Habari rafiki?

Katika uwekezaji watu wengi wamekuwa wanafanya kosa moja kubwa mno. Kosa hili ni kufanya maamuzi ya uwekezaji kwa maneno ya watu wengine, watu ambao hata hawana uelewa mkubwa kwenye uwekezaji.

Watu wamekuwa wanawekeza kwa mazoea na kufuata wengine wanasema nini. Na hili limewapelekea kufanya uwekezaji ambao siyo mzuri kwao.

Watu wamekuwa wanabeba ushauri wa uwekezaji kama ambavyo wanaupokea, bila ya wao wenyewe kujifunza na kufanya maamuzi yanayowafaa wao.

Jambo muhimu sana kwenye uwekezaji ni kujifunza, hata kama unapata ushauri mzuri kiasi gani, lazima wewe mwenyewe, uchukue muda wako na kukaa chini na ujifunze. Kujifunza wewe mwenyewe ni hitaji muhimu sana la uwekezaji.

Mambo ya kujifunza kwenye uwekezaji yapo mengi. Unahitaji kujifunza kuhusu uwekezaji wenyewe, unahitaji kujifunza kuhusu mwenendo wa uchumi, unahitaji kujifunza kuhusu tabia za watu na mengine mengi.

Uzuri ni kwamba tunaishi zama ambazo kujifunza ni rahisi sana. kuna fursa nyingi za kujifunza kuhusu uwekezaji. Lakini wengi wamekuwa hawana muda au utayari wa kujifunza.

Na hawa ndiyo ninaowashauri wasiwekeze, kwa sababu watapata hasara.

Kwenye kipindi cha leo cha ONGEA NA COACH nimekushirikisha mfano wa mtu mmoja ambaye aliwekeza kwa kufuata ushauri wa watu na hatimaye kuishia kupata hasara.

Kupitia mtu huyu nimekushirikisha mambo muhimu sana ya kuzingatia kwenye uwekezaji ili uweze kufanikiwa. Kuanzia kiasi cha kuwekeza, maeneo ya kuwekeza na jinsi ya kufanya maamuzi sahihi ya uwekezaji.

Angalia kipindi hichi cha leo kama unataka kuwa mwekezaji mzuri. Na pia angalia kama umeshaanza uwekezaji.

Kwa wale ambao wanasema hawawezi kuwekeza kwa sababu wanafanya biashara, au hawana kipato cha kutosha, hichi kipindi ni chenu, angalia na uone ni jinsi gani unajidanganya wewe mwenyewe.

Kuangalia kipindi hichi kizuri cha leo bonyeza maandishi haya. Pia unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini.

Jifunze na fanyia kazi yale unayojifunza ili uwe mwekezaji bora kabisa.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

KWA NINI SIYO TAJIRI

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog