Hivi Ndivyo Tabia Zako Binafsi Zinavyoiathiri Biashara Yako Na Kuizuia Kukua Zaidi.

Rafiki yangu mpendwa, Nimekuwa nakuambia sana jambo hili moja kuhusu biashara, kwamba biashara ni kiumbe hai, ambacho kinazaliwa, kinakua au kudumaa na mwishowe kinakufa. Biashara ni kitu ambacho kina maisha yake ya kujitegemea na jinsi ambavyo kinapewa uhuru wake ndivyo inavyofanikiwa zaidi. Lakini pia biashara huwa inakuwa na tabia zake, ambazo zinaweza kuifanya ifanikiwe zaidi... Continue Reading →

Hii Ndiyo Hatua Moja Wanayoiruka Watu Wengi Wanapoingia Kwenye Biashara, Ambayo Inakuja Kuwagharimu Sana Mbeleni.

Rafiki yangu mpendwa, Watu wengi wanaoingia kwenye biashara ndogo huwa wanaruka hatua moja muhimu sana ambayo huja kuwagharimu mbeleni. Watu hawa huwa wanakuwa na wazo zuri la biashara, wanapambana kupata mtaji ili kuingia kwenye biashara hiyo. Wanakuwa na hamasa kubwa ya kuingia kwenye biashara hiyo na wanategemea kupata uhuru mkubwa wa maisha yao kutoka kwenye... Continue Reading →

Tabia Hizi Ishirini (20) Unazoziishi Kila Siku Ndiyo Zinazokuzuia Usifanikiwe Zaidi. Zijue Na Hatua Za Kuchukua Ili Upate Mafanikio Makubwa.

Rafiki yangu mpendwa, Mafanikio yetu yanawategemea sana watu wengine. Nimekuwa nasema kwenye mafanikio hakuna jeshi la mtu mmoja, kwamba mtu mmoja anajitengenezea mafanikio yake mwenyewe, huo ni uongo. Ili ufanikiwe watu wengine wanahusika sana kukuwezesha wewe kupiga hatua. Kama ni kwenye kazi basi walio juu yako, walio ngazi sawa na wewe na hata walio chini... Continue Reading →

Makosa Haya Matano (05) Pekee Ndiyo Yanayoua Kila Aina Ya Biashara, Yajue Na Yaepuke Ili Biashara Yako Isife.

Rafiki yangu mpendwa, Ulimwengu wa biashara siyo lele mama. Biashara zimekuwa na changamoto nyingi mno, hasa katika zama hizia ambazo kila mtu anaweza kufanya kila aina ya biashara anayotaka kufanya. Sasa hivi kuingia kwenye biashara imekuwa rahisi sana, huhitaji hata kuwa na eneo, mtandao wa intaneti umerahisisha sana ufanyaji wa biashara. Unaweza kuwa na huduma... Continue Reading →

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kujijengea Uzoefu Mkubwa Kwenye Kile Unachofanya Na Kuweza Kufanikiwa Sana.

Rafiki yangu mpendwa, Watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba kufanya kitu kwa muda mrefu ndiyo wanapata uzoefu na kuwa bora zaidi. Na hata matangazo mbalimbali ya kazi huwa yanasisitiza kwenye hilo la uzoefu. Wataandika tunataka mtu lakini awe na uzoefu wa miaka kadhaa kwenye kazi hiyo. Kadhalika watu wamekuwa wanajisifia kwamba wana uzoefu mkubwa kwa sababu... Continue Reading →

Eneo Moja Ambapo Biashara Nyingi Zinakwama Na Jinsi Ya Kulivuka Ili Biashara Yako Ifanikiwe.

Rafiki yangu mpendwa, Pamoja na msisitizo mkubwa unaowekwa kwa watu kuingia kwenye biashara na ujasiriamali, njia hii siyo rahisi kama wengi wanavyofikiri wakati wanaingia. Ni njia nzuri inayoweza kukupa uhuru, lakini kabla hujapata uhuru huo utapitia mateso makali. Watu wengi huwa wanafikiria kwamba ukishakuwa na wazo zuri la biashara, ukawa na mtaji wa kutosha na... Continue Reading →

Mahitaji Makuu Manne (04) Ya Watu Ambayo Kila Mjasiriamali Anapaswa Kuyafahamu Na Kuyatimiza.

Rafiki yangu mpendwa, Mafanikio kwenye biashara na ujasiriamali hayaanzii kwako mwenyewe, bali yanaanza kwa wale ambao unawahudumia. Hii ina maana kwamba, kama unataka kufanikiwa kwenye biashara na ujasiriamali, basi unapaswa kwanza kuwawezesha wengine wafanikiwe. Biashara na ujasiriamali ni eneo ambalo halihitaji ubinafsi hata kidogo. Ni eneo ambalo linakutaka ujali kwanza kuhusu wengine kabla hujajali kuhusu... Continue Reading →

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