Rafiki yangu mpendwa,

Zama tunazoishi sasa ni zama ambazo kila mtu anapaswa kuingia kwenye biashara. Iwe mtu anapenda au hapendi, kujihusisha na aina yoyote ya biashara zama hizi ni muhimu kwa sababu maisha yanakuwa magumu na vipato havitoshelezi.

Pia kwa kuwa zama tunazoishi ni zama za watu kuwa na uhuru watakavyo, njia ya uhakika ya kujijengea uhuru wa kipato ni kuwa na biashara.

Kama ilivyo kwenye kila kitu kwenye maisha yetu, biashara hazijawahi kukosa changamoto. Lakini pia changamoto za kibiashara zama hizi zimekuwa kubwa na kali, kiasi kwamba kama biashara haijajengwa vizuri haitaweza kuvuka changamoto hizi.

Na ushahidi upo wazi, tafiti nyingi zinazofanywa kwenye biashara, zinaonesha kwamba biashara 8 kati ya 10 zinazoanzishwa zinakufa ndani ya mwaka mmoja baada ya kuanzishwa. Unaweza kuona ni jinsi gani mazingira ya kibiashara ni magumu na wengi wanapotezwa.

Kila mfanyabiashara, na yeyote anayefikiria kuingia kwenye biashara, kuna changamoto kubwa tano za biashara kwenye zama tunazoishi sasa. Changamoto hizi ni za kipekee kwa zama tunazoishi sasa, hivyo wale ambao wamekuwa kwenye biashara kwa zaidi ya miaka 20 wanaweza kuwa hawazijui, kwa sababu miaka 20 iliyopita, changamoto hizi hazikuwa tatizo kubwa.

095a5b996f7db11bfe3b1d93a17b444b.0

Leo tunakwenda kujifunza changamoto kubwa tano za kufanya biashara zama hizi na mwisho nitakushirikisha kitu kimoja muhimu kufanya ili kuiokoa biashara yako na changamoto hizo.

Zifuatazo ni changamoto kuu tano za kufanya biashara zama hizi;

MOJA; USHINDANI MKALI NA USIO NA HURUMA.

Changamoto kubwa ya kwanza ya kufanya biashara zama hizi ni ushindani mkali, na usio na huruma. Elewa hapo, siyo tu kwamba ushindani ni mkali, bali pia ushindani hauna huruma, ni ushindani wa kikatili, ambao unaweza kukuondoa kabisa kwenye biashara bila ya kujali umeweka juhudi kiasi gani.

Kila biashara unayofanya sasa, kila mtu anaweza kuifanya. Ukijitahidi na kuwa mbunifu, ukaanzisha biashara ya tofauti, ambayo wengine hawajaijua, wakishaona unafanya na unatengeneza faida, na wao watakuiga, na kibaya zaidi watakuja kufanyia pale ambapo na wewe unafanya. Unaona jinsi ushindani ulivyo wa kikatili? Huna namna ya kumzuia yeyote asiige biashara yoyote uliyoibuni wewe.

Pia wateja wapo tayari kukuacha pale anapotokea mwingine anayewahudumia vizuri kuliko wewe, hata kama ulishawasaidia wateja hao huko nyuma. Wateja wengi hawajali sana kuhusu biashara yako, bali wanajali kuhusu kile wanachopata wao.

Ushindani wa biashara zama hizi ni mkali, na unaendelea kuwa mkali na wa kikatili, unahitajika kuwa imara sana kama unataka kufanikiwa kwenye biashara kwa zama tunazoishi sasa.

MBILI; MUDA NI MFUPI NA YA KUFANYA NI MENGI.

Ukiingia kwenye biashara zama hizi, unahitajika kufanya karibu kila kitu kwenye biashara yako. Na hata kama utakuwa na wasaidizi, bado utahitajika kufuatilia kwa makini kila ambacho wanakifanya. Hivyo unajikuta una mambo mengi ya kufanya, lakini muda ni mfupi.

Kadiri biashara yako inavyokua, ndivyo mambo ya kufanya yanapokuwa mengi zaidi. Na hapo bado wateja wako hawaelezi mpangilio wako wa muda. Mteja anaweza kukutafuta muda wowote akitaka umtatulie changamoto yake.

Unapoingia kwenye biashara zama hizi, ni kama unaondoa kabisa uhuru wako kwenye muda wako, kwa sababu yeyote anaweza kutumia muda wako kwa namna anavyotaka yeye, kuanzia wateja mpaka wasaidizi wako kwenye biashara. Pia siku zitakuwa ndefu sana na uchovu mkubwa, lazima uwe tayari kusambaza muda wako kiasi hicho ili kupiga hatua kibiashara.

SOMA; Tofauti Ya Kusudi, Dhumuni Na Lengo La Biashara Na Jinsi Ya Kutumia Hayo Matatu Kukuza Biashara Yako.

TATU; BIDHAA ZINAPITWA NA WAKATI HARAKA.

Nimekuwa naona watu wanalalamika kwamba makampuni ya simu yanatoa matoleo mengi mapya ya simu ndani ya muda mfupi. Nimekuwa nawaambia hiyo ndiyo njia pekee ya makampuni hayo kubaki sokoni. Kwa sababu bidhaa mpya inayotoka leo, haina muda mrefu kabla haijapitwa na wakati.

Kwanza bidhaa mpya inapotoka, ikiwa na vitu vipya, wengine wanaiga bidhaa hiyo, hivyo soko linakuwa na bidhaa hiyo nyingi. Pili vinagunduliwa vitu vipya na njia bora za kufanya kile ambacho wewe tayari umeshakitoa kikiwa hakina njia hizo mpya, hivyo inabidi uzalishe kipa inachohusisha njia hizo mpya.

Zama hizi hutakaa na bidhaa au huduma moja kwa muda unaotaka wewe, mambo yanabadilika kwa kasi na bidhaa au huduma yoyote unayouza leo, miaka mitano inayokuja itakuwa imefutika kabisa. Ni muhimu sana wewe kama mfanyabiashara kuwa mbele ya mabadiliko haya, kubadilika kabla mambo hayajabadilika.

NNE; WATEJA WANA HARAKA KUPITILIZA.

Kwa zama tunazoishi sasa, watu wanataka kitu, ambacho walikuwa hawakijui, lakini walikitaka jana. Yaani watu wana haraka kupitiliza, watu hawana subira kabisa. Uwepo wa wafanyabiashara wengi na wingi wa huduma, na hata usumbufu unaowakumba watu, wamekuwa na haraka na wasio na uvumilivu.

Hivyo mtu kusubiri muda mfupi kwenye zama hizi ni msamiati ambao wengi wameshaanza kuusahau. Kwa mfano mtu ambaye hajawahi kutumia mtandao kwenye simu yake, anapopata mtandao kwa mara ya kwanza, hata kama utakuwa taratibu atavumilia. Lakini anapokuja kukutana na mitandao unayokwenda kasi, anazoea kasi ile. Siku akikutana na mtandao unaokwenda taratibu, atashangaa kama vile hajawahi kukutana na mtandao wa aina hiyo, na hatachukua muda kusubiri, atabadili na kutafuta mtandao unaokwenda kasi.

Unahitaji kuwa tayari kwenda na kasi hii ya wateja ili kuweza kuwahudumia kabla hawajakuacha na kwenda kwa wafanyabiashara wengine.

TANO; WATEJA WANAFIKIRI WANAJUA KILA KITU.

Kabla mteja hajanunua unachouza, jihakikishie kitu kimoja, tayari ‘ameshagoogle’ kitu hicho. Wateja wa zama hizi wanafikiri wanajua kila kitu, hivyo unapaswa kuwa makini sana.

Kwanza unapaswa kuijua biashara yako vizuri sana, unapaswa kuijua nje ndani kiasi kwamba anayefikiri anaijua tu juu juu hataweza kukuteteresha. Maana kama huijui biashara yako, mtu mwenye uelewa wa juu juu kwa vitu alivyotafuta ‘google’, anaweza kukufanya ujione hujui unachofanya.

Pili usiwachukulie watu kama hawajui, kwa kujiona wewe pekee ndiye unayejua kuhusu biashara yako, wape muda wa kuwasikiliza, kisha waelimishe kile ambacho ni sahihi kuhusu biashara yako. Usijifanye kama wewe ndiye unayejua kila kitu na wao wanapaswa kusikiliza, bali mnapaswa kujadiliana kwa namna gani mteja atanufaika.

Wateja wa zama hizi wanafikiri wanajua kila kitu kwa sababu ‘wameshagoogle’, wape nafasi ya kujieleza na waelimishe vizuri zaidi.

Hizo ndiyo changamoto kubwa za biashara kwenye zama unazoishi sasa rafiki, naamini umeweza kuzihusisha na biashara unayofanya wewe, ukaona jinsi gani zinaathiri biashara yako. Pia nina imani umeshaanza kuona kipi cha kufanye kwenye biashara yako ili kila changamoto isiwe tatizo kwako.

Kitu kimoja muhimu kufanya ili kuiokoa biashara yako na changamoto hizo tano.

Changamoto za biashara ni nyingi, hizo tano nimekushirikisha hapo juu ni zile kubwa na zinazoua biashara nyingi. Lakini changamoto ni nyingi zaidi ya hapo. Na kwa kila changamoto, kuna kitu cha kufanya ili biashara iendelee kuwa salama na kujiendesha kwa mafanikio.

Lakini ipo kitu kimoja ambacho ukiweza kukifanya vizuri kwenye biashara yako, kinatatua kila aina ya changamoto kwenye biashara. Yaani ni sawa na kuwa na dawa moja ambayo inatibu kila aina ya ugonjwa. Kwa binadamu ni ngumu kuwa na dawa ya aina hiyo, lakini kwenye biashara, dawa hiyo ipo na tutakwenda kujifunza hapa kuhusu dawa hiyo.

Dawa moja inayoweza kutibu kila aina ya changamoto za kibiashara ni biashara KUTENGENEZA FAIDA. Kama biashara haitengenezi faida, changamoto haya ikiwa ndogo kiasi gani, ni rahisi kuua biashara hiyo. Lakini kama biashara inajiendesha kwa faida, hata kama changamoto ni kali, itaweza kusimama na kufanikiwa.

Hivyo kitu kimoja unachopaswa kufanya kama mfanyabiashara, ni kuhakikisha biashara yako inajiendesha kwa faida. Na kadiri faida inavyokuwa kubwa, ndivyo kuvuka changamoto na kufanikiwa kibiashara kunakuwa rahisi.

Lakini pia kutengeneza faida kwenye biashara siyo rahisi, kwa sababu changamoto tulizojifunza hapa zinazuia biashara kujiendesha kwa faida pia.

Hivyo mimi rafiki yako, nimekuandalia njia bora sana ya kuongeza faida kubwa kwenye biashara yako. Ipo njia ya kuongeza faida kwa zaidi ya asilimia 50 kwenye biashara yako.

Je ungependa kujua njia hii? Basi unayo nafasi ya kuijua njia hii kuanzia tarehe 5 julai 2018.

HABARI NJEMA KWA WAFANYABIASHARA WOTE.

Nimeandaa semina ya biashara inayokwenda kwa jina; NJIA TANO ZA KUKUZA BIASHARA YAKO, Ongeza Faida Kwa Zaidi Ya Asilimia 50 Ndani Ya Mwaka Mmoja.

Hii ni semina ambayo kila mfanyabiashara, na hata mfanyabiashara mtarajiwa atajifunza jinsi ya kuongeza faida kwenye biashara yake kwa zaidi ya asilimia 50 ndani ya mwaka mmoja.

Watu wengi wamezoea faida kuwa asilimia 10 na ikizidi sana asilimia 20 kwa mwaka. Kwenye semina hii unakwenda kujifunza mbinu 50 ambazo unakwenda kuzifanyia kazi kwenye biashara yako na faida itaongezeka kwa zaidi ya asilimia 50.

Semina hii utajifunza kwa namna ya kuchukua hatua, hivyo haitakuwa ya kujua tu, bali utakuwa na kila hatua ya kuchukua.

MAELEZO ZAIDI YA SEMINA HII NI KAMA IFUATAVYO;

Katika semina hii muhimu sana kuhusu biashara, tutakwenda kujifunza yafuatayo;

UTANGULIZI; Umuhimu wa biashara na ukuaji wa biashara kwenye zama tunazoishi sasa, maeneo matatu muhimu sana kwenye ukuaji wa biashara yako.

