Habari za leo rafiki yangu mpendwa?

Nianze kwa kukushukuru sana kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja kupitia kazi hii ya uandishi na ukocha ninayofanya. Hiki ninachofanya ndiyo kusudi kuu la maisha yangu, na bila ya uwepo wako wewe rafiki yangu, kusudi hili haliwezi kukamilika.

Hivyo najivunia kusema ninapenda na kufurahia sana hiki ninachofanya, kwa sababu upo wewe rafiki yangu, ambaye unafuatilia kwa umakini mkubwa, unajifunza na kufanyia kazi haya unayojifunza na maisha yako yanakuwa bora zaidi. Na ndiyo maana mpaka sasa uko pamoja na mimi.

Leo ninayo furaha kubwa sana kukufahamisha kwamba vitabu viwili muhimu sana, ambavyo vina maarifa mazuri kwako kuweza kupiga hatua vimetoka. Vitabu hivi vimetoka kwa mfumo wa nakala ngumu (hardcopy) yaani vimechapwa na hivyo unaweza kupata nakala yako, ukatembea nayo popote unapokwenda na kuweza kujisomea kwa muda wowote unaoupata.

Ninayo furaha kubwa kwa sababu najua maarifa yaliyopo kwenye vitabu hivi yana nguvu kubwa sana ya kuyabadili na kuyaboresha maisha yako kama utayasoma na kuchukua hatua.

Kwenye makala hii nakwenda kukueleza kwa kifupi kuhusu vitabu hivi, jinsi ya kuvipata, ofa ya kipekee ninayokupa kwenye kujipatia vitabu hivi pamoja na tarehe ya uzinduzi wa vitabu hivi.

KITABU; ELIMU YA MSINGI YA FEDHA

KITABU; ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

Rafiki yangu mpendwa, kila mtu amewahi kukutana na matatizo mbalimbali ya kifedha. Iwe ni kipato kutokutosheleza, kuwa kwenye madeni, au kupata fedha nyingi kwa wakati mmoja lakini ukapoteza zote. Hakuna ambaye amewahi kutoka salama inapokuja upande wa fedha.

Matatizo haya tunayoingia kwenye upande wa fedha yanatokana na kukosekana kwa ELIMU YA MSINGI YA FEDHA. Majumbani, mashuleni, vyuoni, makazini na hata kwenye jamii hakuna mahali tumewahi kupewa elimu ya msingi ya fedha. Hivyo chochote tunachojua kuhusu fedha, tumeiga tu kutoka kwa wengine. Sasa hebu niambie unaiga kitu gani pale ambapo watu wote wanaokuzunguka wana matatizo ya kifedha? Ni matatizo.

Hivyo kupitia kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, nimekupatia maarifa yote sahihi unayopaswa kuyajua kuhusu fedha. Nimeanza na msingi mkuu wa fedha, msingi ambao ukiujua hutapata tena shida ya fedha kwenye maisha yako. Kisha nikakueleza kwa kina kuhusu kipato chako na matumizi yake. Hapa ndipo wengi wanapokwama na kujikuta wakiwa kwenye matatizo kila wakati.

Nimekupa pia maarifa sahihi kuhusu kujilipa wewe mwenyewe kwanza na sheria kuu tano za fedha ambazo kila mtu anapaswa kuzijua na kuziishi. Kitabu pia kimeeleza kuhusu uwekezaji wa fedha zako, na kwa mifano tumejadili njia mbalimbali za kuiwekeza fedha yako ili iweze kukuzalishia wewe zaidi.

Kitabu hakijaishia hapo, bali kina maarifa kuhusu kuwa na vyanzo vingi vya kipato na kuhusu biashara kama moja ya vyanzo vyako vya kipato. Utajifunza pia kuhusu kodi mbalimbali unazopaswa kulipa kwenye kipato chako na jinsi ya kupunguza kodi hizo.

Kwenye kitabu pia utajifunza jinsi ya kurithisha elimu hii ya msingi ya fedha kwa watoto wako. Wazazi wengi wamekuwa wanakazana kuwaandalia watoto mali, lakini wanapofariki watoto wanapoteza mali hizo. Sasa wewe utawapa elimu ya msingi ya fedha, ambayo itawawezesha kutumia vizuri mali utakazowaachia au wanazotafuta wenyewe.

Mwisho utajifunza kuhusu utoaji kama sehemu muhimu ya kujiimarisha kifedha. Na utamalizia kwa kujifunza mambo muhimu ya kuzingatia kwenye fedha na utajiri. Kwa sababu kama hujajua, basi jua leo, kadiri kipato chako kinavyoongezeka, ndivyo watu watakuchukia bila sababu yoyote ya msingi, ni asili ya binadamu, hivyo unapaswa kuelewa na kujiandaa kupokea hilo.

ELIMU YA MSINGI YA FEDHA ni kitabu ambacho kila mtu aliye makini na maisha yake anapaswa kukisoma, na siyo mara moja, bali akisome mara nyingi, kwa kifupi kila unapokuwa unapaswa kuwa na kitabu hiki.

Kitabu hiki cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA kinapatikana kwa uwekezaji wa tsh elfu 20 (20,000/=). Nasema uwekezaji kwa sababu kwa kutumia fedha hiyo kununua kitabu hiki, utaweza kupata mara 10, 100 na hata zaidi ya kiasi hicho cha fedha.

Kama upo Dar es salaam utaletewa kitabu ulipo, na kama upo mkoani basi utatumiwa kitabu kwa njia ya basi (utachangia nauli ya kutuma).

Karibu sana ujipatie kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, upate maarifa sahihi ya kifedha yatakayokutoa pale ulipokwama sasa.

KITABU; TANO ZA MAJUMA YA MWAKA

KITABU; TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA.

Rafiki yangu mpendwa, vipo vipimo vingi sana vya muda. Kwa kuanzia chini kabisa tuna sekunde, ambazo zikiwa 60 tunapata dakika, dakika 60 zinatupa saa, masaa 24 yanatupa siku, siku 7 zinatupa juma na majuma 52 yanatupa mwaka. Miaka kumi inaleta muongo, miongo kumi inaleta karne na karne 10 zinaleta milenia.

Katika vipimo hivyo vingi vya muda, kuna kipimo kimoja sahihi sana kwako kukitumia na kukiishi kila siku kama unataka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Kipimo hicho cha muda kinakuwezesha kupangilia mambo yako vizuri na kuweka sawa vipaumbele vyako.

Kipimo sahihi cha muda kwako ni juma moja, yaani siku 7 au masaa 168. Hiki ni kipimo ambacho ukiweza kukitumia vizuri, basi utaweza kufanya chochote unachotaka kufanya kwenye maisha yako, na kufanikiwa sana.

Kwenye kitabu cha TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA, nimeugawa mwaka mzima kwenye majuma 50 ya kufanya kazi na majuma mawili ya kupumzika. Katika majuma hayo 50 ya kazi, nimekupa vitu vya kukusaidia katika kupiga hatua zaidi.

Kwa kila juma la mwaka, nimekupa vitu vitano vya kufanyia kazi;

Moja ni siri muhimu ya mafanikio, ambayo inakufunulia yale usiyojua kuhusu mafanikio na hatua za kuchukua.

Mbili ni uchambuzi wa kitabu cha mafanikio, hapa unapata uchambuzi wa kina wa kitabu kinachohusu mafanikio.

Tatu ni makala ya juma, hapa unapata makala nzuri inayohusu mafanikio kwenye maeneo mbalimbali ya maisha.

Nne ni #TUONGEE PESA, hapa unayapata maarifa sahihi ya kifedha, ambayo yanakuondoa kwenye changamoto mbalimbali za kifedha.

Tano ni #TAFAKARI YA KUFIKIRISHA, hapa unapata tafakari kutoka kwa watu mbalimbali, tafakari ambazo zinatufanya tufikiri upya mazoea yetu na kuchagua kufanya kwa njia tofauti.

Hivyo kwa kitabu kizima, utajifunza siri 50 za mafanikio, utapata uchambuzi wa vitabu 50 vya mafanikio, utapata makala bora 50 za mafanikio, maarifa ya kifedha 50 na tafakari za kufikirisha 50.

Rafiki, kitabu hiki kimeshiba kweli kweli, ni kitabu chenye kurasa 500, ambazo zimejaa dhahabu hasa inapokuja kwenye maarifa.

Hiki ni kitabu ambacho utapaswa kukisoma kwa mwaka mzima, kila juma kusoma sura moja, kuitafakari na kuiweka kwenye matendo. Siyo kitabu cha kusoma mara moja, umalize na kuendelea na mambo mengine. Kitabu hiki unapaswa kukiweka pembeni ya kitanda chako au mezani kwako ili kila siku upate nafasi ya kukipitia unapoamka, kabla hujaanza kazi, kabla hujafunga kazi na kabla hujalala.

Kitabu hiki kinapatikana kwa uwekezaji wa shilingi elfu 50 (50,000/=) ni uwekezaji ambao utakulipa mara dufu, kwa sababu maisha yako yatakuwa bora sana kupitia usomaji wa kitabu hiki, na siyo kwa eneo moja tu, bali kila eneo la maisha yako.

Kama upo Dar es salaam utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa kwa njia ya basi hivyo utachangia nauli ya kutuma kitabu hicho kuja kule ulipo.

Rafiki, kitabu cha TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA ni kitabu ambacho unapaswa kuwa nacho na kukisoma kila siku, sijui nisisitize vipi, ni muhimu sana uwe na kitabu hiki.

MUHIMU; Utakaponunua kitabu hiki cha TANO ZA JUMA, utapata bure nakala tete (softcopy) ya vitabu vyote 50 vilivyochambuliwa kwenye kitabu hiki, kupitia mtandao wa telegram.

UZINDUZI WA VITABU HIVI VIWILI.

Rafiki yangu mpendwa, nitafanya uzinduzi wa vitabu hivi viwili kwa kuwa na mkutano mfupi ambao utafanyika kwa kukutana ana kwa ana Dar es salaam.

Uzinduzi utafanyika siku ya jumamosi tarehe 03/08/2019 kwenye ukumbi wa Golden Park Hotel iliyopo Sinza jijini Dar es salaam.

Kwenye uzinduzi huu nitapata muda wa kugusia kwa kina baadhi ya mambo muhimu kutoka kwenye vitabu hivi viwili, na pia nitaweka sahihi kwenye vitabu ambavyo utanunua na hata kupata picha ya pamoja na kila anayenunua kitabu.

Ili kushiriki uzinduzi huu wa vitabu, utachangia tsh elfu 10 (10,000/=). Nafasi za kushiriki uzinduzi huu ni chache, hivyo kama unapanga kushiriki, tuma ujumbe wa kawaida wa simu, wenye majina yako kamili na namba ya simu ukisema NITASHIRIKI UZINDUZI WA VITABU kwenda namba zifuatazo; 0717 396 253 na hapo utajihakikishia nafasi ya kushiriki uzinduzi huu.

ZAWADI MAALUMU KWAKO YA KUPATA VITABU HIVI VIWILI.

Kwa sababu nakupenda na kukujali sana wewe rafiki yangu, nimechagua kukupa zawadi ya vitabu hivi viwili kwa kukupa ofa ambayo itakuwezesha kupata vitabu hivi viwili kwa urahisi zaidi.

Kuanzia leo tarehe 15/07/2019 mpaka tarehe 31/08/2019 utaweza kupata kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA kwa uwekezaji wa tsh 15,000/= badala ya tsh 20,000/=.

Pia utaweza kupata kitabu cha TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA kwa uwekezaji wa tsh 40,000/= badala ya tsh 50,000/=.

Na zawadi nzuri zaidi ni kwamba, ukijipatia vitabu vyote viwili, badala ya kuwekeza tsh 70,000/= kwa bei ya kawaida au 55,000 kwa bei ya ofa, unawekeza tsh 50,000/= yaani elfu 50 pekee kwa vitabu vyote viwili.

Hii ni zawadi ya kipekee sana kwako rafiki yangu, ambayo itakupa uhakika wa kujifunza kwa mwaka mzima hata kama hutanunua au kusoma vitabu vingine.

Ofa hii ni kuanzia leo tarehe 15/072019 mpaka tarehe 31/07/2019, hivyo chukua hatua mapema ili usikose zawadi hii ya kipekee sana kwako.

JINSI YA KUFANYA MALIPO.

Ili kupata vitabu, ofa na hata nafasi ya kushiriki uzinduzi wa vitabu hivi, unapaswa kufanya malipo yako mapema.

Malipo ya vitabu unaweza kutuma kwa namba 0717 396 253 au 0755 953 887 na kisha kutuma ujumbe kwenye moja ya namba hizo kwamba umelipia kitabu na utapatiwa kitabu chako. Lakini pia unaweza kuagiza kitabu na ukaletewa, ukishakabidhiwa ndiyo unakilipia. Agiza kitabu kwa namba hizo hapo juu na utaletewa ulipo.

Malipo ya kupata ofa ya vitabu unayafanya moja kwa moja kwa namba 0717 396 253 au namba 0755 953 887 au kuagiza na kuletewa vitabu kisha ukalipia.

Malipo ya kushiriki semina ya uzinduzi wa vitabu unafanya kwa namba 0717396253 au 0755953887 kisha unatuma majina yako kamili na namba za simu na maelezo kwamba umelipia kushiriki uzinduzi wa vitabu.

Karibuni sana marafiki zangu wote mjipatie vitabu hivi ambavyo vinakwenda kubadili kabisa maisha yetu. Chukua hatua leo hii ili usikose zawadi au kukosa nafasi ya kushiriki semina ya uzinduzi.

Kumbuka, ofa ya kupata vitabu hivi inaisha tarehe 31/07/2019 hivyo chukua hatua sasa.

Muhimu zaidi, kama utashiriki semina ya uzinduzi wa vitabu hivi (kitu ambacho hupaswi kukosa), tuma majina yako na namba za simu kwenye namba 0717 396 253 na ujumbe kwamba utashiriki uzinduzi na utatunza nafasi yako. Kama utapenda kuja na mtu wako wa karibu ili naye apate mafunzo haya, yatakayomsaidia sana, pia mwekee nafasi yake.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge