Unapotaka kwenda kununua bidhaa fulani au kitu chochote kile ni lazima kwamba ujue sifa ya kile kitu au ubora wa kile kitu ili ufanye maamuzi ya kununua. Hakuna mtu  makini anayekwenda kununua bidhaa ambayo haina sifa nzuri.

Kumbe basi, sifa ndiyo kiashiria cha uhai wa kitu fulani, hata katika uongozi, kuna sifa zake na leo hii tunakwenda kujifunza sifa mbili za kiongozi ambazo unapaswa kuzijua.

Sifa ya kwanza, ni kiongozi kuwahi eneo la kazi. Kama wewe ni kiongozi unatakiwa uwe mfano bora, kuwa wa kwanza katika eneo la kazi inakusaidia kujijengea heshima au nidhamu ya uongozi. Unaweza kutumia muda huo kupangilia ratiba zako, kufanya kitu cha ziada kabla ya muda wa kazi au hata kupitia yale mambo muhimu na kufanya majukumu mapema kabla yaw engine.

Uongozi ni kama biashara tu, unatakiwa kuwa wa kwanza kufungua biashara yako na ukiwa wa kwanza kufungua biashara yako hutoweza kuwa sawa na watu wengine katika upande wa mauzo. Lakini kama wewe ni kiongozi unakuwa wa mwisho kufika hiyo siyo sifa nzuri.

Sifa ya pili, kiongozi kuwa wa mwisho kutoka eneo la kazi. Mchezo ni ule ule unakuwa wa kwanza kufika na kuwa wa mwisho kutoka kama ilivyo katika biashara. Unakuwa wa kwanza kufungua na wa mwisho kufunga kwa namna hii utajijengea sifa nzuri ya uongozi.

Kuwa wa mwisho kutoka ofisini itakusaidia kujua vizuri tathimini ya siku katika kazi imekwendaje, hakuna mtu atakaye kudanganya kwa taarifa za uongo kwani wewe mwenye utakua unashuhudia.

SOMA; Je Unafundishika? Tabia Tano Za Watu Wanaofundishika Na Wenye Nafasi Ya Kupata Mafanikio Makubwa.

Ukishakuwa na hizo sifa, hata wale unaowaongoza pia watajitahidi kuwahi kazini lakini kama wewe ni mchelewaji halafu unataka watu wengine wawe wanawahi utashindwa. Watu wanapenda kutena kwa mfano, wakiona kiongozi wao anawahi nao watajiambia kama mkuu wao wa kazi anawahi mimi nichelewe ni nani?

Hatua ya kuchukua leo; Jijengee sifa bora ya kiongozi kwa kuwa wa kwanza kufika na wa mwisho kuondoka.

Kwahiyo, hata kama wewe siyo kiongozi, kwa kutumia mbinu hizi mbili za kuwa wa kwanza kuwahi na wa mwisho kutoka itakusaidia kuongeza thamani katika eneo lako la kazi.

Makala hii imeandikwa na

Mwl. Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa  http://kessydeo.home.blog vitabu na kwenye klabu yake ya MIMI NI MSHINDI.  Karibu sana.

Ukawe na siku bora sana rafiki.

Rafiki na mwalimu wako,

Mwl, Deogratius kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com //kessydeoblog@gmail.com

Asante sana