Rafiki yangu mpendwa,

Kama ambavyo nimekuwa nakupa taarifa kwa muda sasa, tarehe 03/11/2018 tutakuwa na semina yetu kubwa ya mwaka, SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

Hii ni semina ambayo tunakutana watu wote ambao tuna kiu ya mafanikio makubwa, watu ambao tunajua tunaweza kufanya zaidi ya pale tulipo sasa na tupo tayari kujitoa ili kupiga hatua zaidi.

Ni tukio linalotokea mara moja kwa mwaka, tukio la wanamafanikio, ambalo linakwenda kuangalia changamoto kubwa tunazokutana nazo kwenye safari yetu ya mafanikio na kisha kutuwezesha kuondoka na mpango tunaokwenda kuufanyia kazi.

Safari ya mafanikio haijawahi kuwa rahisi kwa yeyote yule, ukiachana na zile hadithi za kwenye vyombo vya habari, kwamba mtu alianzia chini na sasa ni tajiri, kuna sehemu ndefu sana huwa inarukwa hapo katikati. Ambapo wengi wanaoanzia chini wanaishia hapo katikati.

Moja ya maeneo tutakayoyagusia sana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ni changamoto zinazowafanya wengi waishie njiani kwenye safari hii ya mafanikio.

Katika kuwahudumia watu wengi ambao tupo pamoja kwenye safari hii ya mafanikio, na katika kupitia changamoto ambazo washiriki wa semina wameandika ndiyo zinawasumbua, nimeweza kugundua changamoto kubwa kumi ambazo watu wengi wanazipitia kwenye safari hii ya mafanikio.

Hivyo kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, tutakwenda kuzijadili changamoto hizi na kutengeneza suluhisho ambalo tunakwenda kulifanyia kazi na kuliishi.

SAMSUNG CAMERA PICTURES
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2017

Zifuatazo ni changamoto kumi tutakazokwenda kuzipatia majibu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

  1. Kukuza kipato na kuongeza mifereji ya kipato na kufikia uhuru wa kifedha.

Nani asiyependa fedha zaidi, hasa kwenye zama hizi ambazo gharama za maisha zinaenda juu kila siku? Kama chanzo chako cha kipato ni kimoja, hasa kama ni mshahara, haupo mahali pazuri, unahitaji kuwa na vyanzo mbadala vya kipato. Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018, tutajifunza njia mbadala za kipato unazoweza kufanyia kazi na ukaweza kuongeza kipato chako na hata kujijengea uhuru wa kifedha.

  1. Kuanzisha, kupata mtaji, kusimamia na kukuza biashara.

Watu wengi wanapenda kuanza biashara, lakini hawajui waanzie wapi, wengine wana wazo lakini hawana mtaji, wengine wana wazo na mtaji lakini wamekwama, biashara haikui. Kila hatua ya biashara ina changamoto zake, hivyo usipojipanga unaweza kujiambia biashara ni ngumu na haikufai wewe.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018, tunakwenda kujadili hatua hizi za biashara na jinsi ya kutatua changamoto zake ili uweze kufanikiwa zaidi.

  1. Kutengeneza mfumo wa biashara kujiendesha yenyewe na kusimamia mradi uliopo mbali.

Watu wengi huwa wanafikiria kwamba wakiingia kwenye biashara basi wanakuwa na uhuru na maisha yao, wanaweza kufanya chochote wanachotaka kwa muda wao. Ni mpaka wanapoanzisha biashara zao ndipo wanagundua kwamba wameajiriwa na bosi mbaya kuliko wote duniani. Kwa sababu bosi huyo anakuwa hana muda wa kazi na hana mapumziko.

Watu wengi wanaanzisha biashara kwa lengo la kuzimiliki, lakini biashara zinaishia kuwamiliki, wao wanakuwa ndiyo biashara na biashara inakuwa ndiyo wao. Hawawezi kuondoka kwenye biashara yao na ikabaki salama.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018 tutakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza mfumo wa biashara kujiendesha yenyewe. Pia tutajifunza jinsi ya kusimamia mradi uliopo mbali, maana watu wengi wameumizwa sana kwa kufanya miradi iliyopo mbali na wao, hasa miradi ya kilimo.

