Rafiki yangu mpendwa,

Kabla ya kuweka mafunzo ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA kwenye kitabu ambacho kinapatikana sasa, mafunzo haya yaliendeshwa kama semina mwaka 2017.

Yalikuwa mafunzo bora sana ambayo kila aliyeshiriki aliweza kutoa ushuhuda wake ni kwa namba gani mafunzo hayo yamemfungua na kumpa hatua sahihi za kuchukua.

Ni kutokana na maoni na shuhuda hizi za wengi nikapata msukumo wa kuyaweka mafunzo haya kwenye kitabu, ili yaweze kuwafikia wengi zaidi lakini pia yawe kumbukumbu nzuri kwa wale ambao waliyapata ili waweze kuwashirikisha watu wa karibu pia.

elimu fedha 2

Hapa nimekushirikisha shuhuda tano tu kati ya shuhuda nyingi za wale walioshiriki mafunzo haya.

Soma shuhuda hizi na utaona ni kwa jinsi gani mafunzo hayo yanaweza kukusaidia na wewe pia.

Habari za Coach. Binafsi nimejifunza mengi sana kwenye semina hii kubwa kuliko yote ambalo Kwangu lilikuwa geni kabisa ni juu ya kutenga mafungu ya kipato na pia suala la kubana matumizi hizo mbili ni elimu mpya kabisa nilikuwa naishi tu kama ng’ombe bila kuwa na utaratibu. Jambo lingine ambalo nimefaidika sana ni kuandika matumizi yoyote ya hela ninayofanya na pia kuwa na kijitabu cha kumbukumbu ya jambo lolote ninalopanga kufanya au ninalosikia lenye manufaa

Barikiwa sana. – Elisha Mwambapa

Ahsante sana kocha kwa semina hii nzuri sana nimejifunza mengi baadhi nimechukua hatua tayari kwa wiki hii moja nimeona matokeo makubwa sana ambayo haikuwa rahisi kuyaona kama naweza kutengeneza biashara kubwa sana.

Changamoto niliyokua nayo ni hii Kila nikipata hela nalipa deni sijali kula kuvaa kuweka akiba na Kila kitu lengo kulipa madeni tu nikawa najikuta vitu vingine haviendi sawa inabidi nikope tena ili kubalance hali halisi.

Kwa kweli nikawa naona biashara haikui hata Hamu ya kujifunza zaidi ilikua inanitoka nilitaka nilipe madeni kwanza. Lakini nilipojifunza tu kuongeza thamani kwenye biashara nimeona matokeo yake.

Mashineni nilikua sina mahindi hivyo nikataka nikope benki ili nikanunue mahindi ili niweze kuyauza pindi yatakapoadimika. Wakati wa semina nikakipata kitu kuongeza thamani hivyo nikajiambia lazima niongeze thamani ya mahindi wiki hiyo. Nikaanza kusema na kutenda kua sasa sitatoa hata shilingi mashineni mpaka nifikishe gunia kumi kwa kuanza, mpaka Leo Nina gunia NNE.

Na ningelianza hili mapema ningekua nimeshatoka kwenye madeni muda mrefu. Hali ile ilinifanya nisiwe na hela hata ya kulipia ada ya Kisima cha Maarifa kwa sababu nakua sina hela yoyote ya dharura yaani ikipatikana 10000 nalipa MTU ambaye atazidi kunidai najipa mwezi mmoja tu ntakuwa nimepiga hatua kubwa sana ahsante sana kocha. – Emanuel Salum

Asante sana kocha kwa semina hii nzuri sana. Pamoja na kuwa na umri mkubwa, elimu nzuri na kubahatika kuhudhuria semina nyingi, kwa kweli hii ni ya kipekee kabisa. Maandalizi bora kabisa, na mada safi. Kuhusu bajeti kwa mfano, nilikuwa najidanganya kuwa iko kichwani. Baada ya kugawa kipato na kuandika matumizi yote nimejishangaa nilivyojidanganya na kupata hasara kubwa. Nimenufaika na kutotembea na pesa nyingi mfukoni.  Kumbe nilikuwa natumia hela ovyo sana. Kuhusu masharti ya kubaki kisimani… hapo ndipo penyewe… itabidi kwa namna yeyote nibaki maana bila hii chemchem mimea yangu yote niliyopanda itanyauka. – Mary Materu

Katika masomo niliyowahi kusoma , hii semina ya Elimu ya msingi ya Fedha ipo kiwango cha juu. Mimi binafsi nimefika sana na familia yangu, nimeanza kuwafundisha watoto wangu elimu hii, na muda si mrefu nitaanza kuwawekea compound interest na 72 rule .Pia ninakushukuru Coach tangu 2౦14 nilipoanza kusoma Amka Mtanzania na kisha Kisima cha Maarifa nimefika mengi Sana ikiwa kuwa na vyanzo vya kipato zaidi ya kimoja japo sasa kazi imeisha Nina akiba ya dharura kwa mwaka mzima. Na pia Kuhusu nidhamu yako ya utendaji​ kazi imenibariki na nimeanza kuifanyia kazi. Mungu akubariki sana. – Cuthbert Mtweve.

Asante sana kwa maarifa ambayo nimeyapata kutoka kwenye semina, ilikuwa mara ya kwanza maishani kuona mtu anasema wazi wazi siri za mafanikio ya kifedha. Umejitoa sana maana tulicholipa hakilingani tulichopokea. Mungu akubariki zaidi. Nimejifunza mengi sana, jinsi nilikuwa natumia pesa ovyo, nanunua vitu hata ambavyo situmii, sizingatii muda hivyo natumia usafiri wa boda boda ili kuwahi, nakopa hela kununua vitu ambavyo siyo muhimu. Pia nimeona gharama kubwa ya matibabu ambayo nalipa kwa kuogopa bima ya afya. Kwenye makosa yote nilikuwa nafanya hamna mtu wa kumlaumu , ni Mimi mwenyewe hata kushindwa ni mimi nitaamua. Nilifungua account na utt kwenye umoja account lakini badaye nikaacha kuwekeza. Sina ujanja lazima niwe karibu na watu wenye kiu ya mafanikio, Mafanikio ni kuchukua hatua, mwaka umeisha hakuna nilichokifanya cha maana. Mtu hawezi kubadilika Kama hajachoka , mimi nimechoshwa na madeni mpaka Kuna siku nililia sana na kuwaza hela zinaenda wapi ikiwa nina madeni hivi!? Mshahara unaisha kabla sijaupata. Haya yote nimejifunza wapi nilipokuwa nakosea.

Nimeamua kubadilika pia nitajiunga kisima cha maarifa, ada siyo kubwa kabisa kwani huwa naweza kuchangia kwenye harusi zaidi ya hiyo. Mungu akubariki Sana kwa maarifa haya ya Kiungu. – Nyomokonyo Ginoga

Rafiki, hizo ni shuhuda chache sana kati ya nyingi ambazo watu wametoa baada ya kupata mafunzo ya ELIMU YA MSINGO YA FEDHA.

Ninachotaka kukuambia wewe rafiki yangu ni kwamba, haya pia yanaweza kutokea kwako, na sasa nimerahisisha sana, kwani unaweza kupata kitabu chenye mafunzo yote ya msingi kuhusu fedha, kajifunza na kuchukua hatua na hilo litayafanya maisha yako kuwa bora zaidi.

Kitabu kinapatikana kwa gharama ya tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sasa kuna ofa kama utakipata mapema kabla ya tarehe -1/08/2019 ambapo utakipata kwa tsh elfu 15 (15,000/=).

Kama upo jijini Dar Es salaam utaletewa kitabu ulipo na kama upo mkoani basi utatumiwa kwa njia ya basi.

Kupata kitabu tuma fedha kwenda namba 0717396253 au 0755953887 kisha tuma ujumbe wenye majina yako kamili, namba ya simu na mahali kitabu kinatumwa na utatumiwa au kuletewa. Kama upo mkoani utaongeza gharama za nauli ya kusafirisha.

Karibu sana ujipatie kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, kitakuondoa hapo ulipokwama sana na kukuwezesha kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Pia kuna kitabu kingine kimetoka pamoja na hiki, ambacho kinaitwa TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA, kwa jina jingine tunaweza kuita kitabu hiki MWONGOZO KAMILI WA MAFANIKIO. Ni kitabu kikubwa chenye uchambuzi wa vitabu 50, siri 50 za mafanikio, makala bora za mafanikio, maarifa ya kifedha na tafakari za kubadili fikra zako. Kupata kitabu hiki piga simu au tuma ujumbe kwenye namba 0717396253.

Mwisho kabisa, kutakuwa na mkutano wa kukutana moja kwa moja wa uzinduzi wa vitabu hivi viwili; ELIMU YA MSINGI YA FEDHA na TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA. Uzinduzi huu utafanyika jumamosi ya tarehe 03/08/2019 Golden Park Hotel Sinza, Dar Es Salaam. Kushiriki unalipa ada ya tsh elfu kumi. Kupata nafasi ya kushiriki uzinduzi huu, tuma ujumbe wenye majina yako kamili na namba ya simu na maelezo kwamba utashiriki uzinduzi kwenda namba 0717396253. Karibu sana uwahi kwa sababu nafasi za kushiriki ni chache, tuma ujumbe sasa kama unapanga kushiriki.

Nikutakie kila la kheri, pata vitabu hivi na uvisome na maisha yako hayatabaki hapo yalipo sasa.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge