Rafiki yangu mpendwa,

Kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN BABYLON (kitabu ambacho nimekuwa nashauri kila mtu akisome, na sasa kuna tafsiri yake ya kiswahili, hivyo hakikisha umekisoma), ipo hadithi moja yenye funzo kubwa sana kuhusu fedha na utajiri.

Hadithi inakwenda kwamba Arkard, aliyekuwa mtu tajiri kuliko wote Babeli alikuwa na kijana aliyeitwa Nomasir. Kwa utamaduni wa Babeli, vijana wa kiume walirithi mali za wazazi wao. Lakini Arkard hakupendezwa na hilo, hivyo kijana wake alipofikia umri wa kuanza maisha ya kujitegemea, alimwita na kumwambia kwa kuwa sasa umekua, nataka unidhibitishie kwamba unaweza kuzitunza vizuri mali zangu. Hivyo nitakupa vitu viwili ambavyo mimi mwenyewe sikupewa wakati naanza maisha kwenye umasikini.

Vitu viwili alivyompa mtoto wake ilikuwa mfuko wenye dhahabu, na vibao vyenye sheria tano za dhahabu. Alimwambia kama atazielewa sheria hizo tano, na kutumia dhahabu alizompa, ataweza kufanikiwa sana. baada ya kumkabidhi vitu hivyo alimwambia aondoke na kwenda kuyaanza maisha yake, na miaka kumi baadaye arejee kuja kueleza nini ameweza kufanya kwenye maisha yake.

KWA NINI SIYO TAJIRI

Baada tu ya kuondokwa kwa baba yake, Nomasir alisahau kabisa vile vibao vya kanuni za dhahabu, kilichotokea alitumia vibaya zile fedha, akatapeliwa na mwishowe akapoteza kila kitu. Alijikuta hana tena dhahabu yoyote na hapo ndipo alipokumbuka kwamba baba yake pia alimpa vibao vyenye kanuni za dhahabu. Na hapo ndipo aliposoma kanuni zile, akaanza kuzifanyia kazi na hatimaye akaweza kurejesha fedha alizopoteza na kupata nyingine mara kumi ya alizopewa na baba yake.

Hadithi hii fupi inatufundisha kuhusu kosa moja ambalo watu wengi wamekuwa wanalifanya kwenye kutafuta fedha na utajiri.

Watu wengi wamekuwa wanakazana kupata fedha na siyo kujifunza kwanza misingi ya fedha. Kinachotokea, fedha wanazipata, lakini hazikai, zinapotea zote na hivyo kila wakati ni kama wanaanza upya na wanaanzia chini.

Kama mtu angezijua kanuni za fedha, na akaziishi kwenye maisha yake, hata kama ana kipato kidogo kiasi gani, ataweza kujitengenezea utajiri mkubwa kwenye maisha yake.

Hivyo tunaweza kusema kinachowatofautisha wale wanaopata utajiri na wanaokuwa masikini siyo kipato wanachoanza nacho, bali kanuni na tabia walizonazo kuhusu fedha.

Hii ina maana kwamba hata kama unataka fedha kiasi gani, kama huna kanuni na tabia sahihi, ukipata fedha hizo zinaishia kuwa tatizo kwako kuliko kuwa msaada kwako.

Ndiyo maana hatua ya kwanza na ya muhimu kabisa kwako kuchukua ili kufikia uhuru wa kifedha na utajiri ni kujijengea msingi imara wa kifedha, kujijengea tabia ambazo zinavutia fedha na utajiri na siyo zinazopoteza fedha na utajiri.

Na mimi rafiki yako, kwa kujua jinsi swala hili lilivyo muhimu kwako, nimekuandalia semina muhimu sana.

Semina hiyo inaitwa TABIA ZA KITAJIRI, hii ni semina ambayo utajifunza tabia kumi za kuishi kwenye kila siku ya maisha yako, tabia ambazo zitakuwezesha kutengeneza utajiri mkubwa kwenye maisha yako.

Tabia hizi kumi hazijali una elimu kiasi gani, wala hazijali kipato ulichonacho sasa ni kiasi gani, hazijali umri ulionao wala haziangalii kama umeajiriwa au umejiajiri. Kwa kuzijua na kuziishi tabia hizi, utaanza kuona mabadiliko makubwa kwa upende wa kifedha.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki ukiwa popote duniani.

Ili uweze kushiriki semina hii, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, na kama hujawa mwanachama na huwezi kujiunga sasa, basi ipo nafasi ya wewe kushiriki kwa kulipa ada ya tsh elfu 20 pekee.

Kwa ada ya tsh 20,000/= utapata nafasi ya kujifunza tabia hizo kumi za kitajiri na kuzifanya kuwa sehemu ya maisha yako.

Semina itaanza tarehe 03/01/2019 mpaka tarehe 13/01/2019 na mwisho wa kulipia ili upate nafasi ya kushiriki semina hii ni tarehe 02/01/2019.

Namba za kufanya malipo ni 0755 953 887 au 0717 396 253 majina ya namba hizi ni AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma malipo ya kushiriki semina, tuma ujumbe kwa wasap namba 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia semina ya TABIA ZA KITAJIRI.

Kama una watu wa karibu kwako, labda ndugu zako, watoto wako, wafanyakazi wako na wengine wowote unaohusiana nao, ambao ungetamani waache kuwa tegemeo kwako, basi ipo nafasi ya wewe kuwasaidia. Huwa wanasema ukimpa mtu samaki ataendelea kukutegemea kila siku. Lakini ukimfundisha kuvua, basi hatakutegemea kila siku.

Mlipie mtu wako wa karibu ashiriki semina hii na atatoka akiwa na msingi wa kuweza kujitengenezea kipato na hata utajiri. Kwa uwekezaji mdogo wa tsh elfu 20, utaweza kumsaidia mtu kwa maisha yake yote, na pia ukajipunguzia mzigo wa maisha yako.

Mlipie mtu wako wa karibu leo na tuma majina yake na namba zake na atapata nafasi ya kushiriki semina hii ya TABIA ZA KITAJIRI ambayo itayabadili kabisa maisha yake.

Lipo kundi maalumu la semina ambalo nimeandaa kwa wale ambao watashiriki lakini siyo wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga na kundi la semina hii tumia kiungo hiki; https://chat.whatsapp.com/JvJBnoKixGrJZpZdw3shRv  (kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA usijiunge na kundi hili).

Karibu sana tupate maarifa sahihi ya kutujenge tabia zitakazotufikisha kwenye utajiri mkubwa. Fanya vyovyote vile uwezavyo ili uweze kushiriki semina hii, kwa sababu ukiikosa utakuwa umeamua wewe mwenyewe kufa masikini.

Kwenye dunia ambayo wapo watu waliofanikiwa na kufikia utajiri mkubwa, kila mtu ana nafasi kama hiyo, kama atajua njia sahihi za kufuata. Semina ya TABIA ZA KITAJIRI imekuja kwako kukufundisha njia hizo sahihi kwako kufuata ili kufikia utajiri mkubwa.

Rafiki, fanya malipo yako leo ili uweze kujihakikishia nafasi ya kujifunza tabia hizi kumi zitakazobadili kabisa maisha yako kwa upande mzuri.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge