Habari za leo rafiki?

Kwa muda sasa nimekuwa nawasisitiza sana watu umuhimu wa kusoma vitabu. Na hii ni kwa sababu nimeona jinsi usomaji wa vitabu umebadili maisha yangu, na kuniwezesha kuwa mtu bora zaidi kila siku mpya kuliko nilivyokuwa jana yake.

Lakini kitu kimoja ambacho nimejifunza katika kipindi hichi ni kwamba watu wengi hawasomi vitabu. Kwa kifupi ni kwamba, hata wale wanaoomba au kununua vitabu, unapokuja kuwauliza baadaye kama wamesoma wanakuwa na sababu za kushindwa kusoma.

Ninapopata sababu hizi za watu kwa nini hawasomi vitabu, naanza kufikiri huenda zile semi tunazokuwa tunasikia kwamba ukitaka kumficha Mwafrika kitu kiweke kwenye maandishi. Hii ni kwa sababu naona jinsi watu wanahangaika kutafuta majibu, ambayo wangeweza kuyapata kwenye vitabu kama wangekuwa wasomaji.

Katika kipindi hichi nimekuwa nawadadisi watu kupata sababu za kwa nini wanashindwa kusoma vitabu. Karibu kila mtu ana sababu nyingi sana zinazomzuia kusoma kitabu. Na japo sababu hizi zinaonekana zina mashiko, zote zina majawabu, hivyo yeyote aliyedhamiria kweli, haziwezi kumzuia.

Baada ya kupata sababu hizi za wengi, nimekuwa najiuliza nawezaje kuwasaidia watu kusoma zaidi?

Na hapa ndipo nilipoweza kuja na program ya kusoma angalau kitabu kimoja kila mwezi, kitu ambacho kinawezekana kwa yeyote yule anayeamua kufanya hivyo.

Hapa nina maana kwamba, wewe rafiki yangu, unaweza kusoma angalau kitabu kimoja kila mwezi, na vitabu 12 kwa mwaka, bila ya shida yoyote ile.

Katika kufanikisha hilo, nimekusaidia kuondokana na sababu zinazowazuia wengi.

Kwa mfano wale wanaosema hawasomi kwa sababu hawana muda, kazi au biashara zimewabana sana, nimewapa mpango mzuri sana wa kusoma dakika kumi mara tatu kwa siku. Unapoamka dakika kumi, mchana dakika kumi na kabla ya kulala dakika kumi.

Wale ambao wanasema hawawezi kupata vitabu vya kusoma, au lugha ni changamoto, nimewaonesha jinsi ya kupata vitabu vya ile lugha wanayoiweza wao.

Na wale ambao wanasema hawana fedha ya kununua vitabu, nimewaonesha jinsi ya kupata vitabu vya kusoma bure kabisa.

Yote hayo nimekuelezea kwa kina kwenye kipindi chetu cha leo cha ONGEA NA COACH. Kwenye kipindi hichi pia nimekushirikisha program nzuri ya KUSOMA KURASA KUMI KILA SIKU, kama utaipenda karibu sana tusome pamoja.

Angalia kipindi hichi cha leo na uanze kusoma vitabu leo leo, kwa sababu ukisema unasoma kesho, unakuwa umeipoteza leo.

Unaweza kuangalia kipindi hichi kwa kubonyeza maandishi haya. Lakini pia unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini. Nakusihi uangalie kipindi chote, kwani mwisho nimekupa fursa nzuri ya kusoma vitabu na kujifunza.

Karibu sana kwenye program ya kusoma kurasa kumi za kitabu kila siku, kitu ambacho hakiwezi kumshinda yeyote, hata kama yupo kwenye wakati mgumu kiasi gani.

Kupata maelezo zaidi kuhusu program hii niandikie ujumbe kwenye wasap 0717 396 253 nitakutumia maelezo ya programu hii.

Nimalize kwa kauli hii muhimu; kama unajua kusoma lakini husomi vitabu, huna tofauti na mtu asiyejua kusoma, kwa sababu wote mnakosa hazina kubwa inayopatikana kwenye vitabu.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog