Karibu kwenye uchambuzi wa kitabu kinachoitwa High Growth Handbook kilichoandikwa Elad Gil ambaye ni mzoefu kwenye kampuni za teknolojia zinazokua kwa kasi. Kwenye kitabu hiki Elad anatushirikisha uzoefu wake kwenye hatua ya ukuaji wa kasi wa biashara ambapo wengi hupotea. Kitabu hiki kimesheheni mengi kuanzia kuajiri, masoko, fedha na hata kufukuza wafanyakazi wasio sahihi.

Ujumbe Kutoka Kwa Mwandishi.

Karibu kwenye kitabu hiki kitakachokupa maarifa ya kuiwezesha kuikuza biashara yako kutoka watu 10 mpaka watu 10,000.

Mengi yameandikwa kuhusu hatua za awali za kuanzisha na kukuza biashara, hasa za kiteknolojia. Mambo kama kupata mtaji kutoka kwa wawekezaji, kulijua soko, kuajiri watu sahihi na kukuza biashara kufikia wafanyakazi 10. Lakini zaidi ya hapo, hakuna mengi yameandikwa.

Kipindi cha ukuaji wa kasi wa biashara, baada ya kuwa imepata mtaji, imekamata soko na inaajiri kwa kasi, kutoka wafanyakazi 10 mpaka kufika maelfu ya wafanyakazi ndiyo kipindi chenye changamoto kubwa. Kwa kuwa ni kampuni chache kati ya zinazoanzishwa ndiyo zinafikia hatua ya ukuaji wa kasi, maarifa kwenye eneo hilo hayapo.

Kitabu hiki kinaenda kuwa jawabu la changamoto mbalimbali ambazo biashara huwa zinakabiliana nazo katika kipindi cha ukuaji wa kasi. Kuna changamoto kubwa katika kipindi hicho kama kuongeza zaidi mtaji, kuajiri watu sahihi, hasa viongozi, kutengeneza utamaduni mzuri wa eneo la kazi na hata kununua kampuni nyingine.

Kutokuwa na maarifa na uzoefu kunafanya biashara nyingi kuanguka zikiwa zimefika kwenye kipindi hicho cha ukuaji wa kasi. Hivyo Elad kwa uzoefu alioupata kwenye makampuni mengi ya teknolojia aliyofanya kazi, ana maarifa sahihi ya kuwasaidia wale wanaopitia ukuaji huo wa kasi.

Safari hii siyo rahisi, lakini kwa kuwa na maarifa sahihi kutoka kwenye uzoefu wa wengine, inakupa moyo na kukupa nguvu ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye safari hiyo.

Lakini Elad anatutahadharisha kwamba ushauri wowote unaopokea ni ushauri tu, lazima wewe unayeupokea utafakari kwa kuangalia kile unachopitia na kisha kuona hatua sahihi za kuchukua. Hivyo kitabu hiki siyo msaafu ambao unapaswa kufuatwa kama ulivyo, bali ni mwongozo wa kukusaidia kufanya maamuzi sahihi katika ukuaji wa biashara yako.

Kuhusu mwandishi.

Elad Gil ni mjasiriamali, mshauri na mwekezaji kwenye makampuni ya kiteknolojia. Amewekeza na kushauri kwenye makampuni kama Airbnb, Coinbase, Checkr, Gusto, Instacart, OpenDoor, Pinterest, Square, Stripe, Wish na mengineyo.

Ni mwanzilishi na mwenyekiti wa kampuni ya Color Genomics ambapo alikuwa CEO tangu mwaka 2013 mpaka mwaka 2016. Kabla ya hapo alikuwa mmoja wa wakurugenzi kwenye kampuni ya Twitter.

Elad pia amewahi kufanya kazi kwenye kampuni ya Google ambapo alihusika kwenye kununua baadhi ya makampuni ambayo yameiwezesha Google kukua, kama Android.

Elad ana shahada ya uzamivu (Ph.D.) kutoka chuo cha Massachusetts Institute of Technology na ana shahada ya Hisabati na Baiolojia kutoka chuo cha California, San Diego.

Kwenye makala hii nakwenda kukushirikisha kwa kifupi yale yaliyo kwenye uchambuzi kamili wa kitabu hiki. Kusoma uchambuzi kamili na kuondoka na hatua a kwenda kuchukua kwenye biashara yako, jiunge na channel ya SOMA VITABU Tanzania kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania

Jukumu La Mtendaji Mkuu (CEO)

Kwenye vitabu vingi vya biashara, majukumu ya CEO yamekuwa yanaainishwa kuwa;

1. Kuweka mwelekeo na mkakati wa kampuni na kuuwasilisha kwa wafanyakazi, wateja na wawekezaji.

2. Kuajiri, kufundisha na kutengeneza utamaduni sahihi kwenye kampuni.

3. Kukusanya mtaji na kuugawa kwa usahihi kwenye shughuli za kampuni.

4. Kuwa mwanasaikolojia mkuu wa kampuni, kwa kuwapa wengine moyo pale mambo yanapokuwa magumu.

Yote hayo ni muhimu, lakini kwenye kitabu hiki, Elad anatushirikisha majukumu makuu matatu ya CEO ambapo akiweka nguvu zake kwenye hayo, kampuni itaenda vizuri. Majukumu hayo matatu ni jinsi ya kujisimamia mwenyewe, kuwasimamia walio chini yake na kuisimamia bodi ya wakurugenzi.

Kwenye uchambuzi kamili wa kitabu hiki utajifunza hatua za kuchukua kwenye majukumu hayo matatu, ingia kwenye channel sasa ujifunze. Fungua www.t.me/somavitabutanzania

Kutafuta, Kuajiri Na Kusimamia Vipaji.

Ukuaji na mafanikio ya kampuni unategemea sana watu unaowaajiri kwenye kampuni yako. Ni muhimu uajiri watu sahihi, wenye uwezo wa kutekeleza majukumu yao na hamasa ya kufanya hivyo.

Kwenye uchambuzi kamili wa kitabu hiki utajifunza hatua za kuchukua ili uweze kupata na kuajiri watu sahihi na kukaa nao muda mrefu kwenye kampuni yako. Ingia kwenye channel sasa ujifunze. Fungua www.t.me/somavitabutanzania

Kujenga Timu Ya Watendaji.

Wakurugenzi wa vitengo mbalimbali vya biashara yako ndiyo watendaji kwenye kampuni. Hawa wanahusika kusimamia vitengo vyao ili viweze kuisaidia kampuni kufikia maono yake. Kama mkurugenzi mkuu, utaweza kukuza kampuni yako unapokuwa na timu nzuri ya watendaji.

Kujenga timu bora ya watendaji ni zoezi gumu kwa waanzilishi wachanga, kwa sababu mwanzoni walikuwa wanafanya kila kitu peke yao. Lakini sasa kampuni inakua kwa kasi, hawawezi tena kufanya hivyo. Na hapo bado wengi wanakuwa hawajawa tayari kugatua majukumu yao.

Lakini inafika hatua ambapo kama mwanzilishi huwezi tena kusimamia kila kitu peke yako, kwa sababu majukumu yanayotaka muda wako ni mengi kuliko muda ulionao. Hivyo unakuwa huna budi kujenga timu ya watendaji.

Changamoto kubwa kwenye kuajiri watendaji ni kwamba unapaswa kutafuta watu wenye uzoefu zaidi yako, kitu ambacho siyo rahisi. Lakini unapofanikiwa kuajiri mtendaji wa kwanza vizuri, wanaofuata haitakuwa changamoto kwenye kuwaajiri.

Unapokuwa na watendaji wazuri, mambo mengi kwenye kampuni yanaenda bila ya wewe mwenyewe kuhusika moja kwa moja. Unaona kama ni miujiza maana mambo yaliyokuwa yanakusumbua awali hayakusumbui tena kwa sababu wapo wanaoyafanyia kazi.

Lakini pia kuna wakati makosa yanafanyika kwenye uajiri na mtendaji anayeajiriwa anakuwa siyo sahihi. Hapo msongo unakuwa mara mbili, kwa majukumu yanayokutegemea na mtendaji asiyefaa. Mtendaji wa aina hiyo huwa chanzo cha wafanyakazi wazuri kuikimbia kampuni yako.

Kwenye uchambuzi kamili utajifunza mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kujenga timu ya watendaji.

Muundo Wa Kampuni Na Ukuaji Wa Kasi.

Muundo wa kampuni kwenye kipindi cha ukuaji wa kasi ni jambo lenye changamoto kwa waanzilishi wasio na uzoefu. Hii ni kwa sababu inakuwa vigumu kuwa na muundo mmoja, kadiri kampuni inavyokua, ndiyo mabadiliko yanayohitajika kwenye muundo.

Kwenye uchambuzi kamili utajifunza hatua sahihi za kuchukua kwenye kutengeneza muundo wa kampuni kwenye kipindi cha ukuaji wa kasi.

Masoko Na Mahusiano Ya Umma.

Masoko na mahusiano ya umma (marketing and PR) ni eneo muhimu kwenye ukuaji wa kampuni yoyote ile. Ila kwa kampuni zilizo kwenye hatua ya ukuaji wa kasi, eneo hilo ni muhimu na linapaswa kufanya kwa usahihi.

Mchango wa masoko na mahusiano ya umma ni kujenga jina la kampuni (brand), kutengeneza taswira nzuri kwa umma, kupata kutunza wateja wa kampuni.

Kwenye uchambuzi kamili utajifunza njia bora za kufanya masoko na mahusiano kwa umma ili kampuni iweze kunufaika.

Usimamizi Wa Bidhaa.

Usimamizi wa bidhaa ni eneo muhimu wakati wa ukuaji wa kasi wa kampuni. Hii ni kwa sababu uhitaji unakuwa mkubwa na hivyo kusipokuwa na usimamizi mzuri, bidhaa inaweza isiwe bora au mahitaji ya wateja yasifikiwe.

Usimamizi mzuri wa bidhaa unaiwezesha kampuni kuweka maono makubwa ya bidhaa, mipango ya kufikia maono hayo, mikakati ya kufanyia kazi na hatua za kuchukua.

Usimamizi mbaya wa bidhaa unakuwa fujo kwa kampuni nzima kwani hakuna maono, na mambo hayafanyiki kwa wakati.

Ili kuwa na usimamizi mzuri wa bidhaa, unapaswa kuwa na kitengo mahususi kwa ajili ya bidhaa, kinachosimamiwa na meneja wa bidhaa ambaye anakuwa na ujuzi wa juu kwenye bidhaa husika. Pia unapaswa kutengeneza mchakato sahihi unaofuatwa kwenye kuandaa bidhaa husika.

Fedha Na Uthaminishaji.

Fedha na uthaminishaji ni eneo muhimu kwenye ukuaji wa kasi wa kampuni. Katika kipindi cha ukuaji wa kasi, japo kampuni inaweza kuwa na wateja wengi, lakini inaweza isiwe inazalisha faida. Hivyo kama CEO utahitaji kupata fedha za kuendelea kuendesha kampuni. Huu ndiyo wakati utakaohitajika kuithaminisha kampuni na kisha kukaribisha wawekezaji kuwekeza mitaji yao. Pia unaweza kuiuza kampuni au kuipeleka kwa umma.

Kwenye uchambuzi kamili wa kitabu hiki utajifunza hatua za kuchukua ili uweze kupata mtaji zaidi wa kukuza kampuni yako. Ingia kwenye channel sasa ujifunze. Fungua www.t.me/somavitabutanzania

Kuungana Na Kununua.

Njia nyingine ya kukuza zaidi kampuni yako ni kuungana na kampuni nyingine ambayo ni kubwa zaidi au kununua kampuni ambayo ni ndogo.

Kuungana na kununua (Mergers & acquisitions) kunaiwezesha kampuni kupata bidhaa, teknolojia, timu na hata kuondoa ushindani kwenye soko.

Kwenye uchambuzi kamili tutajifunza mambo ya kuzingatia wakati wa kuungana au kununua kampuni nyingine.

Karibu upate uchambuzi kamili wa kitabu High Growth Handbook ujifunze hatua sahihi za kuchukua wakati wa ukuaji wa kasi wa kampuni yako. Karibu ujiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA, kwa kufungua www.t.me/somavitabutanzania

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.