Rafiki yangu mpendwa,

Kwa kipindi cha miaka saba ambacho nimekuwa kwenye huduma hii ya kutoa mafunzo ya mafanikio, nimepata bahati ya kukutana na watu mbalimbali.

Kupitia watu hao nimejifunza mambo mengi sana, na kila siku bado naendelea kujifunza mambo mengi kupitia wale ninaokutana nao kupitia huduma hii.

Katika mengi ambayo nimejifunza katika miaka hiyo michache, kuna moja ambalo nimekuwa naona linajirudia mara kwa mara na linanistua sana.

 

kusukuma jiwe.
Mafanikio ni kama kusukuma jiwe kwenye mlima, ukiacha kusukuma unaanguka.

Mambo huwa yanaenda hivi;

Mtu anakutana na mafunzo yangu, labda alikuwa anatafuta kitu mtandaoni kisha akakutana na makala, au ameambiwa na mtu mwingine afuatilie mafunzo ninayotoa.

Anayafuatilia na anaona yanamfaa, anajifunza kweli kweli, anajiunga na huduma nyingine mbalimbali ninazotoa.

Anaweka juhudi kubwa na anaanza kuyaona mafanikio makubwa, tofauti na alivyokuwa anafanya miaka ya nyuma. Anakiri wazi kwamba kama angejua mambo hayo mapema, basi angekuwa mbali sana.

Anaendelea kujifunza kwa juhudi kubwa, huku akiendelea kuweka juhudi kubwa kwenye kile anachofanya na matokeo anayopata yanakuwa makubwa.

Baada ya muda wa kukua kimafanikio, anafikia hatua ambayo anaridhika, anaona ameshafika kiwango cha juu na kuamini kwamba tayari anajua kila kitu, hana tena kitu kipya cha kujifunza.

Na hapo ndipo anguko la wengi huanzia, pale anapofikiri ameshajua kila kitu na hana kipya cha kujifunza, anaacha kujifunza, anaacha kuweka juhudi kubwa alizoweka akafika hapo, na hilo linakaribisha anguko lake.

Hiki ni kitu ambacho nimekuwa nakiona kinajirudia kwa wengi, na nimejifunza kiasi kwamba naweza kujua mapema nani ataweza kudumu na mafanikio anayoyapata na nani mafanikio yake yatakuwa ya muda tu.

Utajua hujui.

Mwanafalsafa Socrates, ambaye ndiye baba wa falsafa zote aliwahi kuuliwa kwa nini yeye ni mtu mwenye hekima kuliko watu wote, kwa nini anajua sana. Jibu lake lilikuwa hili; kitu pekee ninachojua ni kwamba kuna vitu vingi sana sivijui, hivyo kila wakati najifunza.

Rafiki, pale unapofikiri umeshajua kila kitu, ndiyo utajua kwamba hujui, ndipo utakapoacha kujifunza na kuanza kufanya makosa ambayo yatakugharimu sana.

Utaanza kuona kila kitu kinakwenda hovyo na utadhani labda ni kisirani au watu wanakuhujumu, lakini ukweli ni kwamba umeuacha msingi sahihi na kile ulichojenga lazima kianguke.

Safari ya mafanikio haina kuhitimu.

Aliyekuwa mhamasishaji maarufu Zig Zigler aliwahi kuulizwa swali kwamba  wale anaowapa hamasa, itadumu nao kwa muda gani? Zigler akajibu hamasa inayotolewa mara moja huwa haidumu.

Kama ambavyo mtu hali mara moja au kuoga mara moja maisha yake, ndivyo ilivyo pia kwamba hamasa ya mara moja haina manufaa. Mtu anakula kila siku na kuoga kila siku, anahitaji pia kupata hamasa kila siku.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye kujifunza, kama unavyolisha mwili wako kila siku, ndivyo unavyopaswa kulisha akili yako na roho yako. Lakini cha kushangaza, watu wana afya nzuri ya mwili, ila akili zina utapiamlo.

Kama unavyosafisha mwili wako na kuupendezesha kila siku, ndivyo unavyopaswa kuisafisha na kuipendezesha akili yako. Utashangaa kuona wengi ni wasafi na wanapendeza kwenye mwili, ila akili zao zimebeba takataka ya kila aina.

