitu kizuri kwa ajili ya wewe kuwekeza fedha yako” Unafahamu kabisa unafanya kazi kwa bidii, halafu unaendelea mbele unajaribu kufikiri ni kweli unathamini fedha yako. Baada ya kuwaza hivyo akili yako inakua imeshalainika kwa huyo mzungumzaji, na kila atachoongea baada ya hapo akili yako itaendelea kuamini kwamba ni kweli. Hata pale mzungumzaji anapohitimisha makala yake au hotuba yake, moja kwa moja akili yako inafikiri kwamba ile bidhaa ndio haswa kitu inachohitaji. Watch out for the things that are obvious. When you see that there are obvious statements being made, put up your guard, and watch for the real reason they are speaking.
7. Usilitazame uamuzi au tatizo kwa ajili ya kulirekebisha tu. Bali lichambue kwa kina. Unapokumbana na uamuzi wa kufanya au tatizo unahitaji kujiuliza wewe binafsi utafanya nini. Mara nyingi watu wanapopatwa na hali hizo hukimbilia kwa marafiki au ndugu kwa ajili ya kuwauliza nini wafanye kwenye hizo hali. Tatizo ni kwamba, kile ambacho ni kizuri kwa mwingine kinaweza kisiwe kizuri kwako. Suluhisho ambalo mwingine analiona ndio zuri, linaweza lisiwe zuri kwako. Unaweza kua umekumbana na uamuzi wakufanya kuhusu kitu gani usome, wengi hufanya uamuzi kwa vile wazazi au marafiki wamewashauri,. Utasikia “yaani wewe unafaa sana ukisoma sheria, yaani ukiwa mwanasheria unapendezea sana au ukikosa sheria unaweza kusoma Uhusiano wa kimataifa (international relation)” basi na wewe unaenda kusoma sheria au international relation. You need to ask yourself what you would do.
8. Maisha ni mtiririko/mfululizo (series) wa maswali na maamuzi ambayo unahitaji kujifunza na kuyafanya. Ili uweze kuishi maisha yenye matokeo. Fikra tunduizi ni ujuzi wa muhimu sana kuwa nao, maana utakusaidia kujifunza jinsi ya kuziendeleza sehemu nyingine za maisha yako na kukuhakikishia unapata matokeo yatakayokufurahisha. Maswali tunaweza kuyafananisha na matatizo/changamoto zinazotukabili kwenye maisha yetu ya kila siku, kwa kukosa ujuzi wa kutatua matatizo hayo au kujibu maswali hayo, wengi huishia kuwauliza wengine wawasaidie kujibu. Na unapomuomba mwingine akusaidie kukujibia maswali (matatizo) ya maisha unakua unakwepa kuwajibika kutokana na matokeo. Kama watafanikiwa kukusaidia utafurahia, ila kama matokeo yatakua mabaya utamlaumu huyo mwenzio kwa kutokufanya maamuzi ambayo yangekuletea matokeo makubwa. Ni muhimu sana kujifunza ujuzi huu wa kutatua matatizo peke yako. If you develop your independent thinking skills, then you can make your decisions in full confidence that they are going to turn out great.
9. Tunapata taarifa nyingi sana tena kwa muda mfupi zaidi kuliko ilivyokua huko zamani, mtu yeyote katika dunia hii mwenye ujuzi wa kutumia kompyuta au simu, anaweza kufahamu chochote kile ambacho anakitaka, anapata taarifa kwenye kiganja chake. Kuna faida nyingi kutokana na hili, ila pia kuna hasara moja kubwa inayozidi nyingine zote, na hiyo ni TUMEPOTEZA UHITAJI WA KUFIKIRI KUHUSU VITU AU MAMBO. Huhitaji kufikiri ili kuweza kutatua mambo tena, kama umekutana na changamoto kwenye chochote unachofanya, unachukua simu yako na kuingia Google, hapo unapata jibu tena kwa haraka, kisha unafanyia kazi, unatatua hilo jambo na kuachana nalo au kulisahau kabisa. Unakua hujifunzi chochote wewe binafsi, unaishia tu kupokea maoni na mawazo ya watu wengine kutoka kwenye makala ulizo soma kwenye mtandao, na hatupati ufahamu wa jinsi ya kutatua matatizo sisi wenyewe. The ability to solve and understand the solution to a problem is key in learning how to use critical thinking to solve your other life problems.
10. Usiogope kuuliza maswali. Ukiangalia wanafalsafa, wanasayansi na wanataaluma wakubwa wa kipindi cha nyuma kama kina Socrates, Newton, Einstein, n,k wana sifa kadhaa zinazofanana, ila moja wapo ni kuuliza maswali, Maswali mazuri ndiyo yanayoleta suluhisho nzuri. Mfano Newton alijiuliza swali kwa nini ukirusha jiwe juu linarudi chini? Kutafuta jibu lake, ndio kukagunduliwa sheria ya uvutano. Kabla hujafanya uamuzi wa kukubaliana na maoni au ushauri wa wengine, uliza maswali. Waweza kujiliza wewe binafsi na hao wanaokupa ushauri. Hata kama unakubaliana nao jiulize kwa nini unakubaliana nao, kama hukubaliani na wanachoeleza, pia jiulize kwa nini hukubaliani? If you aren’t willing to question your direction in life, you are no different than one of those cattle.
SOMA; USHAURI; Mambo Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuacha Ajira Na Kuingia Kwenye Ujasiriamali.
11. Kuwa Critical thinker katika manunuzi ya vitu. Katika kununua vitu, wengi huingia kichwa kichwa bila kufikiri kwa kina, kwa vile tu mwenzake kamwambia kitu fulani ni kizuri basi na yeye anataka anunue au kwa vile hicho kitu ni maarufu au kinatangazwa sana basi unanunua. Kwa bahati mbaya watu wengi huangukia kwenye mitego ya wauzaji, yaani anaamini kila kitu anachoambiwa na muuzaji bila kujua kwamba muuzaji ana mgongano wa kimaslahi (conflict of interest) kwenye hicho anachouza, hivyo sio rahisi yeye kukwambia ukweli utakaokufanya usinunue ile bidhaa au huduma.
Jinsi ya kuepuka kutumika vibaya kama soko la wengine. Unahitaji kufahamu kwamba wauzaji wananyemelea fedha zako, usipokua makini unaweza kua mtu wa kutumika vibaya kama soko la wengine. Hapa nimeweka mbinu chache za kudhibiti manunuzi yako.
12. Kabla hujanunua chochote jiulize kwanza hicho kitu kinatangazwaje? Kama ukiona katika kutangazwa kwake kuna kundi la watu wenye furaha, kukiwa na maana kwamba unahitaji hicho kitu (bidhaa au huduma) ili uwe na furaha na wewe, basi itakua vyema ukaacha kununua hicho kitu. Kwa sababu huhitaji kitu chochote ambacho huna sasa hivi ili kuwa na furaha.
13. Jiulize nani unajaribu kumfurahisha. Kabla hujanunua kitu jiulize kama unanunua kwa sababu unakihitaji hicho kitu kweli au unanunua kwa vile unafikiri kitakwenda kumfanya mtu fulani avutiwe na wewe. Kama hua unanunua vitu ili kuwafanya wengine wakupende au wavutiwe na wewe, basi unahitaji kufikiri upya kuhusu watu na marafiki wanakuzunguka. The real friends in your life aren’t going to be impressed with what you buy, they are going to like you for you.
14. Jiulize Je unaweza kuishi bila hicho kitu unachotaka kununua? Kuna vitu utakutana navyo ambavyo vinaonekana ni vizuri na vyenye kupendeza kwa nje, lakini wapaswa kufikiri kabla hujavinunua. Sio vibaya kununua kitu kwa sababu unakitaka, lakini usipokua makini baada ya muda utakuja kushtukia umenunua vitu vingi visivyokua na maana kwa sababu tu ya uzuri wa matangazo yake. Kumbuka wauzaji wanachofanya ni kukutengenezea kiu ya kununua hata kama huna mpango wa kununua, na ndio maana wanaweka juhudi katika kuitangaza bidhaa au huduma wanazozalisha.
15. Jiulize hizo fedha ungeweza kutumia kufanyia shughuli nyingine? Kumbuka una majukumu mengine, ni vyema ukafanya maamuzi sahihi, badala ya kununua tu kitu, angalia mbadala wa matumizi ya hiyo hela, kama usipotumia hiyo hela kununulia hicho kitu, ni matumizi gani mengine yangekua na manufaa zaidi. Utaingia kwenye matatizo mengi kama utakua unanunua vitu kwa tama, huku ukisahau vitu vya muhimu ambayo vinakusubiri. So think these purchases through carefully before you buy them.
SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha The Four Purposes of Life (Makusudi manne ya Maisha)
Njia za kutekeleza fikra tunduizi kwa vitendo katika maisha yako binafsi
16. Kwanza, Achana na ukusanyaji wa taarifa
Kama tulivyoona kwamba dunia imejaa taarifa nyingi sana, Aidha ziko kwenye intaneti, kwenye vitabu, kutoka kwenye makala, kutoka kwa marafiki, familia au kutoka hata kwa madaktari au wabobevu. Unahitaji kuachana na ukusanyaji wa taarifa usiokua na tija, na kisha anza kuchunguza ukweli wako mwenyewe. Ndio unaweza kupata ushauri kutoka kwa hawa watu, lakini usiweke msingi wa mawazo yako yote kwenye yale unayoyasikia kwa watu. You need to form your own thoughts and opinions, and be comfortable with that.
17. Kua kama mjinga anayetaka kujua kwa kuhoji maswali.
Usiogope kuuliza maswali. Uliza kila kitu maana kuuliza maswali ni kwa muhimu sana. Uliza kwa nini (why) kuhusu kila kitu. Usiwe kama kipofu tu kupokea kila kitu, na kuamini kila jambo. Hoji kuhusu dini yako, hoji kuhusu kazi unayofanya, kila kitu hakikisha unahoji.
18. Ukweli wa mtu mwingine unaweza usiwe ukweli wako.
Hii dunia ni kubwa, na kuna watu wengi sana tofauti tofauti. Kuna wale wanaamini njia fulani na kuifuata, ila pia kuna wengine ambao wanaamini njia ambayo ni kinyume kabisa na zile za wengine. Ukweli wa mambo ni kwamba wote wako sahihi. Ki uhalisia hakuna njia mbaya katika kutafuta ukweli wako, unachohitaji ni kufana kile kinachokupa furaha. Kuwa mtu ambaye yuko sawa na kua Yeye bila kufuata mkumbo. Usiwe mtu ambaye mpaka akubaliwe na wengine, maana ukiwa mtu wa kutaka ukubaliwe na wengine utakua mnafiki kwako binafsi, maana hata kama ukweli unaujua lakini utafuta wengine ili wakukubali. What’s true for one person may not be true for you. Some things that may be right for other people may not be right for you.
19. Fikiri
Mada kubwa katika kitabu hiki ni fikra tunduizi. Unahitaji kufikiri, bila kujalisha unafanya nini, usikwame kwenye njia za wapuuzi au wapumbavu, unahitaji kufikiri. Analyze. Feel. Dream. There is no end to the ways that you can think about things, so think think think.
20. Kua mdadisi
Haijalishi una umri gani au umefanikisha nini katika maisha, kamwe usipoteze udadisi wako. Udadisi ni ile hali ya kutaka kujua tena kwa kuuliza au kuhoji. Unapaswa wakati wote uwe mtu wa kushangazwa jinsi vitu vinavyofanya kazi. Usikubaliane na kitu kirahisi rahisi, kwamba vitu fulani viko tu kama vilivyo tafuta kujua kwa nini viko hivyo. Unaweza kushangaa au kuhoji jiko lako linafanyaje kazi, unaweza kushangaa au kuhoji gari lako linafanyaje kazi, au hata jinsi gani kazi yako ina mchango kwa jamii. Learn how things work. If you don’t know, look it up. If you do know, analyze.
Asanteni sana
Tukutane wiki ijayo
Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au barua pepe daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com