Moja ya kitu ambacho kinatupa matatizo binadamu wote ni fedha. Matatizo ya fedha hayapo tu kwenye utafutaji bali hata kwenye matumizi, utunzaji na uwekezaji wa fedha.

  Tunaona watu wengi wanateseka sana kupata fedha ila baada ya kuzipata wanajikuta hakuna la maana wanalofanya na mwishowe wanabaki na matatizo yaleyale.(soma; tatizo sio fedha tatizo ni wewe)

gold

  Katika maisha yako kuna kipindi umewahi kupanga ukipata kiasi fulani cha fedha basi mambo yako yatakwenda vizuri. Ama kipato chako kikiongezeka na kufikia kiwango fulani basi hutosumbuka tena na fedha. Ila kwa bahati mbaya ulipata kiwango hicho cha fedha na matatizo ndio yakaongezeka zaidi.

  Huenda unatamani sana kujiwekea akiba ili baadae uweze kuwekeza na huenda ulishajidunduliza ila ukawekeza sehemu fulani na kujikuta umepoteza fedha zako zote.(soma; unawalipa watu wote kasoro huyu mmoja wa muhimu)

  Umekuwa ukitamani kuanzisha biashara zako ili kuondoka kwenye ajira ama kujikwamua kimaisha. Tatizo kubwa unalolalamikia mpaka sasa ni mtaji. Unafikiri kama ukipatiwa mtaji wa kiasi fulani basi utaanzisha biashara zako na mambo yako yatakwenda vizuri.

  Kama umepitia ama unapitia moja kati ya mambo hayo hapo juu una matatizo. Matatizo hayo sio kosa lako bali ni kutokujua sheria za fedha zinazotumika kote ulimwenguni kwa zaidi ya miaka elfu mbili sasa.

  Sheria hizo za fedha zimeelezwa katika kitabu cha MTU TAJIRI WA BABELI(The richest man in Babylon). Ni kitabu kifupi kilichojaa mafundisho mazuri kuhusu utafutaji, uhifadhi na uwekezaji wa fedha.

babylon

  Katika kitabu hiki imeelezwa tiba saba za mifuko iliyosinyaa, sheria tano za fedha, kuhifadhi asilimia kumi ya mapato yako na mbinu nyingine nyingi.

  Nimeshawatumia watu wengi kitabu hiki tokea mwezi wa kwanza mwaka 2013. Huenda nimeshakutumia ila bado hujakisoma, nakusihi kisome kitabu hiki kabla mwaka huu haujaisha. Ni kitabu kifupi ambacho unaweza kukisoma kwa siku moja au mbili kama utakisoma kwa masaa mawili au zaidi.

  Kama hujakipata kitabu hiki bonyeza hayo maandishi hapo chini kukidownload.

MTU TAJIRI WA BABELI(The richest man in Babylon).

  Kama umeshakisoma kitabu hiki tafadhali tushirikishe ni kipi ulichojifunza kutoka kwenye kitabu hiki. Tafadhali weka maoni yako hapo chini kuhusiana na kitabu hiki au jambo lolote.

  Nakutakia kila la heri katika msimu huu wa sikukuu. Kumbuka kuwa mwangalifu katika msimu huu(soma; mambo matano muhimu ya kuzingatia msimu huu wa sikuu)