Mpendwa rafiki yangu,

Hakuna sehemu ambayo ni salama kwa kila kitu. Kila mmoja wetu kuna changamoto fulani anayopitia kwenye maisha yake. Unapojikuta uko katika hali fulani ya changamoto ndiyo sehemu ya maisha hivyo unatakiwa tu kujifunza namna ya kuikabili hiyo hali.

Unajua vitu vyote vitapita na kuisha lakini changamoto hazitokuja kuisha ila vitaisha kwako tu pale tu utakapokufa lakini kama uko hai, maisha ni changamoto na pambana ili uishi vile unavyotaka wewe.

Huwa kuna watu wanatabia ya kuchukua mambo ya kazini na kuyaleta nyumbani, na wengine na kuchukua ya nyumbani na kuyapelekea kazini. Vitu kama hivi vinakuwa vinaathiri utendaji wa kazi wa sehemu zote mbili kwa kiasi kikubwa sana.

Acha kila sehemu ijitegemee yenyewe, kama ni mambo ya nyumbani yaache yaende nyumbani na kama ni ya kazini yaachie huko kazini. Kumbuka mafahari wawili hawakai zizi moja kama wasemavyo waswahili.

vitabu softcopy

Tunapochukua matatizo ya kazini na kuyaleta nyumbani tunakuwa tunaharibu mahusiano yetu ya kifamilia na hata ndoa zetu zinakuwa hazina afya. Nyumbani ni sehemu ambayo kila mtu huwa anaamini ni salama hivyo tunaweza kupumzika na kupata kile tunachotaka ndiyo maana hata unapokuwa eneo lako la kazi unafanya haraka umalize ili tu uwahi nyumbani kila mtu akifika nyumbani basi anajisikia furaha kama siyo raha.

Siku moja mtu mmoja alikuwa anamwambia mwenzake, ‘’ mimi huwa sipeleki matatizo ya kazini nyumbani… mwenzake akamuuliza kwanini? Akamjibu mimi huwa matatizo ya nyumbani huwa na yakuta huko huko na ya huku na yaacha huku huku kazini.

SOMA; Njia Bora Ya Kukuwezesha Kutumia Nguvu Zako Kwenye Mambo Yenye Manufaa Kwako Badala Ya Kuzipoteza Kama Unavyofanya Sasa.

Ni kweli, ukienda nyumbani utayakuta ya nyumbani yanakusubiri huko huko na ukienda kazi utayakuta yakazini huko huko.

Jaribu kutumia muda wako vizuri kama ni kazi za nyumani ziache nyumbani na kama ni kazi za ofisini zifanyie ofisini na usizipeleke nyumbani kwani nyumbani siyo sehemu ya kufanyia kazi.

Muda wa nyumbani ni muda unatakiwa kushughulika na mambo ya nyumbani. Muda wa familia na kujenga mahusiano yako na familia yako na hata mwenza wako. Unapoleta kazi zako nyumbani maana yake unaiba muda wa familia na hivyo huwezi kubaki salama.

Hatua ya kuchukua leo; kazi za ofisini ziache ofisini na zifanyie ofisini na siyo nyumbani. Na matatizo ya ofisini usiyapeleke nyumbani kwani ukienda nyumbani, matatizo ya nyumbani utayakuta huko huko nyumani.

Kwahiyo, jifunze kutumia muda vizuri, heshimu muda wa kazini na wa nyumbani. Acha kila sehemu ijitegemee kwani ni taasisi mbili tofauti. Kila binadamu anahitaji amani na utulivu ili aweze kufanya yale muhimu hivyo tumia kila kitu sehemu sahihi ili upate utulivu na amani.

Makala hii imeandikwa na

Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa www.mtaalamu.net/kessydeo, vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI.  Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net

Asante sana