Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo.
Ni ile siku ambayo jana ulisema kesho nitafanya.
Kesho yenyewe ndiyo hii, hivyo basi tunza ahadi yako.

Tafadhali sana usiseme tena kesho utafanya, hakuna kesho nyingine zaidi ya leo.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.
Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu LET GO OF REACTION…
Kuna wakati mtu anaweza kufanya jambo linalokufanya uhamaki, na hivyo kutaka kumjibu haraka kwa kile alichofanya, lakini kwa kufanya hivyo hakuna chochote unachobadili. Haibadili kilichofanyika na wala humbadili aliyefanya, hivyo kwa kifupi unakuwa umepoteza muda na nguvu zako.
Kwa mfano kaka unaendesha gari na dereva mwingine ‘akakuchomekea’, yaani akakatisha mbele yako kinyume na sheria na taratibu za barabarani, jambo ambalo linaweza kuketa ajali. Unaweza kukasirika na kuanza kumnyooshea vidole na kumpa maneno makali, huku yeye aliendelea na mwendo wake wa kasi. Lakini kufanya hivyo hakumbadili dereva wala hakubadili kilichofanyika.
Hivyo badala ya kupoteza muda na nguvu kukasirika ba kupiga kelele, achilia kujibu kwako na angalia kwamba upo salama. Jua utakutana na watu wa aina hiyo wengi kwenye kila eneo la maisha yako. Na kilicho muhimu ni wewe kutoka salama.
Siyo kila kitu lazima ujibu, siyo kila mtu lazima umjibu, siyo kila anayekupinga anastahili maelezo yako.
Pima kama kujibu kwako au kutoa maelezo yako kunabadili chochote. Kama hakubadili, achilia mbali na songa mbele.
Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.