Moja ya kizuizi kikubwa sana katika safari ya mafanikio ni kuyaendea mafanikio huku ukiwa katika hali ambayo ni ya mazoea. Wengi tunapenda kufanya vitu vyetu tukiwa katika hali zetu za mazoea tunazozijiua, lakini kwenye mafanikio ukitaka kweli kufanikiwa mambo hayako namna hiyo.

Hiyo iko hivyo kwa sababu, unapoyaendea mafanikio yoyote yale, kwanza hiyo ina maana kwamba unaendea kitu kipya ambacho kitu hicho hujawahi kukifanya. Sasa kama unaendea kitu kipya, kwa vyovyote vile ili ukipate hutakiwi kuwa katika hali ya mazoea ambayo unayo kila wakati.

Itafika muda au kipindi ambacho wewe utalazimika kufanya vitu ambavyo hujawahi kuvifanya, kwa sababu ndivyo mafanikio yanavyotaka. Na ukiangalia ili uweze kufikia mafanikio ni lazima ufanye vitu vipya na si vile ulivyovizoea.

vitabu softcopyIkiwa kama unataka kufanikiwa na unataka kuendelea kuishi katika hali zile zile na maisha yale yale ambayo uliyoyazoea, haiwezi kutokea kwako ukafanikiwa. Kama nilivyosema mafanikio yanataka sana uwe katika hali ambayo si ya mazoea kama ilivyo kawaida yako.

Hata kama kuna kitu ambacho unakipenda sana na unataka kukifanikisha na kwa kuwa kitu hicho hujawahi hata siku moja kukipata, utalazimika kuishi maisha ambayo si ya mazoea, maisha yaliyojaa nidhamu, ambapo maisha hayo yatakulazimisha wewe upate kitu hicho.

Unaposema unatafuta mafanikio ya aina fulani, ujue kabisa unaiendea njia mpya ambayo hujawahi kuipita. Kwa hiyo kwa chochote ambacho utakua unakutana nacho kwenye njia hiyo iwe miiba au kitu gani, kubali kuvumilia, kwa sababu ni njia mpya.

Usiwe mwepesi sana wa kuanza kulalamika na kutaka kuishi maisha yako ambayo umeyazoea wakati unatafuta mafanikio. Hautaweza kufanikiwa nakufikia mafanikio yako kama unataka kuishi maisha yako ya mazoea wakati unatafuta mafanikio.

Yapo mambo mengi sana ambayo unatakiwa kujikana ili uweze kutimiza mafanikio yako. Ikitokea hautaweza kujikana na kuchukulia kila kitu kitakwenda sawa, uwe na uhakika utashindwa tu kila wakati kufikia mafanikio yako.

Ni asili ya binadamu kutokujisikia katika hali ya mazoea pale inapotokea tunafanya jambo jipya. Wengi huwa wanajisikia hawako huru nakuona kama wanabanwa na kutaka kurudi kule walikotoka.

Sasa ikiwa kama inakutokea hivi, kila ukitaka kufanya jambo jipya la mafanikio yako unashindwa kujibana na kurudi kule ulikotoka kwa kuishi maisha yale yale ya mazoea, kufanikiwa kwako kutakuchukua muda mrefu sana.

Kuyaendea mafanikio unapaswa uelewe unatakiwa kujikana sana, kwa mambo mengi. Unatakiwa usijipende sana, unatakiwa usiishi  katika ‘comfotable zone’ kabisa ili kutimiza ndoto zako, lakini kinyume cha hapo utaendelea kuishi maisha ambayo ni ya ndoto.

Wale wote unawaona washindi katika maisha, inafika kipindi wanafanya vitu ambavyo hata hawapendi, lakini wanafanya hivyo kwa sababu wanajua ndio hatua ya kuwasaidia kuweza kufikia mafanikio yao kwa kiasi kikubwa.

Unatakiwa kukabiliana na hali mpya kila siku ili uweze kutengeneza mafanikio yako. Ukishindwa kabisa kukabiliana na hali mpya na ukategemea sana kuishi maisha yale yale, kushindwa katika safari ya mafanikio yako kutakuhusu.

Usikibali ukashindwa kuyafikia mafanikio yako kwa sababu tu unayaendea mafanikio katika hali ya mazoea. Ni hatari sana kufanya vitu katika mazoea yako uliyoyazoea, kwani ukifanya hivyo utabaki hapo ulipo.

Najua unawajua watu ambao miaka nenda rudi maisha yao yapo pale pale, kama ulikuwa hujui sababu mojawapo iliyowabakisha hapo wamekuwa ni watu wa kuishi sana katika hali ya mazoea kuliko ambavyo unafikiri.

Ni sumu kubwa sana katika kufikia mafanikio yako kama unaishi kwa mazoea na kwa kufanya hivyo utapoteza mafanikio yako kwa sehemu kubwa sana. Anza sasa kuyasaka mafanikio kwa kujiepusha kuishi kwa maozea na utafanikiwa.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; http//www.amkamtanzania.com

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com