Habari za wakati huu rafiki?
Unaendeleaje na safari yako ya kuyafanya maisha kuwa bora sana? Ni imani yangu bado unaweka juhudi kubwa na umeshasahau kabisa kama kuna kitu kinaitwa kukata tamaa. Hongera sana kwa hatua hizi unazochukua ili kuboresha maisha yako.
Napenda kuchukua nafasi hii kukukumbusha ya kwamba leo ndiyo siku ya mwisho kabisa ya wewe kujiunga na semina UTOAJI WA HUDUMA BORA KWA WATEJA. Leo hii tarehe 30/04/2016 ndiyo siku ya mwisho na jumatatu tarehe 02/05/2016 semina yetu hii muhimu itaanza.
Kama ungependa kupata mafunzo haya ambayo yatakuongezea maarifa ya kuwa bora zaidi hakikisha unachukua hatua ya kujiunga na semina hii leo hii, tena sasa hivi kabla hujasahau halafu ukaikosa nafasi hii nzuri.
Kama bado hujafanya maamuzi iwapo ushiriki au usishiriki nakushauri ufanye sasa kwa sababu watu wengi huwa wanakuja kuomba kuingia kwenye semina wakati mafunzo yameshaanza na wamekuwa wanaikosa nafasi hiyo.
Chukua hatua sasa ili upate maarifa yatakayokuwezesha kuwa bora zaidi na hivyo kuweza kufikia mafanikio makubwa. kumbuka hakuna maarifa yanayokwenda bure, lazima kuna kitu kipya ambacho utajifunza, hata kama una utaalamu mkubwa kwenye jambo hilo.
Kujifunza kila mara ndiyo kitu kimoja kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa. Na njia za kujifunza ndiyo hizi za ushiriki wa semina, kusoma vitabu na kusoma makala. Tumia nafasi hii nzuri ili kujiongezea maarifa ambayo yatakufanya uwe bora zaidi.
Karibu sana rafiki yangu tujifunze kwa pamoja.
Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao, yaani kwa njia ya kutumiwa masomo kwenye email yako na pia kuwepo kwenye kundi la wasap. Hivyo unaweza kushiriki semina hii popote pale ulipo duniani, huhitaji kutoka na kwenda eneo la semina, utayapokea mafunzo hapo ulipo. Utakuwa na mambo ya kufanyia kazi na pia utapata nafasi ya kuuliza maswali na kushiriki mijadala mbalimbali itakayohusiana na mafunzo haya.
Karibu sana ushiriki semina hii. Semina itaanza tarehe 02/05/2016, lakini mwisho wa kujiunga ni leo tarehe 30/04/2016, hivyo yamebaki masaa tu. Kama kweli unataka kushiriki semina hii na bado hujajiunga basi fanya hima kwa sababu muda uliobaki  ni mchache sana. Chukua hatua sasa usije kuipoteza nafasi hii nzuri sana kwako.
Katika semina hii tutajifunza yafuatayo;
1. Kila mtu anauza, je wewe unauza nini?
2. Nani ni mteja wako?
3. Mahitaji ya msingi ya mteja wako.
4. Jinsi ya kutatua hali ya kutoelewana baina yako na mteja wako.
5. Mfanye mteja kuwa rafiki yako.
6. pokea maoni ya wateja wako.
7. Kitu kimoja unachotakiwa kuzingatia sana na kitakunufaisha wewe na mteja wako.
8. Gharama za huduma mbovu kwa wateja wako.
9. Vaa viatu vya mteja wako.
10. Matumizi ya mtandao na teknolojia katika kuboresha huduma kwa wateja.
Karibu sana ushiriki semina hii ambayo itakupa mbinu bora za kutoa huduma bora kwa wateja wako na hivyo kuendelea kufanikiwa kwenye biashara na kazi yako. Kushiriki semina hii tuma ada ya ushiriki ambayo ni tsh elfu 20 (20,000/=) kwenye namba zifuatazo; mpesa 0755 953 887, tigo pesa 0717 396 253 namba zote jina ni Amani Makirita. Baada ya kufanya malipo tuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo au tuma ujumbe kwa wasap kwenye namba 0717396253 Ujumbe uwe na majina yako kamili na neno SEMINA YA HUDUMA KWA WATEJA. Pia bonyeza maandishi haya na jaza taarifa zako.
Ni wakati sasa wa kuongeza umakini kwenye biashara na kazi yako ili uweze kufikia mafanikio makubwa zaidi. Karibu tujifunze kwa pamoja.
TUPO PAMOJA,
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani.
makirita@kisimachamaarifa.co.tz