Mwaka 1884, Leo Tolstoy, aliyekuwa mwandishi mashuhuri kutokea nchini Usrusi alipata wazo; “vipi kama kukiwa na kitabu ambacho kinakusanya mawazo ya hekima kutoka kwa watu wenye hekima sana ambao wamewahi kupita hapa duniani?”

Tarehe 15 mwezi Machi mwaka 1884 Tolstoy aliandika kwenye kijitabu chake; “nahitaji kuandaa mwongozo wa kusoma kwa ajili yangu, ambao utatoka kwa watu wenye hekima kama Epictetus, Marcus Aurelius, Lao-Tzu, Budha, Yesu na wengineo”

Basi alifanyia kazi wazo hili kwa miaka 15, akisoma vitabu na waandishi bora na kukusanya mawazo yenye hekima kutoka kwa waandishi na vitabu hivyo. Na mwaka 1902 alianza kuandika kitabu kujumuisha mawazo hayo ambacho kilitoka mwaka 1904. Kitabu hicho kilikuwa na mawazo ya hekima ya kila siku kwa siku za mwaka na kimekuwa kinaitwa majina mengi kwa matoleo mbalimbali, lakini jina kuu la kitabu hicho ni KALENDA YA HEKIMA.

Rafiki yangu mpendwa, ninayo furaha kukujulisha ya kwamba mwaka 2020 tunakwenda kupata hekima kila siku kutoka kwenye kitabu hiki cha Leo Tolstoy kinachoitwa A Calendar of Wisdom.

a-calendar-of-wisdom.jpg

Tutakwenda kupata hekima hizi, pamoja na maelezo ya nyongeza kutoka kwangu kupitia TAFAKARI za kila siku ambazo zinapatikana kwenye KISIMA CHA MAARIFA pekee.

Mwaka 2019 tulikwenda na kitabu cha hekima za ustoa kila siku kwa mwaka mzima ambazo zilitoka kwenye kitabu cha Ryan Holiday kinachoitwa THE DAILY STOIC.

Mwaka huu 2020 tunakwenda kupata hekima kutoka kwa watu wenye hekima sana ambao wamewahi kupita hapa duniani kupitia TAFAKARI hizo za kila siku.

Habari njema zaidi kwako rafiki yangu ni hii, kwa mwaka 2020 TAFAKARI za siku zitakuwa mbili badala ya moja kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma. Kutakuwa na tafakari ya kuianza siku ambayo unaipata asubuhi na mapema, yaani unapoamka unakutana na tafakari. Na pia kutakuwa na tafakari ya kuimaliza siku ambayo inawekwa usiku, hivyo kabla hujalala unakuwa na kitu cha kutafakari.

Kwa tutakwenda pamoja kwa tafakari hizi za 2020 na kuzifanyia kazi basi maisha yetu lazima yatakuwa bora sana, kwa sababu hekima haijawahi kumwangusha yeyote.

Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, chukua hatua sasa ili usikose mambo haya mazuri ya mwaka mzima. Maana nikikuahidi kitu, nakifanya kweli, ije mvua lije jua. Niliahidi kuandika kurasa za mafanikio kila siku kuanzia tarehe 01.01.2015 na kwa miaka mitano sasa nimekuwa naandika kila siku, bila ya kuacha hata siku moja. Mwaka 2019 tumejifunza tafakari za kitabu cha Daily Stoic kila siku ya mwaka, bila ya kuacha hata siku moja.

Na sasa una nafasi ya kupata hekima kila siku kwa mwaka mzima, na siyo tu hekima za kukupa wewe ufahari kwamba unajua sana, bali hekima za kuyawezesha maisha yako kuwa bora zaidi.

Kupata nafasi ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA kama wewe siyo mwanachama tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA.

Usichelewe rafiki yangu, tayari tumeshazianza hekima za 2020, mfano tafakari ya tarehe moja ni kuhusu kusoma vitabu bora, na mwaka huu 2020 tutasoma vitabu vilivyopendekezwa na watu wenye mafanikio makubwa, ambavyo vimeorodheshwa kwenye mtandao wa www.mostrecommendedbooks.com ambapo chambuzi za vitabu hivyo pamoja na vitabu vyenyewe vitapatikana kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA, fungua kiungo kujiunga; https://www.t.me/somavitabutanzania

Tafakari ya tarehe 02 imekuwa kuhusu dini ya kweli ambayo ni upendo, upendo una nguvu kubwa mno, nguvu ya kushinda au kuvunja chochote. Hivyo mwaka huu 2020 tunakwenda kuishi kwa upendo, kuanzia kujipenda sisi wenyewe, kuwapenda wengine na kupenda chochote tunachofanya.

Unayakosaje mambo haya mazuri ambayo tutaendelea kujifunza kwa mwaka mzima na kuyaweka kwenye matendo ili maisha yetu yaweze kuwa bora sana? Tuma sasa ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA kwenda namba 0717396253, ujumbe utume kwa wasap pekee.

Nikutakie kila la kheri rafiki yangu, ukawe na mwaka bora sana 2020, uwe mwaka wa wewe kuwa na hekima na kuweza kufanya maamuzi ya busara yatakayopelekea kuwa na maisha bora.

Nakupenda sana, ndiyo maana natumia kila fursa kukushirikisha maarifa yaliyo bora kabisa.

Kuna makala nzuri na za bure kila siku kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA (www.amkamtanzania.com) pamoja na mfumo wetu wa email ambapo kila siku unapokea email za mafunzo bure kabisa. Kujiunga na mfumo huu fungua; http://eepurl.com/dDZHvL

kwa ada kidogo mno, unaweza kupata vitabu na chambuzi zake kila wiki, hivi vinapatikana kwenye channel yetu ya SOMA VITABU TANZANIA, ambapo kujiunga unafungua hapa; https://www.t.me/somavitabutanzania

Pia kuna vitabu mbalimbali ambavyo vinakupa wewe maarifa ya kukuwezesha kupiga hatua zaidi. Vitabu hivi ni kama ELIMU YA MSINGI YA FEDHA,BIASHARA NDANI YA AJIRA NA TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA. Hivi ni vitabu ambavyo nilivichapa mwaka 2019 na wengi sana wamenufaika navyo. Kama wewe bado hujavipata na kunufaika navyo, piga simu 0678 977 007 au 0752 977 170 na utapewa utaratibu wa kuvipata.

Mwisho kabisa, kwa ada ya mwaka, tunaweza kuwa karibu zaidi, tukijifunza na kushirikiana kwa njia mbalimbali kupitia KISIMA CHA MAARIFA. Kwenye KISIMA CHA MAARIFA unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap na pia kuna mtandao wenye mafunzo mbalimbali ambao ni www.kisimachamaarifa.co.tz hakuna maarifa ambayo utayakosa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Hivyo rafiki yangu mpendwa, ambaye ninakupenda kweli kutoka ndani ya moyo wangu, chagua huduma ninazotoa ambazo zitakufaa na twende pamoja. Ikiwa ni za bure, za kulipia kidogo au kulipa ada ya mwaka, mimi nitaendelea kukupenda kwa huduma yoyote utakayochagua. Kwa sababu bila ya wewe, kazi yangu mimi haina maana.

Tukawe na mwaka 2020 ambao ni bora sana, mwaka wa kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu.

Kocha na Rafiki yako mpendwa,

Dr. Makirita Amani.