SEMINA; UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WATEJA.

Habari za wakati huu rafiki?
Hongera kwa kuendelea kuwa msomaji mzuri wa AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA. Nina imani kubwa kuna mengi ambayo unajifunza na ndiyo maana mpaka sasa tupo pamoja. Ombi langu kwako ni moja na limekuwa hili kila siku kwamba kile ambacho unajifunza basi kifanyie kazi rafiki yangu. Kifanyie kazi na ndipo utaona matokeo mazuri kwenye kazi yako, biashara yako, mahusiano yako, afya yako na maisha yako kwa ujumla.
Kama ilivyo kawaida yetu, kila mwaka huwa tunakuandalia semina mbalimbali ambazo zinakuongezea maarifa katika utendaji wako wa kazi, ufanyaji wa biashara yako na hata jinsi unavyoishi maisha yako ya kila siku. Katika semina hizi tunakushirikisha mbinu bora za kuhakikisha unapata matokeo bora sana kwenye maisha yako.
Kwa mwaka huu 2016 tumejipanga kukuandalia semina nne, na ya kwanza imekwishafanyika mwezi wa kwanza mwaka huu. Ilikuwa ni semina ya malengo na washiriki walijifunza mengi, wakaweza kuweka malengo makubwa kwenye maisha yao na sasa wanayafanyia kazi. Nina uhakika mwisho wa mwaka huu tutakuwa na wengi waliofanya mabadiliko kwa sababu wengi wanaendelea kufanyia kazi malengo yao.

Leo nina habari njema sana kwako rafiki yangu, na habari hizi ni kuhusu semina yetu ya pili kwa mwaka huu. Semina yetu ya pili kwa mwaka huu itafanyika mwanzoni mwa mwezi wa tano. Na kwa sababu tunataka kila msomaji wa AMKA MTANZANIA na KISIMA CHA MAARIFA aweze kushiriki semina hii basi inafanyika kwa njia ya mtandao. Hii ina maana kwamba popote ulipo duniani, iwe mkoa wowote wa Tanzania au nchi nyingine yoyote Duniani basi unaweza kushiriki kwenye semina hii.
Semina yetu ya pili kwa mwaka huu inakujia kwa jina UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WATEJA.
Huduma kwa wateja ni eneo muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku. Ukiangalia kwa haraka unaweza kusema hii inawahusu wafanyabiashara, na hapo ndipo unapokuwa unafanya makosa makubwa kwenye maisha yako. utoaji wa huduma bora kwa wateja ni jukumu la kila mtu ambaye kazi yake au shughuli yake inahusisha yeye kukutana na mtu mwingine. Kama unakutana na mtu, iwe kwenye kazi au maisha ya kawaida, basi kuna mbinu unazohitaji ili mahusiano yenu yaweze kuwa bora sana. Na hapa ndipo unapokuja umuhimu wa semina hii.
Semina hii itakwenda kwa siku kumi, na kila siku tutajifunza somo moja muhimu sana kuhusiana na utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Yafuatayo yatafundishwa kwenye semina hii ya UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WATEJA.
1. Kila mtu anauza, je wewe unauza nini?
Hapa utajua kile hasa ambacho mtu mwingine anakitaka kutoka kwako, ili uweze kukitoa kwa ubora wa hali ya juu.
2. Nani ni mteja wako?
Kila mtu ana mteja, na ni muhimu umjue mteja ili uweze kujenga naye mahusiano mazuri. Hapa utamjua vizuri mteja wako.
3. Mahitaji ya msingi ya mteja wako.
Pamoja na kujua kile unachouza, na kumjua mteja wako, bado kuna hatua moja muhimu sana ambayo ni kujua mahitaji ya mteja wako. Hapa utajua nguvu mbili zinazomsukuma mteja wako na jinsi ya kuzitumia vizuri.
4. Jinsi ya kutatua hali ya kutoelewana baina yako na mteja wako.
Mahusiano yoyote baina ya watu wawili huwa hayakosi mikwaruzano, hapa utajua njia bora za kutatua changamoto hizo na kuboresha mahusiano yako na mteja wako.
5. Mfanye mteja kuwa rafiki yako.
Mteja anapokuwa rafiki yako, hakuna kitakachokuzuia kufanikiwa kwenye biashara, hapa utajifunza mbinu za kujenga urafiki na mteja wako ambao utakunufaisha sana.
6. pokea maoni ya wateja wako.
Hapa utajifunza njia bora ya kupokea maoni ya wateja wako na jinsi ya kuyatumia kuboresha zaidi kile unachofanya. Pia utajifunza jinsi ya kutumia maoni chanya.
7. Kitu kimoja unachotakiwa kuzingatia sana na kitakunufaisha wewe na mteja wako.
Hiki hupaswi kukichezea hata kidogo, ni rahisi lakini asilimia kubwa ya watu wanashindwa kukitumia, utajifunza kwenye semina hii.
8. Gharama za huduma mbovu kwa wateja wako.
Hakuna kitu ambacho hakina gharama, kama unaona kutoa huduma bora ni gharama kwako, basi hapa utajifunza gharama za kutoa huduma mbovu na zinavyokugharimu.
9. Vaa viatu vya mteja wako.
Hii ni mbinu moja utakayojifunza, ambayo itabadili kabisa mtazamo wa kile ambacho unakifanya, hutaendelea tena kufanya kwa mazoea.
10. Matumizi ya mtandao na teknolojia katika kuboresha huduma kwa wateja.
Aisee rafiki yangu, kama bado hujaanza kutumia nguvu ya mtandao na teknolojia, unaachwa nyuma. Kupitia semina hii utajifunza matumizi bora ya mtandao na teknolojia katika kuboresha huduma kwa wateja wako.
Watu ambao semina hii inawafaa.
Semina hii haiwezi kuwafaa watu wote, hakuna kitu ambacho kinamfaa kila mtu. Hapa kuna watu maalumu ambao semina hii inawahusu sana. Angalia kama upo na uhakikishe hukosi semina hii;
1. Wafanyabiashara wote, wakubwa, wakati na wadogo.
2. Waajiriwa wote ambao wanakutana na watu moja kwa moja.
3. Waajiriwa ambao wanafanya kazi chini ya watu wengine, hii inawahusu sana.
4. Watoa huduma wote katika maeneo mbalimbali.
5. Watu wote ambao wamejiajiri wenyewe.
6. Wanafunzi wa elimu ya juu.
7. Watu wote ambao bado wanatafuta ajira, hii inawafaa sana.
8. Watu wote wenye familia.
9. Viongozi wote wa kisiasa, kidini, kijamii.
10. Watu ambao wanapenda kujifunza na kuongeza maarifa.
Jinsi semina hii itakavyoendeshwa.
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao, na kutakuwa na njia mbili za kujifunza. Njia ya kwanza ni kupitia email na njia ya pili kupitia kundi maalumu la wasap.
Kwa siku kumi, kila siku utapokea somo moja la semina hii, utalisoma, utafanyia kazi zoezi ambalo unatakiwa kufanya siku hiyo na kutoa mrejesho.
Mpaka kufikia mwisho wa semina hii utakuwa umetengeneza sera yako maalumu ya huduma kwa wateja na mfumo bora wa kuhudumia wateja wako.
Ada ya ushiriki wa semina.
Ada ya kushiriki semina hii itakuwa ni tsh elfu ishirini (tsh 20,000/=).
Ada inalipwa kwa njia ya mpesa kwenye namba 0755953887 au tigo pesa 0717396253. Katika malipo jina litakaloonekana ni Amani Makirita. Baada ya kulipa tuma ujumbe wenye majina yako kwenye moja ya namba hizo.
Semina itaanza siku ya jumatatu tarehe 02/05/2016 na itaisha tarehe 13/05/2016.
Kujiunga na semina hii ni kuanzia leo tarehe 04/04/2016 na mwisho ni jumamosi ya tarehe 30/04/2016.
Nafasi za ushiriki wa semina hii zitakuwa chache ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja kama timu. Hivyo ili kuhakikisha hukosi nafasi hii ya kipekee, jiandikishe mapema.
Kujiandikisha na semina hii bonyeza maandishi haya na ujaze taarifa zako.
Karibu sana tujifunze kwa pamoja ili tuweze kuboresha kazi zetu na biashara zetu pia.
Hakikisha unajiandikisha leo ili usikose nafasi hii nzuri, bonyeza hapa kujiandikisha.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s