Rafiki yangu,

Makala hii nitaifanya fupi iwezekanavyo, kwa sababu sitaki kukuchosha. Nitagusia mambo matatu muhimu;



MOJA; ASANTE RAFIKI.

Kwanza napenda kutoa shukrani kwa marafiki zangu wote ambao mmekuwa mnasoma makala zangu, kwenye email na hata kwenye AMKA MTANZANIA, mnafanya sehemu ya kazi yangu kuwa na maana.

Pia nawashukuru sana katika hichi kipindi cha kuelekea kwenye SEMINA YA ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, nimekuwa natuma email nyingi kuliko ilivyo kawaida. Kama umepokea hii maana yake umenivumilia vya kutosha, maana wapo wengi walikereka na kuniambia niwaondoe kwenye email. Wengine walinipa mpaka vitisho vikali sana. 

Naelewa yote hayo na kazi yangu itaendelea.

MBILI; KARIBU KWENYE SEMINA.

Nachukua pia nafasi hii kuwakaribisha wale wote ambao wamejiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili kuweza kushiriki semina hii ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, elimu ambayo ni muhimu sana kwa kila mtu aliye makini na maisha yake. Ni imani kubwa sana mmejenga juu yangu, na mimi sitawaangusha. Nimejiandaa vya kutosha kwa semina hii, na nitajitahidi kadiri ya uwezo wangu kuhakikisha kila aliyewekeza fedha yake, basi anapata marejesho, yaani maarifa anayopata yanakwenda kumsaidia na aone faida.

Karibuni sana wanafamilia wapya kwenye KISIMA CHA MAARIFA, hii ni familia ya wanamafanikio. Tutaendelea kushirikishana na kujifunza mengi ndani ya familia hii inayokua kila siku.

Kuna watu waliofanya malipo ila hawajatuma ujumbe, tafadhali fanya kutuma ujumbe ili uweze kuingia kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

TATU; NAFASI 10 ZA MWISHO KABISA, KWA KULIPA NUSU.

Mwisho kabisa, kuhusu kujiunga na semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, mwisho ilikuwa jana tarehe 30/06/2017. Hivyo kama hukupata nafasi hiyo ya kujiunga jana, maana yake umekosa fursa hii ambayo haiji kutokea tena kwenye maisha yako.

Lakini kwa sababu wewe ni rafiki yangu, na umenivumilia kwa muda mrefu, nimeona siyo vyema ukose kabisa. Hasa kwa wale ambao walishindwa kulipa ada kamili ambayo ni tsh elfu 50.

Sasa leo hii, tarehe 01/07/2017 natoa nafasi kumi tu, tafadhali rafiki, KUMI TU, za kuweza kulipia na kushiriki semina hii ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, kwa kulipa nusu ya ada, ambayo ni tsh 30,000/= na inayobaki utamalizia ndani ya mwezi mmoja.

Hii ni nafasi ya kipekee kwa wale ambao wameniandikia mara nyingi kwamba wangependa sana kushiriki ila mambo yamewabana. Na najua hasa pale unapotaka kitu halafu ukabanwa, unakosa furaha kabisa.

Hivyo rafiki yangu, nafasi zipo 10, kama kweli hutaki kukosa semina hii, basi chukua hatua sasa hivi. Cha kufanya, nipigie simu kwanza, kwenye 0717396253 ili nikuambie kama nafasi zipo au la. Kama zitakuwepo nitakuambia ndiyo ulipie.

Nakuomba sana rafiki yangu, usitume malipo leo kabla hujanipigia simu kwanza, kwa sababu nafasi hizo zikiisha, sitaweza kukupokea zaidi ya hapo. Hivyo nipigie kwanza simu ndiyo nikuambie ulipie.

Rafiki, napenda uelewe siweki ukomo huu ili kukunyanyasa, ila ni teknolojia tunayotumia kwenye semina hii ndiyo ina ukomo. Kundi la wasap linaweza kubeba idadi ya watu 256 pekee, huwezi kuchukua zaidi ya hapo. Hivyo nafasi kumi zilizobaki ndiyo zinakamilisha 256 ya watu wanaopaswa kuwa kwenye kundi.

Rafiki, siwezi kukuhakikishia kama utapata nafasi hizo kumi, ninachoweza kukushauri, ni sasa hivi unavyosoma hapa, chukua simu yako, piga simu namba 0717396253 uliza kama nafasi zipo ufanye malipo.

Baada ya semina hii tutarudi kwenye utaratibu wetu wa kuwa nakutumia email mbili mpaka tatu kwa wiki. Email zitakazokupa maarifa na hatua za kuchukua ili kuwa na maisha bora na yenye mafanikio.

Kwa sasa uwe na wakati mwema.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA 
MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.