  1. Kupata wasaidizi bora na kuandaa viongozi wa kushika nafasi kwenye biashara inayokua.

Changamoto nyingine kubwa sana kwenye biashara ni pale inapoanza kukua, kwa sababu biashara huwa zinakuwa kwa kasi kuliko mmiliki wa biashara na hata wale wanaomsaidia. Pale biashara inapokua kuliko mmiliki, mmiliki bila ya kujua, anaizuia isikue, labda yeye au wale wanaomsaidia kwenye biashara hiyo.

Ili kuepuka hili, lazima kila biashara iwe na mpango wa kuwaandaa viongozi wa kuiwezesha biashara hiyo kukua zaidi. Viongozi hao ndiyo watachochea biashara kukua zaidi na kuiepusha kufa.

Kama biashara yako inakua na unakutana na changamoto za kukosa wasimamizi sahihi, kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018 tutajifunza njia bora ya kuandaa viongozi ambao watasimamia vizuri biashara inayokua.

  1. Kupangilia muda na kuweka vipaumbele.

Linapokuja swala la muda, kuna habari nzuri, moja ni mbaya na moja ni nzuri.

Habari mbaya ni kwamba, hakuna muda utakaoongezwa siku zozote za karibuni, masaa ya siku yataendelea kuwa yale yale ambayo ni 24, siku za juma zitaendelea kuwa 7 na majuma ya mwaka 52. Hakuna nyongeza, hata uwe nani au ufanye nini.

Habari nzuri ni kwamba, wewe ndiye mpangiliaji mkuu wa muda wako, na ndani ya masaa yako 24 unaweza kupata muda wa kufanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwako. Hata kama umeajiriwa na kazi zako zinakubana sana, bado unaweza kupata muda wa kufanya yale muhimu.

Hivyo kama unajiambia huna muda, njoo kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 na utaondoka na mkakati wa kukuwezesha kuwa na muda zaidi kwenye siku yako na kufanya yale ambayo ni muhimu.

  1. Masoko kwenye bidhaa za kilimo.

Eneo la kilimo lina changamoto kubwa sana, kuanzia kwenye kilimo chenyewe, kwenye mazingira yetu ambayo maji ya uhakika ni changamoto, kupata mbegu sahihi na pembejeo nyingine ni kazi kubwa.

Lakini ugumu zaidi unakuja pale unapokuwa umevuna, soko nalo linakuwa shida. Unakuwa umevuna kipindi ambacho kila mtu amevuna na hivyo soko kuwa baya na hivyo kupata hasira.

Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 tutakwenda kujadili njia mbalimbali za kupata masoko kwa bidhaa za kilimo, na hata ufugaji pia.

  1. Kushinda kukatishwa tamaa na kukata tamaa mwenyewe.

Kuna maadui wawili wakubwa wa mafanikio yako, na maadui hawa wana nguvu kubwa sana, usipowajua na kuweza kuwadhibiti, hutaweza kupiga hatua yoyote kubwa kwenye maisha yako.

Adui wa kwanza ni wewe mwenyewe, utaweka mipango mikubwa kwenye maisha yako, halafu wewe mwenyewe utaanza kujihukumu, utaanza kujiambia nini kinakufanya uone unaweza, utaanza kujiambia huwezi au haiwezekani, na haitakuchukua muda utakata tamaa.

Adui wa pili ni watu wako wa karibu, wale wanaokuambia wanakujua sana, na hivyo unapopanga makubwa wanakuambia acha kujidanganya na kujisumbua, huwezi, haiwezekani, na walijaribu wengine kama wewe na hawajafika popote. Hawa ni watu ambao unawaamini sana, hivyo maneno yao kwako yatakuwa na uzito, hivyo ni rahisi kukukatisha tamaa.

Ili kuweza kuwashinda maadui hawa wakubwa wawili, karibu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 na utajifunza mbinu sahihi za kuwasambaratisha kabisa maadui hao wasifikie ndoto zako kubwa na kuziharibu.

  1. Jinsi ya kujitofautisha na kuondokana na ushindani mkubwa wa kibiashara.

Kuna njia mbili za kuingia kwenye biashara,

Njia ya kwanza ni umeona wengine wanafanya biashara fulani, ukaona inalipa na wewe ukaingia kufanya.

Njia ya pili ni unapata wazo la tofauti, ambalo bado halijafanywa na hivyo kuwa wa kwanza kuanzisha biashara ya aina hiyo.

Kwa njia zote hizo mbili, mwisho wa siku unaishia kukaribisha ushindani, kwa sababu ukiingia kwenye biashara ambayo tayari wengine wanafanya, unajipeleka kwenye ushindani. Na ukianzisha biashara mpya, na wengine wakaona inafanya vizuri, watakuiga.