Unapoingia kwenye safari ya mafanikio makubwa, unapoamua kwamba unataka kuwa na maisha ya tofauti, basi umejiandikisha kufanya vitu hivi viwili mpaka siku unakufa; kujifunza na kujaribu mambo mapya.

Siku utakayoacha kufanya vitu hivyo, ndiyo siku ambavyo utaanza kuanguka.

Ni kawaida kwa wale ambao hawajafanikiwa, kuwaona waliofanikiwa wakiendelea kuhangaika na kusema ningekuwa na mafanikio kama yake nisingejisumbua.

Aliyefanikiwa lakini anaendelea kujisumbua ni kwa sababu anajua bila kujisumbua mafanikio hayo hayatadumu. Asiyefanikiwa lakini anajiambia akifanikiwa hatajisumbua, hawezi kufanikiwa.

Karibu kwenye mazingira yatakayokusukuma kujifunza na kujaribu vitu vipya bila kuacha.

Unahitaji mazingira ambayo yatakusukuma kujifunza vitu vipya kila siku na kujaribu mambo mapya ili uweze kufanikiwa na hata kudumu kwenye mafanikio.

Mazingira ambayo yatakufanya uone bado kuna vitu vingi huvijui, lakini pia yanayokusukuma kuweka malengo makubwa sana, ambayo yatakusukuma kuyafanyia kazi kila siku.

Unahitaji mazingira ambayo kadiri unavyofanikiwa, ndivyo unavyokua na kiu ya kufanikiwa zaidi, hivyo kuendelea kujifunza zaidi na kuendelea kujaribu mambo mapya.

Mazingira hayo ni KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa kwenye KISIMA, unapaswa kujiwekea lengo kubwa sana ambalo unalifanyia kazi kwenye maisha yako. Na hata ukifikia lengo hilo, unaweka jingine kubwa, ambalo ni mara kumi (10X) ya lengo ulilofikia mwanzo, hivyo huwezi kuridhika na kujiona umeshapata kila kitu.

Pia kwenye KISIMA CHA MAARIFA unalazimika kujifunza vitu vipya kila wakati, kila mwezi unapaswa kusoma angalau kitabu kimoja. Kuna mafunzo ya semina mbalimbali za mtandaoni na za ana kwa ana yanayokuwezesha kujifunza na kuwa bora zaidi kwenye kile unachofanya.

Kwenye KISIMA kuna utaratibu wa kujifanyia tathmini kila mwezi, ukifanyia kazi kipengele hiki kila mwezi, wewe mwenyewe utajionea uko wapi ukilinganisha na kule unakokwenda. Wengi wanaoamini wameshafika kilele cha mafanikio au wameshajua kila kitu, ni kwa sababu hawajifanyii tathmini ya mara kwa mara.

Ukichagua kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, na kuhakikisha unaendelea kuwa mwanachama huku ukijifunza na kuchukua hatua, utajijengea mafanikio ambayo hayawezi kuangushwa na chochote. Na hata ikitokea kuna namna mafanikio yako yameanguka, haitakuchukua muda utarudi kwenye mafanikio makubwa kutokana na aina ya maisha unayokuwa umechagua kuyaishi kila siku.

Rafiki yangu mpendwa, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi jua unajichelewesha sana kufikia mafanikio makubwa. Unajiweka kwenye hatari ya kupata mafanikio kidogo yakawa kikwazo kwa mafanikio yako makubwa, kwa sababu utaona umeshajua kila kitu na huna haja ya kujisumbua tena. Kwenye KISIMA kila siku ni siku ya kujifunza na kujaribu vitu vipya.

Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii, ili upate nafasi ya kupata mafunzo, mwongozo na hamasa ya mafanikio kila siku bila ya kuhitimu, huku ukijisukuma kuchukua hatua mpya kila siku bila ya kujali mafanikio gani umeshayapata.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

  1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.
  2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)
  3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
  4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.
  5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.
  6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.
  7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.
  8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.
  9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.
  10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania