Rafiki yangu mpendwa,

Moja ya elimu muhimu sana ambazo kila mmoja wetu anapaswa kuipata ni ELIMU YA MSINGI YA FEDHA. Hii ni elimu ambayo ina manufaa sana kwa kila mtu, lakini imekuwa haifundishwi popote.

Na kama kila mmoja wetu anavyojua, fedha ndiyo kitu pekee ambacho kila mtu anakitafuta na kukipigania. Kwa sababu bila ya fedha, maisha hayawezi kwenda. Kila kitu kwenye maisha kinahitaji fedha.

Kwa kujua umuhimu huu wa elimu ya fedha, na kwa kuona namna wengi tunavyoteseka inapokuja swala la fedha, nimetafiti na kuandika kitabu kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA FEDHA (BASIC FINANCIAL EDUCATION).

elimu fedha 2

Kitabu hiki kinakupa maarifa yote muhimu unayopaswa kuwa nayo kuhusu fedha na hatua za kuchukua ili uweze kutoka kwenye umasikini na kwenda kwenye utajiri na uhuru wa kifedha.

Moja ya vitu ambavyo utajifunza kwa kina kutoka kwenye kitabu hiki ni SHERIA TANO ZA FEDHA, ambazo ukizijua na kuzifanyia kazi, hakuna namna utashindwa kutoka kwenye umasikini na matatizo ya kifedha.

Moja ya vitabu nilivyowahi kusoma kuhusu fedha na nikavielewa na hata kujenga msingi wangu wa kifedha ni kitabu THE RICHEST MAN IN BABYLON. Kitabu hiki kimetoa elimu muhimu sana kuhusu fedha kwa kutumia hadithi ya enzi za utawala wa Babeli. Kitabu kimeeleza kwa kina kuanzia kuongeza kipato, kuweka akiba, kuwekeza, kuondoka kwenye madeni, kulinda utajiri na mengine muhimu.

Kwenye kitabu hiki, ipo hadithi ya mtu mmoja tajiri, ambaye baada ya kijana wake kufikia umri wa kuweza kujitegemea, alimwita na kumwambia anataka ampime na kuona kama anaweza kurithi mali zake. Na alimpa mfuko wa fedha, pamoja na kitabu cha sheria za fedha, na kumwambia miaka kumi ijayo, arudi kwake na kumwambia amefanya nini na fedha zile.

Kama ilivyo kwa wengi wanaopata fedha nyingi kwa wakati mmoja, hakuhangaika na zile sheria za fedha, badala yake alianza kutumia fedha zile. Alishauriwa kujihusisha na biashara asizozielewa, mojawapo ikiwa ni kamari na kupoteza fedha zote. Baada ya kubaki hana kitu, ndiyo alikumbuka baba yake alimpa sheria za fedha, akazitafuta na kuanza kuzisoma na kuzifanyia kazi. Miaka kumi baadaye alirudi kwa baba yake akiwa na fedha mara tatu ya alizoepwa, na kumshukuru baba yake kwa sheria zile.

Sura hii inaanza na maelezo kwamba, mpe mtu achague kati ya fedha au hekima ya fedha, wengi watakimbilia fedha. Kinachotokea, wanapuuza hekima ya fedha, na kupoteza fedha wanazokuwa wamekimbilia.

Hivyo kabla ya kutaka kuongeza kipato na hata kufikia utajiri, ni vyema tukajifunza sheria hizi tano muhimu za fedha. Sheria hizi ni za vizazi na vizazi, hazipitwi na wakati. Sheria hizi nimezitoa kwenye kitabu cha THE RICHEST MAN IN BABYLON. Tuzisome na kuziishi maisha yetu yote, tutajenga msingi imara kifedha.

SHERIA YA KWANZA YA FEDHA; KUJILIPA MWENYEWE.

Fedha huenda kwa mtu ambaye anatenga siyo chini ya sehemu ya kumi ya kipato chake kwa ajili ya maisha ya badaye kwake na kwa familia yake.

Hapa ndipo ilipo dhana ya kujilipa wewe mwenyewe kwanza. Kwamba kipato chochote kinachopita kwenye mikono yako, hata kiwe kidogo kiasi gani, hakikisha sehemu ya kumi ya kipato hicho huitumii kwa matumizi ya aina yoyote ile. Hii ni kwa ajili ya maisha ya baadaye, kwako wewe na vizazi vyako.

Kama unatumia kipato chako chote unachoingiza, huwezi kutengeneza utajiri na uhuru wa kifedha, hata iweje. Tenga sehemu ya kumi na iweke pembeni. Unaitumia kufanya nini hiyo? Angalia sheria zinazofuata.

SHERIA YA PILI YA FEDHA; FEDHA KUKUFANYIA KAZI.

Fedha hufanya kazi kwa juhudi kwa yule mtu ambaye anaweza kuiwekeza kwenye eneo ambalo linazalisha. Kwa kifupi, fedha ni mfanyakazi mzuri, kama ukiweza kuiweka mahali pazuri na kuisimamia vizuri.

Kile ambacho unajilipa wewe mwenyewe kwanza, siyo kwa ajili ya matumizi ya baadaye, badala yake ni kwa ajili ya kujizalishia zaidi baadaye. Ila hapa sasa fedha inakuwa inafanya kazi zaidi ya unavyofanya wewe. Hivyo unaweza kuweka fedha hiyo kwenye biashara au hata uwekezaji, kiasi kwamba itakuzalishia faida zaidi.

SHERIA YA TATU YA FEDHA; UWEKEZAJI MAKINI.

Fedha hung’ang’ana kwa yule ambaye anaiwekeza kwa ushauri wa watu wenye hekima. Ni muhimu uwekeze fedha yako kwa ushauri wa wale ambao wanajua kuhusiana na uwekezaji ambao unaufanya. Au uchukue muda kujifunza ili uwe na uhakika wa usalama wa fedha yako.

Fedha inapowekezwa kwa umakini na ushauri wa watu wenye hekima, huzaliana zaidi na zaidi na hapo ndipo utajiri na uhuru wa kifedha unapotengenezwa.

SHERIA YA NNE YA FEDHA; HASARA KWENYE UWEKEZAJI.

Fedha huwakimbia wale ambao wanafanya uwekezaji wasioujua au hawapati ushauri wa watu wanaojua uwekezaji huo. Watu wengi wanaoshika fedha nyingi na kukosa elimu sahihi ya kifedha, hufanya uwekezaji ambao siyo makini, hilo hupelekea wao kupoteza fedha walizowekeza. Wanawekeza kwenye mambo ambayo hawayajui na hawaombi ushauri kwa wanaojua.

Fedha isipowekezwa kwa umakini na ujuzi, matokeo yake ni hasara kwa mwenye fedha.

SHERIA YA TANO YA FEDHA; UTAJIRI WA HARAKA.

Fedha hupotea haraka kwa watu ambao wanataka kutumia fedha kidogo kupata utajiri mkubwa na wa haraka. Watu wanaposhika fedha kiasi au nyingi kwa mara ya kwanza, huwa wanashawishiwa sana kujiingiza kwenye biashara ambazo zinaleta faida kubwa sana kwa muda mfupi na bila ya wao kufanya chochote. Hii ni hali ambayo imewaletea watu wengi sana hasara.

Unapokuwa na fedha, waogope sana watu wanaokushawishi kuziwekeza au kujihusisha na biashara ambayo inaonekana faida yake ni kubwa kuliko kawaida, ya haraka na wewe hupaswi kufanya chochote. Watu wa aina hiyo huwa ni matapeli au wananufaika zaidi kwa kile utakachofanya na fedha zako hizo.

Ukiziangalia sheria hizi tano za fedha, utaona mambo makuu yanayosisitizwa ni haya;

  • Jiwekee akiba kutoka kwenye kila kipato chako.
  • Itumie akiba hiyo kukuzalishia zaidi, hapo unahitaji kuwa na biashara au uwekezaji unaozalisha.
  • Wekeza kwa umakini, kwenye maeneo unayoyajua au umeshauriwa na watu wenye hekima. Usijiamulie mwenyewe na wala usikimbilie kupata faida kubwa na ya haraka.

Tunapaswa kuziishi sheria hizi kila siku, na hizi ndiyo zitatuwezesha kujijengea uhuru wa kifedha kwenye maisha yetu.

PATA KITABU CHA ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

Rafiki, ili kujifunza zaidi kuhusu fedha na kuweza kupata mikakati ya kuondoka kwenye umasikini na kwenda kwenye utajiri pata na usome kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

Kitabu hiki kimechapwa na kinatumwa popote ulipo Tanzania.

Kitabu hiki kinapatikana kwa uwekezaji wa tsh elfu 20, (20,000/=) lakini kama utakinunua kabla ya tarehe 01/08/2019 basi utakipata kwa bei ya punguzo ambayo ni tsh elfu 15 (15,000/=).

Kama unahitaji kitabu na upo dar, tuwasiliane kwa namba 0717396253 au 0755953887 kisha utaletewa kitabu ulipo. Kama upo mkoani tuma elfu 15 ya kitabu pamoja na elfu 5 ya nauli kwenye namba hizo hapo juu, kisha tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na mahali ambapo kitabu kinatumwa.

Rafiki, usikose kabisa kitabu hicho, uwekezaji utakaofanya kwa kujipatia kitabu hicho, utakulipa sana sana sana.

KARIBU KWENYE UZINDUZI WA VITABU.

Rafiki, tutafanya uzinduzi wa kitabu hiki cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, pamoja na kitabu kingine kinachoitwa TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA siku ya jumamosi ya tarehe 03/08/2019.

Kwenye uzinduzi huu tutajifunza mambo muhimu kuhusu usomaji wa vitabu, jinsi ya kunufaika na usomaji wa vitabu, jinsi ya kupata muda wa kusoma vitabu na pia tutajifunza yale muhimu kuhusu vitabu hivyo viwili.

Kupata nafasi ya kushiriki uzinduzi huu unapaswa kutoa taarifa kupitia namba 0717396253 au 0755953887. Tuma ujumbe wenye majina yako kamili na maelezo kwamba utashiriki uzinduzi na hapo utawekewa nafasi yako.

Ada ya kushiriki uzinduzi huu ni shilingi elfu 10 (10,000/=) na unapaswa kuilipa kabla ya tarehe 01/08/2019.

Usomaji wa vitabu ni moja ya uwekezaji ambao ukiufanya utakulipa maisha yako yote. Jipatie sasa kitabu chako cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na pia karibu kwenye uzinduzi tujifunze mengi zaidi kuhusu vitabu.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge