Rafiki yangu mpendwa,

Hatua ya kwanza kwako kuchukua kama unataka kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako, ni kuacha kujidanganya.

Lakini hicho ni kitu kigumu sana kufanya, kwa sababu ukweli huwa unaumiza, na kitu ambacho tupo tayari kutumia nguvu nyingi kukizuia ni maumivu.

Hivyo katika kuepuka maumivu, tumekuwa tunajidanganya, na kupitia kujidanganya huko, tumekuwa tunajizuia kufikia mafanikio makubwa.

Muulize mfanyakazi yeyote ambaye amekaa kwenye ajira kwa miaka mingi, huku akiwa hajapiga hatua yoyote, kwa nini hafanikiwi na atakuwa na majibu mengi sana. Atakuambia amekuwa analipwa kidogo, mwajiri wake hajali, maisha magumu, wategemezi wengi na mengine. Lakini hatakuambia ukweli halisi wa maisha yake, kwamba amekuwa akifanya kazi zake kwa mazoea miaka yote, hajawahi kuweka akiba yoyote kwa miaka yote ya kazi na licha ya kuwa na muda, hajawahi kufanya kitu cha pembeni kumuingizia kipato.

Muulize mfanyabiashara yeyote ambaye yuko kwenye biashara miaka mingi na hafanikiwi au biashara yake imekufa, taka kujua kwa nini hafanikiwi na utapata majibu ambayo yatakufanya umuonee huruma. Kwamba ushindani umekuwa mkali, mazingira magumu, mtaji ni tatizo na chuma ulete wamekuwa wanachukua fedha zake. Lakini hatakueleza kwamba alianza biashara kwa kuiga wengine, amekuwa anaifanya kwa mazoea, hana kinachomtofautisha na wengine na hajawahi kutenganisha matumizi ya fedha za biashara na maisha binafsi.

Muulize yeyote aliye kwenye umasikini licha ya kuwa na viungo vyote na afya kamili ya akili na mwili kwa nini yupo kwenye umasikini. Hapo utapewa sababu na orodha ya wote waliomsababisha mtu kuwa kwenye hali hiyo, kuanzia wazazi waliomzaa, serikali iliyopo madarakani, wategemezi na mengine mengi. Lakini taka kujua jinsi gani mtu huyo amekuwa anatumia kipato anachopata, utaona wazi kwamba amekuwa anatumia kipato chote, na hata kikiisha hatulii, anaenda kukopa, hivyo anatumia hata fedha ambayo bado hajaipokea.

Hii ni mifano michache, lakini kwa kila hali, mambo ndiyo yako hivyo. Tumekuwa tunatafuta sababu nzuri za kutuliwaza, na kutufanya tuone tatizo siyo sisi, na hapo ndipo tunapojizuia kufanikiwa.

Rafiki, kama kweli unataka kufanikiwa, jiangalie pale ulipo sasa, kisha nenda mbele ya kioo na yule unayemwona mnyooshee kidole, mwambie wewe ndiye umekuwa adui yangu kwa miaka yote, lakini sasa sikubali uendelee kuwa adui tena.

Ninachokuambia ni kwamba, popote ulipokwama, chochote ulichoshindwa, jipe sababu uwezavyo, lakini tatizo kuu ni mtu mmoja, ambaye ni wewe mwenyewe. Utakapojua na kukubali hili mapema, litakusaidia sana kuchukua hatua sahihi ili uweze kufanikiwa.

Karibu upate nafasi ya kuukabili ukweli wako.

Rafiki, pamoja na kuona umuhimu wa kuukabili ukweli ili uweze kufanikiwa, ni vigumu sana kufanya hivyo peke yako.

Hii ni kwa sababu jamii inayokuzunguka, iko tayari kukufichia udhaifu wako ili usiumie. Jamii hiyo imekuandalia watu na hali ambazo unaweza kuzilalamikia kwa chochote kinachotokea kwenye maisha yako.

Hata kama umejitoa kiasi gani, jamii ina nguvu kubwa ya kukuonesha kwamba tatizo siyo lako, bali tatizo ni la mfumo, tatizo ni la hali ya uchumi, mazingira na mengine mengi.

Hivyo kama unataka kukabili ukweli na uweze kufanikiwa, unahitaji kuwa kwenye mazingira tofauti, mazingira ambayo hayataki kukubembeleza kwa kukudanganya, bali kukuambia ukweli na kama utakuumiza basi ndiyo vizuri, ili uweze kubadilika.

Mazingira hayo yanapatikana kwenye jamii ya tofauti kabisa ambayo tunaijenga, jamii ya watu wenye kiu ya mafanikio makubwa na ambayo tayari wanajitoa sana kupiga hatua. Jamii hii ni KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA kila mwezi unapata nafasi ya kujitathmini kwa kila unachofanya kwenye maisha yako, na kisha Kocha anapata nafasi ya kupitia tathmini zako na kukuonesha wapi unafanya vizuri na wapi umekuwa unajizuia kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA unajifunza na kuishi maisha ambayo ni mwiko kulalamika au kulaumu yeyote, maisha yako unayafanya kuwa jukumu lako na chochote ambacho hukipendi au kukubaliana nacho unakibadili, na kama huwezi kukibadili basi unaachana nacho.

KISIMA CHA MAARIFA ni sehemu sahihi kwako, kama unataka mafanikio makubwa, bila ya kujali uko wapi na unafanya nini. Kila mtu anaweza kupiga hatua kubwa, lakini kwanza lazima aache kujidanganya yeye mwenyewe.

Rafiki, jua kabisa kwamba safari ya mafanikio siyo rahisi, na peke yako utakutana na vikwazo vingi. Unahitaji kuwa eneo ambalo litakupa nguvu ya kupambana na vikwazo hivyo. Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa maelezo yanayopatikana hapo chini, yasome mpaka mwisho.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania