Kama unataka kuwa mjasiriamali ambaye una mafanikio, kimsingi hutakiwi kwenda kiholela au kwenda kwa kukurupuka kama unavyotaka wewe. Kuna sheria au  misingi ambayo unatakiwa uifate ili uweze kufanikiwa kwa viwango vya juu.

Tatizo la wajasiriamali wengi wanajikuta ni watu wa kukwama kwa sababu ya kushindwa kuzifata sheria hizo za muhimu ambazo kwa kawaida ukizifuata ni lazima zikupe mafanikio ambayo unayoyataka.

Najua hapo ulipo una kiu kubwa sana ya kutaka kufanikiwa hasa kwa kile ambacho unachokifanya. Pamoja na kwamba una kiu hiyo, je ni kuuulize, unazijua sheria muhimu au kanuni muhimu ambazo ukiwa kama mjasiriamali unatakiwa uzifuate na zikufanikishe?

Kama huzijui sheria hizo naomba usitoke hapa ulipo , kaa nami hapa tujifunze kwa pamoja sheria za msingi ambazo ukizifuata sheria hizo kwa vyovyote ni lazima zitaweza kukusaidia kukufanikisha na kukupa mafanikio makubwa sana uyatakayo.

vitabu softcopy

 

Sheria ya 1; Zingatia mambo ya muhimu.

Sheria ya kwanza kwenye ujasiriamalia ambayo unatakiwa uifate na kuifatilia kikamilifu ni kuzingatia mambo ya muhimu kwenye biashara ambayo unaifanya. Kama lengo lako ni kutengeza faida na kukuza biashara zingatia hilo sana.

Kwa kawaida kwenye biashara kuna mambo mengi sana, kama changamoto, kupata hasara au kukimbiwa na wafanya kazi, lakini yote hayo yanapotokea kwako yasikutishe, kikubwa kwako zingatia mambo ya msingi yatakayokusaidia kukabiliana na changamoto hiyo na sio kulaumu.

Ikiwa kama jicho lako badala ya kuzingatia mambo ya msingi katika biashara na linazingatia mambo mengine ya hovyo kama lawama au kulogwa hapo uwe na uhakika utakwama hata kama hutaki. Sheria hii inakutaka kuzingatia kile unachokitaka kama kuikuza biashara na kadhalika.

Sheria ya 2; Usijilinganishe na watu wengine.

Unapokuwa kwenye biashara, jitahidi sana kukimbia mbio zako mwenyewe. Jitahidi kufanya mambo yatakayokusaidia kukuza biashara yako. Acha kufanya maamuzi ya kujilinganisha na watu wengine kwenye kile ambacho unachokifanya.

Ukiwa ni mtu wa kuiga biashara za wengine na wewe kutaka kuzifanya na ukasahau kufanya kile ambacho kilikuwa moyoni mwako muda utafika tu na utakwama.  Jitahidi sana kuwa bora kuliko jana yako kwenye biashatra uliyonayo.

Watu wengi kwenye maisha na biashara wanakwama kwa sababau ya kujilinganisha na watu wengine na kusahau kuboresha kazi au biashara zao. Jitahisdi sana kujenga mafanikio ya biashara yako wewe mwenyewe na si kwa kuiga iga tu, utapotea.

Sheria ya 3; Jifunze kuwa na tahadhari.

Unapokuwa mjasiriamali ni muhimu sana kujifunza kuwa na tahadharai. Hapa nikiwa na maana katika kila maamuzi unayochukua maaumizi hayo kuwa nayo makini. Usiwe mtu wa kukurupuka katika kuchukua maaumuzi utakwama.

Wajasiamali walio wengi na wenye mafanikio ni makini katika hili na linawasaidia kutokujiingiza katika hasara ambazo hazina sababu yoyote. Na wewe unatakiwa kuwa na kitu kama hicho ili kikusaidie kuweza kufanikiwa na kupiga hataua za kimafanikio.

Kwa kifupi, hizi ndio sheria za msingi ambazo unatakiwa uzijue ili kuwa mjasiamali mwenye mafanikio kwenye maisha yako.

Fanyia kazi sheria hizi za msingi na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.

Tunakutakia kila la kheri na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku kujifunza maisha na mafanikio.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,

Ni wako rafiki katika mafanikio,

Imani Ngwangwalu,

Mshauri wa mafanikio, mwandishi na mjasiriamali,

Tovuti; http://www.amkamtanzania.com,

Mawasiliano; +255 767 048 035, +255 713 048 035,

Email; dirayamafanikio@gmail.com