NJIA YA KWANZA; WATEJA TARAJIWA, njia 10 za kuwafikia wengi zaidi na biashara yako.

NJIA YA PILI; KIASI CHA WATEJA TARAJIWA WANAOKUWA WATEJA HALISI, njia 10 za kuwashawishi wanaoijua biashara yako kuwa wateja.

NJIA YA TATU; IDADI YA MIAMALA AMBAYO MTEJA MMOJA ANAFANYA, njia 10 za kuongeza idadi ya miamala mteja anayofanya.

NJIA YA NNE; WASTANI WA FEDHA ANAYOLIPA MTEJA, njia 10 za kuongeza wastani wa malipo anayofanya mteja kwenye biashara yako.

NJIA YA TANO; KIASI CHA FAIDA KWENYE KILA UNACHOUZA, njia 10 za kuongeza kiasi cha faida kwenye kila unachouza.

HITIMISHO; KANUNI SAHIHI YA KUTUMIA ILI KUKUZA BIASHARA YAKO KWA KUONGEZA FAIDA KWA ZAIDI YA ASILIMIA 50 KWA MWAKA.

Njia hizi tano za kukuza biashara zinategemeana, na kama ambavyo tutajifunza kwenye semina hii inayokuja, zote zinafanyika kwa pamoja na siyo kwamba unachagua njia moja na kuacha njia nyingine.

Nikukaribishe sana rafiki yangu kwenye semina hii ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, ni semina ambayo imekuja wakati sahihi kwako kwa sababu kila biashara zina changamoto na kipindi hichi, changamoto zimekuwa nyingi zaidi.

Semina hii itafanyika kwa njia ya mtandao, kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo unaweza kushiriki semina hii ukiwa popote pale, bila ya kuhitajika kusafiri au kuacha shughuli zako. Unachohitaji kufanya ni kutenga muda kwenye siku yako ya kufuatilia masomo haya na kisha kufanyia kazi.

Semina hii nzuri itafanyika mwezi julai 2018, itafanyika kwa siku saba, kuanzia tarehe 05/07/2018 mpaka tarehe 11/07/2018. Hizi zitakuwa ni siku saba za kujifunza mambo ambayo yataifanya biashara yako iweze kukua kwa kiasi kikubwa sana.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii unahitaji kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Ukishakuwa mwanachama huhitaji kulipa gharama za ziada kushiriki semina hii.

Kama bado hujawa mwanachama, unapaswa kulipa ada ya mwaka ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo kwa sasa ni shilingi elfu hamsini (50,000/=). Hii ni ada ya mwaka mzima, ambayo inakupa nafasi ya kuendelea kujifunza kila siku kwa mwaka mzima tangu ulipolipia.

Ili kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA, tuma ada, tsh 50,000/= kwa MPESA 0755 953 887 au TIGO PESA/ AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina yatakuja AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako kamili na email yako kisha utaunganishwa kwenye kundi la KISIMA CHA MAARIFA na kuendelea kupata mafunzo.

Ili upate nafasi ya kushiriki semina hii, inabidi uwe umejiunga na KISIMA CHA MAARIFA kabla ya tarehe 05/07/2018. Hivyo mwisho kabisa wa kujiunga ili unufaike na semina hii vizuri itakuwa tarehe 03/07/2018

Karibu sana kwenye semina ya UKUAJI WA BIASHARA YAKO, uondoke na vitu vya kwenda kufanyia kazi kwenye biashara yako ili iweze kukua kwa kiasi kikubwa na uweze kufikia malengo makubwa uliyojiwekea kwenye maisha yako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Rafiki, kama ungependa kujifunza zaidi kupitia mafunzo ninayotoa, karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Hii ni blog maalumu inayoenda na kundi maalumu la wasap ambapo kila siku unajifunza na kuhamasika, kila wiki kuna madarasa ya mafanikio na kila mwaka kuna semina tatu nzuri sana kwa mafanikio yako.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwa wasap kwenda namba 0717396253 au fungua hapa;  www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha

Kujiunga na Kundi la kusoma vitabu; www.amkamtanzania.com/kurasa

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Usomaji