Unahitaji kuwa na njia ya kukutofautisha, njia ya kuifanya biashara yako kuwa ya kipekee na kuwafanya wateja waache wafanyabiashara wengine wote na waje kwako wewe tu.

Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018 utajifunza njia ya kujitofautisha na kutengeneza upekee wako kwenye biashara au chochote unachofanya.

  1. Kupata wabia sahihi kwenye biashara.

Watu huwa wanasema kosea kujenga nyumba lakini usikosee kuoa au kuolewa, maana maisha yako yatakuwa magumu.

Na mimi nina cha kuongeza, kosea vyote kwenye maisha, lakini usikosee kuchagua mbia wa biashara, kwa sababu utayapoteza maisha yako.

Hebu fikiria wewe unaamini kwenye wazo la biashara ulilonalo, hupati usingizi usiku, unafanya kazi usiku na mchana, unajinyima, unainyima familia yako ili biashara yenu ikue, halafu mwenzako anakuja kuondoka na fedha za biashara na kuzitumia vibaya. Na kama hilo halitoshi, anakuachia wewe madeni.

Unahitaji kuwa makini sana unapochagua mbia wa biashara. Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018 tutajifunza sifa muhimu za kuangalia pale unapochagua mtu wa kushirikiana naye kwenye biashara.

  1. Kutengeneza mahusiano bora ya kindoa na familia kwa ujumla.

Kuna changamoto moja kubwa ambayo nimeona inawaandama wengi wanaochagua kuishi maisha ya mafanikio. Kwa sababu wanabadili mfumo wao wa maisha kabisa, kitu cha kwanza kinachoanza kutikisika ni ndoa zao. kwa sababu wenza wao waliwasha wazoea kwa tabia fulani za nyuma, sasa anakuja na tabia mpya ambazo hawazielewi.

Bila ya kuwa makini, juhudi zako za kufanikiwa zaidi zinaweza kuleta matatizo kwenye ndoa yako, au ndoa yako ikaleta matatizo kwenye mafanikio yako. Hivi ni vitu viwili ambavyo kila mtu anapaswa kwenda navyo vizuri na kwa umakini.

Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 tutakwenda kujifunza njia bora ya kutengeneza mahusiano bora ya ndoa na familia kwa ujumla. Kwa sababu mahusiano haya yakishakuwa bora, hakuna kinachoweza kukuangusha.

Rafiki yangu mpendwa, kama lolote kati ya hayo 10 linakuhusu wewe moja kwa moja, fanya uwezavyo kuhakikisha unashiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018. Kwa sababu kwenye semina hii utajifunza njia sahihi ya kukabiliana na changamoto unazopitia na kuweza kufikia mafanikio makubwa.

KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.

Rafiki, tarehe 03/11/2018 ndiyo siku ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, semina hii itafanyika kwenye moja ya hoteli zilizopo jijini dar es salaam.

Itakuwa ni semina ya siku nzima, kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa moja jioni. Yatakuwa ni masaa 12 ya kujifunza, kujuana na wengine, kuhamasika na kuweka mkakati wa kwenda kufanyia kazi kwa mwaka mzima.

Ada ya kushiriki semina hii ni tshs 100,000/= (laki moja) ada ambayo itajumuisha huduma zote za siku ya semina, kuanzia chai, chakula cha mchana, vitafunwa vya jioni, vijitabu vya kuandikia na kalamu.

Ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii, unapaswa kulipa ada yako kabla ya tarehe 31/10/2018, ambayo ndiyo tarehe ya mwisho ya kulipia ada.

Pia nafasi za kushiriki semina hii ni 100 pekee, na zilizobaki ni chache sana. hivyo kama hutaki kukosa nafasi hii, lipa ada yako mapema ili tuweze kuwa pamoja kwenye semina hii.

Nakusubiri kwa hamu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, kwa sababu yapo mengi mazuri nimekuandalia kwa mafanikio yako kwa mwaka 2018/2019.

Namba za kufanya malipo ili kushiriki semina hii ni MPESA- 0755 953 887 au TIGO PESA/AIRTEL MONEY – 0717 396 253. Majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA. Ukituma fedha tuma na ujumbe wa kueleza umefanya malipo ya semina, ukiambatana na jina lako na namba yako ya simu kwa ajili ya kupewa taarifa zaidi za semina.

Ni mimi rafiki na kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha