Rafiki yangu mpendwa,

Kama umewahi kufika mahali na kukata tamaa na maisha, huku ukiona maisha yako hayana maana, tatizo siyo maisha, bali tatizo ni wewe binafsi.

Na tatizo lako linatokana na mambo mawili makubwa.

Jambo la kwanza ni hupambani na  changamoto za kutosha kwenye maisha.

Hapa unaweza kushangaa na kuona siyo kweli, kwa sababu kila siku umekuwa unakutana na changamoto mbalimbali kwenye maisha yako.

Hilo ni kweli kabisa, lakini je umekuwa unapambanaje na changamoto hizo? Umekuwa unazikabili na kuzitatua au umekuwa unazikimbia?

Kwa walio wengi, tabia imekuwa ni kuzikimbia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo.

Wapo wanaozikimbia kwa kuzikataa na kuona changamoto hizo siyo zao, hivyo kutafuta watu wengine wa kuwatupia lawama za changamoto hizo.

Wengine wanazikimbia changamoto kwa kutafuta kitu cha kuwasumbua ili tu wasifikirie changamoto hizo. Hapa ndipo vilevi, matumizi ya mitandao ya kijamii na kufuatilia maisha ya wengine vinapotumika sana, mtu anakuwa hajui vitu hivyo vinampa nafasi ya kutoroka changamoto zake.

Sasa changamoto mbalimbali zinazokukabili kwenye maisha huwa haziondoki zenyewe, badala yake huwa zinaendelea kukua kadiri zinavyoachwa.

Kwa kutokukabiliana na changamoto zako, unazipa nafasi ya kukua na kuendelea kuwa imara, huku wewe ukiwa dhaifu kwa sababu huna unachofanya ili kuzikabili changamoto hizo.

Inafika mahali ambapo changamoto ni kubwa na imara sana huku wewe ukiwa dhaifu, ukiziangalia changamoto katika ngazi hiyo, unaishia kukata tamaa na kujiona huwezi tena kukabiliana na changamoto na maisha yako yanakosa maana.

Jambo la pili ni kutokujifanyia tathmini.

Tatizo la pili linalopelekea wewe kuona maisha yako hayana maana ni kutokuyafanyia maisha yako tathmini mara kwa mara.

Njia pekee ya kujua kama unapiga hatua kwenye maisha yako ni kujifanyia tathmini na kujipima mara kwa mara.

Kutenga muda ambao utakuwa unajiangalia ulikotoka, ulipo na unapokwenda.

Kuangalia malengo uliyojiwekea, hatua ulizochukua na matokeo uliyopata.

Ni tathmini za aina hii ndiyo zinazokuonesha wapi uko imara, wapi una mapungufu na hatua zipi za kuchukua ili uweze kupata matokeo bora zaidi.

Bila ya kufanya tathmini ya aina hii mara kwa mara unakuwa gizani, hujui nini kinaendelea kwenye maisha yako, hujui kama unapiga hatua kwenda mbele au unarudi nyuma.

Hali hiyo inapelekea iwe rahisi kwako kukata tamaa na kuona maisha yako hayana thamani.

Ili maisha yako yawe na maana na uendelee kuwa na matumaini makubwa kwenye maisha yako, hakikisha unafanyia kazi vitu hivyo viwili, kukabiliana na changamoto unazokutana nazo kwenye maisha na kujifanyia tathmini mara kwa mara na kuchukua hatua kuwa bora zaidi.

Karibu Upate Msukumo Wa Kukabiliana Na Changamoto Na Kujifanyia Tathmini Mwenyewe.

Rafiki yangu mpendwa, jamii yetu ina kila njia ya kutusaidia kuyatoroka maisha yetu, ina kila sababu tunazoweza kutumia pale ambapo mambo hayaendi kama tunavyotaka.

Sehemu ya kwanza ni kwenye lawama, kila mtu ana orodha ya watu anaoweza kuwalaumu kwa chochote kinachotokea kwenye maisha yake.

Utashangaa mtu mwenye umri wa miaka zaidi ya 20 akilaumu kwamba maisha yake ni magumu kwa sababu ya mambo ambayo wazazi au walezi wake walifanya au hawakufanya.

Utapigwa na butwaa pale mtu aliyefanya kazi kwa zaidi ya miaka kumi lakini hakuna kikubwa alichofanya na sababu ni mwajiri wake kutokumjali au kumlipa vizuri.

Utashangaa zaidi pale kila tatizo ambalo mtu analo basi linatokana na serikali.

Sababu zote hizi ni nzuri na zinaliwaza, lakini zinakuzuia usiuone ukweli.

Njia nyingine ambayo jamii imetufundisha kutumia kutoroka maisha yetu ni kwenye usumbufu.

Jamii inakuuliza je una changamoto? Usihofu, kunywa bia baridi au vuta sigara fulani na changamoto zako hazitakusumbua tena.

Jamii inakuambia kama hujisikii vizuri, tafuta picha yako nzuri, weka mitandaoni na baada ya muda mfupi utaanza kupokea mafuriko ya likes na maoni kwamba umependeza, uko vizuri na hapo utajisikia vizuri.

Rafiki, njia hizo za mkato zimekuwa hazifanyi kazi na ndiyo maana watu huishia kukata tamaa na kuona maisha hayana thamani.

Ipo sehemu moja sahihi kwako kupata msukumo wa kukabiliana na changamoto unazokutana nazo kwenye maisha yako ya kila siku na pia kujifanyia tathmini ya mara kwa mara.

Sehemu hiyo ni kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unabadili kabisa mtazamo wako kuhusu changamoto unazokutana nazo kwenye maisha.

Unaacha kuziona changamoto kama ni kitu kibaya cha kukwepa na unaziona kama ni kitu kizuri cha kukaribisha, kwani changamoto hizo ndiyo zinakufanya ukue zaidi.

Lakini pia kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA, kila mwezi unajifanyia tathmini ya kina kwenye maisha yako kwa kila ulichofanya na kisha kumtumia kocha. Kitendo tu cha kufanya tathmini hiyo ya mwezi, kinakufanya uyaone maisha yako kwa uhalisia na siyo kwa kujidanganya.

Karibu sana ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo, ili unufaike kuwa kwenye jamii ya kipekee kabisa, jamii ambayo inakaribisha changamoto na kuzitatua ili kuwa bora zaidi na ambayo kila mwezi unapata nafasi ya kujifanyia tathmini ya kina kwenye maisha yako na kuona kila kitu bila ya kujidanganya.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania