“Tukijilinganisha na vile tunavyoweza kuwa, ni kama tupo usingizini… Tunatumia sehemu ndogo sana ya uwezo mkubwa wa kiakili na kimwili tulionao.” Aliyasema hayo mwanasaikolojia William James.

Watu wengi hawakuwa wanalielewa hilo kipindi anasema maneno hayo, kwa sababu walishaaminishwa kwamba kile ambacho mtu anafanya, ndivyo alivyopangiwa kufanya, ndiyo hatima yake.

Jamii ilikuwa imempa mtu jukumu au ukomo wa uwezo wake na watu hawakupata nafasi ya kuweza kufanya zaidi ya walivyokuwa wanategemewa kufanya na jamii hizo.

Lakini kwa bahati, kuna baadhi waliweza kufanya tofauti na zaidi, na hao wakazalisha matokeo makubwa tofauti kabisa na yaliyozoeleka na hao ndiyo waliofikia mafanikio makubwa.

Watu hao hawakujua nini kimewawezesha kufanya tofauti, walijikuta wakipata msukumo mkubwa kutoka ndani yao, labda kutokana na mazingira waliyopitia au mapenzi makubwa ambayo walikuwa nayo kwenye kile walichokuwa wanafanya.

Habari njema ni kwamba hatuhitaji tena kubahatisha ndiyo tuweze kufanya makubwa. Kwani maendeleo ya sayansi na teknolojia yameweza kutuonesha nguvu kubwa sana iliyopo kwenye mwili na akili zetu ambayo kwa sasa hatuitumii.

Ni nguvu hiyo ndiyo inawawezesha baadhi ya watu kufanya makubwa sana na kufanikiwa.

Ni nguvu hiyo ndiyo inayoleta miujiza kwenye maisha ya wengi, kwa kuwawezesha kupata matokeo ambayo hawakuwahi kudhani wangeweza kuyapata na hata wengine hawajawahi kuyapata.

Uzuri ni kwamba, nguvu hiyo ya akili na mwili tayari ipo ndani yako, lakini umekua hunufaiki nayo kwa sababu hujui kama ipo na hujui jinsi ya kuitumia.

Kwenye kitabu kipya nilichotoa, kinachoitwa UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, nimekuonesha nguvu hiyo iliyopo kwenye akili na mwili wako na jinsi ya kuifikia na kuitumia kufanya makubwa.

Kama kuna popote ulipokwama kwenye maisha yako, jibu halipo nje, bali lipo ndani yako. Ukianza na jibu hilo la ndani yako, utaweza kujikwamua na kufanya makubwa sana.

Karibu sana usome kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA ili uanze kuchukua hatua za tofauti na kupata matokeo makubwa kwenye maisha yako.

Kitabu hiki kimechapwa (hardcopy) na bei yake ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini kwa sababu nakupenda sana wewe rafiki yangu, ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 tu. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Kwa maisha yako yote, umekuwa unafichwa siri ambayo iko mbele ya macho yako, ni wakati sasa wa kufichua siri hiyo ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako na upate mafanikio makubwa.

ZAWADI NYINGINE YA KITABU.

Rafiki, kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA kimeambatana na kitabu kingine kipya nilichotoa kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Kwa hali inavyoenda, kwa ukosefu wa ajira uliopo na unaoendelea kukua, biashara ndiyo mkombozi pekee kwa kila mtu kuweza kuingiza kipato sahihi kwake.

Lakini wengi wamekuwa wanaingia kwenye biashara kwa kubahatisha, nasema hivyo kwa sababu watu hawaanzi na mawazo sahihi ya biashara, hawajui taratibu mbalimbali za kufuata na pia hawana mikakati ya kuiwezesha biashara kukua na kutokuwategemea.

Kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA kimekuja na jawabu, kinakupa yale maarifa ya msingi kabisa ambayo kila mtu aliye kwenye biashara au anayepanga kuingia basi anapaswa kuyajua na kuyafanyia kazi.

Hivyo kama tayari upo kwenye biashara au unapanga kuingia kwenye biashara, pata nakala yako leo ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA ili uweze kujenga biashara yako kwenye misingi sahihi na ufanikiwe.

Kitabu hiki kimechapwa (hardcopy) na bei yake ni tsh elfu 20 (20,000/=) lakini leo ninakupa kama zawadi kwa kulipia tsh elfu 15 pekee. Chukua hatua sasa ya kukipata kitabu hiki kwa kupiga simu au kutuma ujumbe kwenda namba 0752 977 170. Kama upo Dar utaletewa kitabu ulipo, kama upo mkoani utatumiwa.

Rafiki, changamkia sasa zawadi hizi nzuri za vitabu viwili nilivyokupa, kwani vitakusaidia sana kwenye maisha yako. Kimoja kinakufundisha jinsi ya kufanya makubwa kwa kuanzia hapo ulipo sasa na kingine kinakupa misingi ya kuanzisha na kukuza biashara. Wasiliana sasa na mtu wa mauzo kwa namba 0752 977 170 kupata zawadi hizo za vitabu.

Rafiki, karibu upate na kusoma vitabu vizuri vya maendeleo binafsi na mafanikio kwa lugha ya Kiswahili. Pakua na weka app ya SOMA VITABU na upate maarifa sahihi. Kwa maelezo zaidi fungua; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania