Hivi Ndivyo Elimu Ya Msingi Ya Fedha Ilivyobadili Maisha Ya Wengi, Na Inavyoweza Kubadili Maisha Yako Pia.

Rafiki yangu mpendwa, Kabla ya kuweka mafunzo ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA kwenye kitabu ambacho kinapatikana sasa, mafunzo haya yaliendeshwa kama semina mwaka 2017. Yalikuwa mafunzo bora sana ambayo kila aliyeshiriki aliweza kutoa ushuhuda wake ni kwa namba gani mafunzo hayo yamemfungua na kumpa hatua sahihi za kuchukua. Ni kutokana na maoni na shuhuda... Continue Reading →

Haya Ndiyo Mambo Matano Muhimu Ya Kujifunza Kila Juma Kwa Mwaka Mzima Ili Ufanikiwe Sana.

Rafiki yangu mpendwa, Aliyekuwa mwandishi na mhamasishaji maarufu Jim Rhon amewahi kunukuliwa akisema, mafanikio huwa yanaacha alama, kama utafanya kile ambacho waliofanikiwa wanafanya, na wewe lazima ufanikiwe. Huu ni ukweli usiopingika kwamba mafanikio huwa yanaacha alama, mafanikio siyo siri, mafanikio yapo wazi kabisa kama tutakuwa tayari kujifunza kupitia wale waliofanikiwa na kupiga hatua zaidi. Lakini... Continue Reading →

TAARIFA MUHIMU; Vitabu Vipya Viwili Vimetoka, Elimu Ya Fedha Na Tano Za Juma. Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuvipata.

Habari za leo rafiki yangu mpendwa? Nianze kwa kukushukuru sana kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja kupitia kazi hii ya uandishi na ukocha ninayofanya. Hiki ninachofanya ndiyo kusudi kuu la maisha yangu, na bila ya uwepo wako wewe rafiki yangu, kusudi hili haliwezi kukamilika. Hivyo najivunia kusema ninapenda na kufurahia sana hiki ninachofanya, kwa sababu... Continue Reading →

Hatua Tatu (03) Zitakazokutoa Kwenye Umasikini Na Utegemezi Na Kukufikisha Kwenye Utajiri Na Uhuru Wa Kifedha.

Rafiki yangu mpendwa, Kwa mujibu wa tafiti zilizofanywa na taasisi inayoitwa Social Security Administration, ya nchini Marekani, zinaonesha kwamba ukiwachukua watu 100 wanaoanza kazi au biashara na kisha kuwafuatilia kwa miaka 40 mpaka pale wanapostaafu, hiki ndiyo utakachokiona; mmoja pekee ndiyo atakuwa na utajiri mkubwa, wanne watakuwa na uhuru wa kifedha, 5 bado watakuwa wanafanya... Continue Reading →

Kauli Nane Kuhusu Fedha Za Kuziacha Mwaka 2018 Ili Mwaka 2019 Uwe Wa Mafanikio Makubwa Kifedha Kwako.

Rafiki yangu mpendwa, Watu husema ya kwamba kauli zinaumba. Kile unachofikiri na kusema muda mrefu, ndiyo kinachotokea kwenye maisha yako. Hapo ulipo sasa ni matokeo ya fikra ambazo umekuwa nazo kwa muda mrefu na kauli ambazo umekuwa unazitumia. Na linapokuja swala la fedha, zipo kauli nyingi ambazo umekuwa unatumia na zinachangia wewe kubaki kwenye umasikini.... Continue Reading →

Ishi Kwa Tabia Hizi Kumi (10) Kila Siku Ya Maisha Yako Na Utaweza Kupata Mafanikio Makubwa Sana Kwenye Maisha Yako.

Rafiki yangu mpendwa, Mtu mmoja amewahi kusema kwamba huwa tunajenga tabia, kisha tabia zinatujenga. Na hili ni kweli kabisa. Mwanzoni wakati tunajifunza tabia yoyote ile, iwe nzuri au mbaya huwa tunaweka kazi hasa. Lakini baadaye ikishakuwa tabia tunajikuta tunafanya bila hata ya kufikiri. Maisha yetu yapo pale yalipo sasa kutokana na tabia ambazo tumejijengea siku... Continue Reading →

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