UCHAMBUZI WA KITABU; Born To Win (Umezaliwa Kushinda, Ijue Siri Yako Ya Mafanikio)

Kila mtu amezaliwa na uwezo mkubwa sana ndani yake, kila mtu ana vipaji vya kipekee na kila mtu anaweza kuwa mshindi kwenye maisha yake.

Lakini dunia imefanya kazi moja kubwa ya kutuaminisha kwamba siyo kila mtu anaweza kufanikiwa. Hivyo wachache wameweza kufanikiwa huku wengi wakiishia kuwa na maisha ya kawaida ambayo hawayapendi wala kuridhika nayo.

Kazi kubwa ambayo aliyekuwa mwandishi, mzungumzaji na mhamasishaji Zig Zigler aliifanya katika kipindi cha uhai wake, ni kuwapa watu maarifa sahihi na hamasa ya kuweza kuchukua hatua ili kuweza kufikia ushindi ambao upo ndani yao.

Ni katika kitabu hichi cha Born To Win ambapo Zig Zigler na mwanae Tom Zigler wanatushirikisha njia sahihi ya kila mmoja wetu kuweza kuwa mshindi kwenye maisha yake.

Zigler anasema kwamba umezaliwa kushinda, lakini ili uweze kushinda unahitaji kwanza upange kushinda, ujiandae kushinda kisha ndiyo utegemee kushinda.

Kitabu hichi kimegawanyika katika sehemu kuu tatu;

Sehemu ya kwanza ni kujipanga kushinda.

Hapa Zigler anatupa msingi muhimu wa kufikia ushindi ambayo ni kuwa na maono makubwa, kuwa na malengo na pia kuwa na shauku kubwa ya kushinda. Bila ya vitu hivyo huwezi kushinda kamwe.

Sehemu ya pili ni kujiandaa kushinda.

Hapa Zigler anatuambia vitu tunavyohitaji ili kuweza kufikia ushindi. Anatushirikisha ujuzi tunaopaswa kuwa nao, elimu tunayohitaji na hata ushauri tunaohitaji kutoka kwa wengine.

Sehemu ya tatu ni kutegemea kushinda.

Baada ya kupanga kushinda, kisha kufanya maandalizi ya kushinda, kinachofuata ni kufanyia kazi mpango wa ushindi na kutegemea kupata matokeo mazuri ya ushindi. Kuna nguvu kubwa sana kwenye matarajio, na hapa ndipo mtazamo chanya unapofanya kazi yake.

born to win

Karibu sana kwenye uchambuzi huu wa kitabu na panga pia kusoma kitabu hichi. Kila mshindi anapaswa kusoma kitabu hichi, kwa sababu kina mkusanyiko wa kazi zote bora za Zig Zigler.

 1. Shauku ni mama wa hamasa.

Ili uweze kushinda, unahitaji kitu kimoja muhimu sana, hamasa ya kuweza kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata kile unachotaka. Bila ya hamasa hutafika mbali, changamoto zitakuangusha mara moja.

Hamasa inatokana na shauku kubwa ambayo mtu anakuwa nayo juu ya kitu. Kama una shauku, una hamu kubwa kweli ya kupata kitu, basi lazima utakuwa na hamasa ya kuchukua hatua ili kukiupata.

Hivyo hatua ya kwanza kabisa ya kufikia ushindi ni kuwa na hamu na shauku ya kushinda.

 1. Maono makubwa yanatengeneza hamu na shauku.

Tumeona ya kwamba ili uweze kuwa na hamasa kubwa ya mafanikio, unahitaji kuwa na hamu na shauku kubwa. Lakini je shauku hii inatoka wapi? Je wapo watu ambao wamezaliwa na shauku na ndiyo maana wanafanikiwa?

Swali ni hakuna anayezaliwa na shauku, bali kila mmoja anaweza kuizaa shauku. Na shauku inazaliwa kutoka kwenye maono makubwa ambayo mtu anakuwa nayo.

Ili uweze kushinda, unahitaji kuwa na maono makubwa ambayo yanakupa shauku inayoleta hamasa ya kuweka juhudi ili ufanikiwe. Angalia wote waliofanikiwa, huwa wanaanza na maono makubwa.

 1. Kujitoa na ung’ang’anizi ni muhimu kwa ushindi.

Siyo kwamba ukishakuwa na maono makubwa, utakuwa na shauku halafu hamasa inakupeleka moja kwa moja kwenye mafanikio. Dunia haifanyi kazi hivyo. Pamoja na maono makubwa unayoweza kuwa nayo, pamoja na mipango mikubwa unayoweza kuweka, utakutana na changamoto nyingi mno kwenye safari yako ya ushindi.

Na hapa ndipo unapohitaji vitu viwili muhimu sana, kujitoa na ung’ang’anizi.

Lazima ujitoe kweli ya kwamba unataka kushinda na hakuna chochote cha kukuzuia wewe kushinda.

Lazima kia uwe king’ang’anizi, lazima uendelee kuweka juhudi licha ya kukutana na changamoto na hata kushindwa.

 1. Maeneo saba muhimu ya maisha ya mafanikio.

Watu wengi wanaposikia kuhusu mafanikio hufikiria fedha na mali. Tunakazana kupata fedha na mali nyingi tukiamini hayo ndiyo mafanikio. Lakini je yafaa nini iwapo utapata fedha nyingi halafu afya yako ikawa mbovu? Au ukawa na mali za kutosha lakini huna maelewano na familia yako?

Mafanikio ya kweli yanahusisha maeneo saba ya maisha, lazima ufanikiwe kwenye maeneo yote ili kuwa na mafanikio ya kweli.

Eneo la kwanza ni afya yako binafsi, lazima uijali na kuilinda.

Eneo la pili ni familia yako, hawa ni watu muhimu sana kwako.

Eneo la tatu ni akili, lazima uiendeleze vizuri.

Eneo la nne ni fedha, lazima uwe na uhuru wa kifedha.

Eneo la tano ni wewe binafsi, lazima ujijali na kupata yale muhimu kwako.

Eneo la sita ni roho, lazima uwe mtu wa imani.

Eneo la saba ni kazi/biashara, lazima ufanye kile ambacho kina mchango kwa wengine.

Ukifanikiwa maeneo machache na kushindwa mengine, huna maisha ya mafanikio.

 1. Mambo sita yanayojenga msingi wa maisha ya mafanikio.

Watu wengi wamekuwa wanataka kufanikiwa, lakini hawazingatii misingi. Hufikiri mafanikio ni kitu kinachoweza kutokea tu kama bahati. Hapa yapo mambo sita muhimu yanayojenga msingi wa mafanikio;

Moja; uaminifu, lazima uwe mtu wa kutekeleza kile ulichoahidi, kufanya kama ulivyosema.

Mbili; tabia, tabia yako lazima iwe njema na yenye kuwapendeza watu. Watu wajisikie vizuri kujihusisha na wewe kutokana na tabia zako nzuri.

Tatu; imani, lazima uwe na imani ya kwamba unaweza kufanikiwa na unaweza kufanya makubwa.

Nne; uadilifu, unachofanya mbele ya watu na unachofanya ukiwa mwenyewe, lazima viwe vinaendana. Usiwe na maisha ya aina mbili.

Tano; upendo, lazima upende unachofanya na uwapende wengine pia.

Sita; kutunza imani ya wengine kwetu. Unapaswa kuwafanya wengine wajisikie salama kukuamini kwamba utatunza imani waliyoiweka juu yako.

Bila ya msingi huu imara wa mafanikio, huwezi kuwa na maisha ya ushindi.

SOMA; KITABU CHA JULY; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.

 1. Malengo yanakuwezesha kukaa kwenye njia moja ya mafanikio.

Safari ya maisha ya ushindi ina vishawishi vingi. Pamoja na kuwa na maono makubwa, zipo njia nyingi ambazo zinaweza kukushawishi uzitumie kufikia maono yako. Kama utafuata kila njia, hutaweza kufanikiwa.

Hapa ndipo unapaswa kuwa na malengo ambayo yanaonesha ni njia ipi unachukua, kipi unafanya na kwa wakati gani. Unapokuwa na malengo ambayo unayafuata na kuyafanyia kazi, unakuwa kwenye njia sahihi na kuepuka vishawishi vinavyokupotezea muda.

 1. Unahitaji kuchukua hatua kila siku.

Watu wengi wamekuwa wakifikiri kwamba kuna kitu kimoja tu ambacho ukishakifanya basi unafanikiwa. Wengi wamekuwa wanakimbizana na siri za mafanikio, wakiamini kuna siri ambayo wao hawajaijua na wakishaijua basi hawatakuwa na haja ya kuhangaika tena.

Kama siri ipo basi ipo wazi kabisa, ya kwamba ili kufanikiwa, lazima uchague kile unachotaka, halafu uwe tayari kuchukua hatua kila siku, KILA SIKU. Mafanikio ni mkusanyiko wa mambo madogo madogo yaliyorudiwa rudiwa kufanywa na siyo jambo kubwa lililofanywa mara moja.

Hivyo chochote unachotaka kufanya na unataka kufanikiwa, kama hupo tayari kufanya kila siku kwa maisha yako yote, sahau kuhusu ushindi na mafanikio.

 1. Thamani na kusudi vitakupa kichocheo cha kufanya kila siku.

Kuweza kufanya kitu kila siku kwa maisha yako yote siyo rahisi, wengi hukata tamaa na kuacha baada ya muda.

Vipo vitu viwili ambavyo vinaweza kukupa kichocheo cha kuendelea kufanya kila siku;

Cha kwanza ni thamani unayotoa, unapoona thamani unayotoa na namna inavyowasaidia wengine, unapata hamasa ya kuendelea kufanya zaidi ili kuwasaidia wengi zaidi.

Cha pili ni kusudi, unapojua kusudi la maisha yako na kulifanyia kazi, utaendelea kufanya kila siku.

Jua ni thamani gani unatoa kwa wengine na pia jua kusudi la maisha yako. Hivi vitakuwezesha wewe kuweza kufanya kila siku.

 1. Swali muhimu la kujua kusudi la maisha yako na kutengeneza maono yako.

Swali hilo ni KWA NINI?

Kwa nini upo hapa duniani?

Kwa nini unafanya kile ambacho unafanya?

Swali la kwa nini linakupa fursa ya kujiangalia ndani na kupata sababu halisi ya kwa nini upo hapa duniani na kwa nini unafanya yale unayofanya. Unapoweza kujibu swali hili unapata kusudi la maisha yako na kuweza kutengeneza maono makubwa ya maisha yako.

 1. Upo tayari kushindwa?

Japokuwa umezaliwa kushinda na una kila kinachokuwezesha kushinda, maisha yako hayatakuwa ushindi pekee. Kuna wakati utakutana na kushindwa, hasa pale unapohitajika kujaribu mambo mapya, ambayo huna uzoefu wa kuyafanya.

Wale ambao wanaogopa kushindwa huwa hawajaribu mambo mapya, na hivyo kujizuia kabisa kushinda.

Wale wanaojaribu mambo mapya, na kuwa tayari kushindwa, hushindwa, lakini pia hujifunza na hivyo kushinda zaidi baadaye.

Usiogope kujaribu mambo mapya na hata yanayoweza kuonekana hatari kama unataka kushinda.

SOMA; NYEUSI NA NYEUPE; Kizazi Cha Alama A+ Na Zawadi Ya Kushiriki.

 1. Maamuzi mabovu yana madhara makubwa kuliko unavyofikiri.

Iwapo ungejua nguvu kubwa ya maamuzi unayofanya kwenye maisha yako, usingekuwa unafanya maamuzi kirahisi rahisi tu. Wengi hukimbilia kufanya maamuzi, ambayo huwa ni mabovu na yanawaharibia zaidi.

Kwa mfano, unapofanya maamuzi mabovu, unapata matokeo mabovu, matokeo hayo mabovu yanapelekea hali yako kuwa mbaya, na ukishakuwa na hali mbaya unakuwa huna namna, unaona hakuna tena unachoweza kufanya.

Lakini kwa upande wa pili, ukifanya maamuzi bora, unapata matokeo mazuri, ambayo yanafanya hali yako kuwa nzuri na kuona mambo mazuri zaidi ya kufanya.

Kuwa makini sana na maamuzi unayofanya.

 1. Chagua marafiki na wanaokuzunguka kwa umakini mkubwa.

Sababu kubwa inayowazuia wengi kufanikiwa ni maoni ya wale ambao wamewazunguka. Unaweza kuwa na mipango mikubwa sana ya mafanikio, lakini kama umezungukwa na watu waliokata tamaa, watakukatisha tamaa na hutaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Watu wengi ambao wana mtazamo hasi na waliokata tamaa huwa hawafanikiwi, hivyo chunga sana hawa wasiwe watu wa karibu kwako, maana hawatakuruhusu wewe ufanikiwe.

 1. Unahitaji elimu sahihi ya mafanikio.

Huwezi kufanikiwa kama hujielimishi kwa maarifa sahihi. Maarifa sahihi yanakuwezesha wewe kuona kule unakokwenda na kukuwezesha kuamka tena pale unapoanguka.

Katika safari ya mafanikio, kuanguka ni swala la kawaida, unahitaji elimu sahihi ili uweze kuinuka na kuendelea na safari.

 1. Elimu pia inayafungua macho yako kuziona fursa.

Jambo moja la kushangaza kuhusu fursa ni kwamba, zipo mbele yetu kila siku, tena pale pale ambapo tupo. Lakini wengi hatuzioni kwa sababu macho yetu hayajui jinsi ya kuziona fursa hizi.

Elimu sahihi inakuwezesha wewe kuziona fursa ambazo tayari zipo mbele yako. Kadiri unavyokuwa na ufahamu mkubwa juu ya jambo lolote, ndivyo unavyoweza kuziona fursa nyingi zaidi hata kama wengine hawaoni.

Hivyo chochote unachofanya, hakikisha unakijua vizuri sana. Hilo litakuwezesha wewe kuziona fursa nyingi zaidi.

 1. Kabla hujategemea kushinda, lazima uwekeze ndani yako kwanza.

Hakuna mafanikio bila ya uwekezaji ndani yako. Na uwekezaji tunaozungumzia hapa ni uwekezaji wa maarifa na taarifa sahihi za mafanikio.

Lazima uwe mtu wa kujifunza kila siku na kila wakati. Lazima usome vitabu, usome makala na machapisho yanayohusu kile unachofanya na mafanikio kwa ujumla.

Na muhimu zaidi, pale unapokuwa kwenye safari, geuza safari yako kuwa chuo cha kujifunza. Fanya hivyo kwa kusikiliza vitabu vilivyosomwa na hivyo kujifunza huku ukiendelea na safari yako.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; THINK LIKE A CHAMPION (Fikiri Kama Mshindi, Elimu Isiyo Rasmi Kuhusu Biashara Na Maisha.)

 1. Ubora unatokana na kufanya.

Huwezi kuwa bora kama hufanyi, huwezi kuwa bora kwa kujifunza na kupanga pekee. Hata kama ungejifunza na kujua kwa kiasi gani, unapoanza kufanya lazima utakosea. Lakini kadiri unavyoendelea kufanya, unazidi kuwa bora zaidi na zaidi.

Jua kipi unachotaka, na anza kuweka kwenye vitendo, kila wakati kazana kuwa bora zaidi ya wakati uliopita, hii itakupeleka kwenye mafanikio.

 1. Sehemu mbili za kupata uzoefu.

Uzoefu ni muhimu sana kwenye mafanikio, lazima kuwa na uzoefu wa mambo gani ya kufanya na yapi siyo ya kufanya ili kuweza kufanikiwa.

Tunaweza kupata uzoefu kutoka sehemu mbili;

Moja; kutokana na makosa yetu wenyewe, hapa inatubidi tufanye makosa na kujifunza. Uzoefu huu una gharama kubwa na unachukua muda kuupata, kwa sababu huwezi kujaribu kila kitu.

Mbili; uzoefu wa wengine, hapa unajifunza kutoka kwa wengine na kupata ushauri wao pia. Huu ni uzoefu usio na gharama na hauhitaji muda kuweza kuupata.

Changamoto ni kwamba watu wengi huwa hawapendi kupokea ushauri, wanaamini wao wanajua kuliko wengine na hivyo kurudia makosa ambayo yameshafanywa na wengine.

 1. Kuwa mchimbaji wa ushauri.

Japokuwa unahitaji ushauri ili kufanikiwa, siyo kila ushauri unakufaa wewe, hata kama unatolewa na mtu gani.

Kupata ushauri ni sawa na kuchimba dhahabu. Ili upate kilo moja ya dhahabu utachimba sehemu kubwa sana ya ardhi, utahitajika kuondoa uchafu mwingi mno, lazima ichomwe na kuchujwa ndiyo ipatikane dhahabu safi.

Hivyo ndivyo ilivyo kwenye ushauri pia, kuna ushauri mwingi unahitaji kuutupa ili kuweza kubaki na ule ushauri mzuri na wenye thamani kwako.

 1. Sifa saba za washauri wazuri.

Unahitaji kuwa na mshauri au mtu unayemsikiliza kwenye maisha yako. Huyu anaweza kuwa menta wako, kocha wako au hata mtu unayependa kuwa kama yeye.

Ili kupata mtu atakayekusaidia, angalia sifa hizi saba muhimu;

Moja; awe na tabia nzuri, ambayo upo tayari kuiiga.

Mbili; awe na historia nzuri ya mafanikio kwenye yale anayofanya.

Tatu; awe msikilizaji mzuri na siyo mtu wa kuongea pekee.

Nne; awe mtu wa kufanya maamuzi mazuri.

Tano; awe mtu ambaye anasema ukweli mara zote, hata kama unakuumiza.

Sita; awe na mahusiano mazuri na watu wengine.

Saba; awe anafurahia mafanikio ya watu wengine, asiwe na wivu pale wengine wanapofanikiwa.

Inaweza kuwa vigumu kumpata mtu mmoja mwenye sifa zote hizo saba, lakini kama mtu hana sifa hata moja kati ya hizo saba, usichukue ushauri wowote anaokupa, utakuangamiza.

 1. Baada ya kupanga na kujiandaa, sasa tegemea kushinda.

Wanaweza kuwepo watu wawili, wenye elimu sawa na wote wanafanya kazi au biashara ya aina moja. Baada ya muda unakuta mmoja kafanikiwa sana na mwingine akaishia kuwa kawaida. Tofauti kubwa huwa inaanzia kwenye mategemeo. Wale wanaoshinda huwa wanategemea kushinda. Baada ya kuwa wamejipanga vizuri kisha wakafanya maandalizi mazuri, wanajua lazima watapata matokeo mazuri kwenye maisha yao.

Ili kuwa na mategemeo ya ushindi, lazima uwe mtu chanya, ambaye una mtazamo chanya na kwenye kila jambo unaangalia upande chanya. Ukiwa mtu hasi unakata tamaa na huwezi kuendelea na safari ya mafanikio.

 1. Maeneo matatu unayohitaji kuyafanyia kazi kwa mafanikio yako.

Sisi binadamu tumegawanyika katika sehemu kuu tatu, zote ni muhimu na zinashirikiana sana katika kuwa na maisha ya mafanikio.

Sehemu ya kwanza ni mwili, hapa unahusisha afya yako ya mwili, ambapo unahitaji kuulisha mwili wako vizuri na kuulinda kiafya.

Sehemu ya pili ni akili, ambapo unahusisha fikra zako, hapa unahitaji kuzitengeneza vizuri, ziwe chanya na uendelee kujifunza.

Sehemu ya tatu ni roho, hapa unahusisha imani, lazima uwe mtu wa imani, uweze kukua kiroho ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha.

Bila ya maendeleo na ukuaji kwenye maeneo hayo matatu, huwezi kuwa na maisha ya mafanikio.

Kama nilivyokuambia rafiki, hichi ni kitabu muhimu sana kusoma kwa sababu kila mmoja wetu anapenda kuwa mshindi na kupiga hatua zaidi kwenye maisha yake. Pata muda usome kitabu hichi, utajifunza mengi ya kufanyia kazi kwenye maisha yako na kuweza kweli KUWA MSHINDI KAMA AMBAVYO UMEZALIWA KUSHINDA.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

MIMI NI MSHINDI

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz

 

UCHAMBUZI WA KITABU; Raising Positive Kids In A Negative World (Jinsi Ya Kulea Watoto Wenye Mtazamo Chanya Kwenye Dunia Hasi).

Hakuna awezaye kubisha kwamba tunaishi kwenye dunia ambayo ni hasi. Dunia ambayo ukisoma gazeti, kuangalia TV, kusikiliza redio au kuperuzi mitandao ya kijamii, kipaumbele kikubwa ni habari mbaya na zenye kutia hofu.

Tunaishi kwenye dunia ambayo matumizi ya madawa ya kulevya, ulevi na matendo ya ngono na ubakaji yanazidi kuwa mengi.

Dunia hii imekuwa changamoto mno katika malezi ya watoto. Na kwa kuwa hakuna darasa lolote linalofundisha njia bora ya kulea watoto hatua kwa hatua, wazazi wengi wamekuwa wanalea watoto wao kwa mazoea, kitu ambacho ni hatari kwa mazingira ya sasa.

Zig Zigler ambaye alikuwa mwandishi na mhamasishaji mkubwa enzi za uhai wake, aliandika kitabu hichi cha How To Raise Positive Kids In A Negative World, ambapo toleo la kwanza lilitoka mwaka 1985. Lakini changamoto za kipindi hicho, mpaka sasa zipo na zinazidi kuwa kubwa zaidi.

Zigler, kupitia kitabu hichi, anatupa darasa muhimu la kuwalea watoto wetu, ili waweze kuwa na maisha mazuri na yenye mafanikio. Lakini Zigler anaweka nguvu nyingi ya kutusaidia sisi wazazi kuwa na mafanikio kwanza kwa sababu, watoto wanajifunza kwa kuiga yale wazazi wanafanya kuliko wanayosema.

Hichi ni kitabu ambacho kila mtu mwenye mtoto au anayetarajia kuja kuwa na watoto anapaswa kukisoma. Kila ukurasa wa kitabu hichi una madini muhimu kwenye malezi ya watoto.

raising positive kids

Karibu sana kwenye uchambuzi huu wa kitabu hichi kizuri cha malezi, pamoja na uchambuzi huu, pata kitabu hichi na kisome.

 1. Mtazamo wa wazazi unaathiri mtazamo wa watoto.

Watoto wanajifunza kwa kuiga tabia za wazazi kuliko kusikia kile wanachowaambia. Iwapo wewe kama mzazi utakuwa na mtazamo hasi, huo ndiyo mtazamo ambao mtoto ataubeba kwenye maisha yake. Haijalishi utampa moyo kiasi gani na kumwandaa kuwa chanya, kama wewe mwenyewe haupo chanya, unajisumbua.

Hivyo usipoteze muda wako kumwandaa mtoto kuwa chanya kama wewe upo hasi. Na wala usiseme unataka kulea watoto wako wawe na mafanikio wakati wewe hujafanikiwa. Kuyajenga maisha yako katika msingi wa mafanikio kutawanufaisha sana watoto wako.

 1. Malezi ya watoto yanahitaji viungo vingi.

Tofauti na wazazi wengi wanavyolea watoto kwa mazoea, malezi bora ya watoto yanahusisha viungo vingi ambavyo kila mzazi lazima awe navyo. Baadhi ya viungo hivyo ni upendo, nidhamu, uadilifu, kusamehe na vingine. Vyote hivi lazima viwe kwa kila mzazi ili kuweza kuwasaidia watoto kuwa watu bora.

Kwa maana hii, kulea watoto chanya na watakaokuwa na mafanikio makubwa, siyo zoezi rahisi ndiyo maana wengi hukata tamaa na kuacha watoto waende tu kama wanavyoenda.

 1. Misingi miwili muhimu ya kulea watoto chanya.

Msingi wa kwanza; upo hapo ulipo na hivyo ulivyo kutokana na kile ambacho umejifunza siku za nyuma. Ukitaka kuwa tofauti na ulivyo sasa, lazima ubadili kile kinachoingia kwenye akili yako. Kadhalika kwa watoto, kile wanachoingiza kwenye akili zao, kinajitokeza kwenye matendo yao.

Msingi wa pili; maisha ni magumu kwa kila mtu, lakini ukiwa mgumu kwako binafsi, maisha yanakuwa rahisi kwako. Hili linahitaji nidhamu ya hali ya juu sana, na ni muhimu kila mzazi kuwaandaa watoto kwa hilo. Watoto waelewe kwamba dunia siyo rahisi, hata kama wana nafasi kubwa kiasi gani.

 1. Kuna kitu kikubwa ndani ya kila mtoto.

Kila mzazi anapenda mtoto wake awe na malezi mazuri na baadaye aje afanikiwe. Wazazi wengi wanajitahidi sana kuhakikisha watoto wanapata malezi hayo bora, lakini bado maisha yao yanakuja kuwa magumu. Hii ni kwa sababu wengi wanakuwa hawajajua nini kipo ndani ya watoto wao. Wanakuwa hawajajua uwezo wake mkubwa na kuuendeleza, badala yake wanawalazimisha kuwa watu wengine tofauti.

Katika kuwalea watoto wako kuwa chanya na wenye mafanikio, kwanza jua uwezo mkubwa ambao upo kwa kila mtoto, kisha msaidie kwenye kufikia uwezo huo. Atakuwa na maisha bora sana.

 1. Ulimwengu hasi ukoje?

Ulimwengu hasi umejawa na kauliza kushindwa na kukata tamaa. Hizi ni kauli ambazo mzazi anaweza kuwa anatumia kila siku, kwa mazoea lakini zinajenga mtazamo hasi kwa mtoto na anaiona dunia kwa mtazamo wa tofauti.

Kila kitu kinachukuliwa kwa hali ya kutisha na ya hatari. Kila taarifa ya habari ina habari za kifo, wizi, ajali na kadhalika. Na kila mtu anapotaka kufanya jambo, anaanza kwa kujiambia kwamba hawezi au atashindwa.

Haya yote yanazalisha watu ambao wapo hasi na hawawezi kufanikiwa kamwe.

SOMA; Ifahamu Sehemu Iliyogeuka Kuwa Kimbilio La Wazazi Wengi Katika Malezi Ya Watoto.

 1. Kuangalia TV kusikodhibitiwa ni sumu kwa mtoto.

Iwapo mtoto anaangalia TV anavyojisikia yeye mwenyewe, bila ya usimamizi wa mzazi, mtoto huyo yupo kwenye hatari kubw aya kuharibika, hasa kwa wale wadogo ambao wanapenda kujaribu kila wanachojifunza.

Huwezi kuangalia TV za kawaida ikapita dakika kumi watu hawajagombana, kufanya mapenzi, kunywa pombe au jambo lolote hasi kutokea.

Ni wajibu wako mzazi kuchagua vipindi gani mtoto anaweza kuangalia, ambavyo vina maadili na mtoto anajifunza kadiri ya umri wake.

 1. TV pia zinaharibu afya za watoto.

Mtoto anapotumia muda mwingi kuangalia TV, hapati muda wa kutosha wa kucheza na wengine. Hivyo anakosa ule uchangamfu wa utoto, muda wote amekaa na hata afya yake inakuwa siyo nzuri, anaweza kuwa na uzito unaopitiliza, hasa pale anapoangalia TV huku akila.

Ni jukumu la mzazi kumfanya mtoto apende michezo inayohusisha mazoezi ya viungo, hii pia itamsaidia kujenga ushirikiano na wengine. Na wakati mwingine, wewe mzazi cheza na watoto wako.

 1. Njia bora ya kumlinda mtoto dhidi ya wabakaji na walawiti.

Matukio ya watoto kutekwa, kubakwa na kulawitiwa yanazidi kuwa mengi katika nyakati hizi. Matukio haya yanafanywa na watu ambao ni wa karibu kabisa kwa mtoto au wenye mamlaka ambayo watoto hawawezi kuyapinga.

Njia bora ya kuepusha hili ni kujua kila wakati mtoto wako yuko wapi, yuko na nani na anafanya nini. Usiruhusu kabisa mtoto wako kuwa eneo ambalo hujui, hata kama yupo na ndugu au mtu unayemwamini kiasi gani. Wengi wanaoharibu watoto ni watu wanaoaminika sana.

Kitu kingine muhimu ni kujenga ukaribu na mtoto ili asikufiche kitu chochote cha ajabu ambacho ameambiwa au ametaka kufanyiwa. Hili litakusaidia kukatisha mapema jaribio la kuharibiwa kwa mtoto, maana wengi wanaoharibu watoto, huanza kidogo kidogo ili kujenga uaminifu kwa watoto.

 1. Jua kuna vitu huwezi kuwafanyia watoto wako.

Kosa kubwa ambalo limekuwa linafanywa na wazazi, hasa wale ambao wana mafanikio makubwa, ni kufikiri wanaweza kufanya kila kitu kwa watoto wao. Hivyo hujaribu mpaka kununua matatizo ya watoto wao, wakiona wanawasaidia wasipate shida.

Lakini ukweli ni kwamba lazima watoto wajue maisha ni magumu na dunia ina changamoto. Lazima wajue wataumizwa, wataumwa, watakatishwa tamaa. Pia lazima wajue kwamba wakikosea dunia itawaadhibu kwa njia yoyote ambayo ni sahihi. Kwa kuwafundisha hayo, unawaandaa kukumbana na hali halisi ya dunia.

 1. Kama mafanikio yako yataharibu watoto wako, haina haja ya kufanikiwa.

Kumekuwa na jambo la kushangaza sana kwenye maisha ya zama hizi, watu wanakimbizana na mafanikio, hasa ya mali na fedha na kusahau kabisa kuhusu watoto wao. Wanafanya hivyo wakiamini kwamba wanawasaidia watoto kwa kuwa na maisha mazuri. Kumbe wanawaharibu zaidi watoto.

Watoto wanahitaji uwepo wa wazazi wao katika kipindi cha ukuaji wao kuliko kitu kingine chochote kile. Hivyo kama mafanikio kwako yanamaanisha kuwa mbali na familia yako, kukosa muda kabisa na watoto wako, mafanikio hayo hayatakuwa na maana yoyote kwako wala watoto wako.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; Boys Of Few Words (Jinsi Ya Kuwalewa Watoto Wa Kiume Wawe Na Mawasiliano Bora Na Mahusiano Mazuri Na Wengine.)

 1. Kama unampenda mtoto wako mpe MUDA.

Mapenzi kwa watoto ni muda na siyo kitu kingine chochote. Mtoto anapopata muda wako, hasa pale anapokuhitaji kweli, anafarijika mno. Mtoto anapoingia duniani, hasa pale anapoanza shule, anakutana na changamoto nyingi kila siku. Anahitaji mtu wa kumshirikisha changamoto hizo, ambaye atazielewa na kumsaidia kuzitatua. Kwa bahati mbaya mzazi anakuwa hayupo karibu, yupo bize na kazi na hata muda mchache anaopata, hawezi kutenga wa kukaa na watoto.

Hili linapelekea watoto kupata ushauri wao kwa watu wabaya, ambao wanawaharibu kwa kuwabaka, kuwalawiti, kuwafundisha ulevi na hata tabia nyingine mbaya.

 1. Tabia za mafanikio mtu unaweza kujifunza na kuwafundisha watoto.

Tabia zozote ambazo tunaziona kwa watu waliofanikiwa, tunaweza kuzijenga kwetu binafsi na pia kuwasaidia watoto wetu kuwa nazo pia. Lakini hili linahusisha kazi kubwa na hivyo lazima mzazi uwe tayari kwa kazi hii. Ukitaka kupeleka malezi kama wengi wanavyopeleka, ya kuacha mtoto aende anavyoenda, mtoto anakosa msingi muhimu wa maisha ya mafanikio.

Kwa kujifunza tabia hizi za mafanikio, unamsaidia mtoto kuweza kutambua na kutumia uwezo mkubwa ambao upo ndani yake.

 1. Watoto wanahitaji msingi imara wa maadili.

Bila ya maadili, watoto hawawezi kuwa na maisha mazuri, wataishia kwenye ulevi au jela. Dunia ina changamoto nyingi, mtoto akilelewa kwamba anaweza kwenda kama anavyotaka yeye, kupata kila anachotaka bila ya kipingamizi, ataishia pabaya mno.

Ni wajibu wa mzazi kumjengea mtoto msingi imara wa maadili ambao unahusisha uaminifu, kuheshimu sheria, kujali wengine na uvumilivu.

Katika kuwafundisha watoto maadili haya, tukumbuke kwamba watoto wanatuangalia kuliko wanavyotusikiliza. Kama unamfundisha mtoto kwamba uaminifu ni msingi muhimu kwenye maisha, halafu dakika chache baadaye anakusikia ukiongea na simu na kusema upo kazini wakati upo nyumbani, mtoto atabeba kile ulichofanya, kwamba kudanganya siyo jambo baya.

 1. Tabia nzuri ni usalama na mtaji wa kutosha.

Msingi muhimu sana ambao mzazi anapaswa kumjengea mtoto ni katika kujenga tabia nzuri. Mafanikio yoyote kwenye maisha, yanategemea zaidi kwenye tabia ambayo mtu anayo.

Mtoto anapolelewa kwa kujengewa tabia nzuri, kila mtu anamwamini na unakuwa usalama wake kwenye kazi na hata biashara. Pia tabia nzuri ni mtaji, kwa sababu watu wanathamini tabia nzuri kuliko kitu kingine chochote. Hakuna mtu mwenye tabia nzuri, mwaminifu ambaye amewahi kukosa kazi ya kufanya na akawa masikini kabisa.

 1. Wafundishe watoto kulinda majina yao na sifa zao.

Jina linabeba maana kubwa sana kwenye maisha ya mtu. Jina la mtu linapotajwa mahali, kuna picha ambayo watu wanaipata, hata kama mtu huyo hayupo.

Lazima watoto wafundishwe kulinda majina yao, kwa kuhakikisha yanaendana na sifa nzuri. Jina linapotajwa mahali, watu wawe na amani na kupata picha ya mtu mwaminifu na anayeweza kutegemewa.

Jina linaweza kumfanya mtu kuaminiwa na kupewa kitu ambacho wengine hawawezi kupewa. Wasaidie watoto kujenga na kulinda majina yao.

Katika kulinda majina yao, wasijihusishe kabisa na watu wenye sifa mbaya, wala kujaribu kufanya jambo lolote ambalo litaharibu sifa na majina yao.

 1. Angalia kitu kuzuri kilichopo kwa kila mtoto.

Wakati mwingine wazazi wanakata tamaa na kuona watoto hawawezi kuwa chanya na wenye mafanikio. Hili linatokana na mtoto kuwa na mapungufu mengi, labda anafeli shuleni, ni mtundu, hasikii na mengine mengi.

Lakini pamoja na yote hayo, kila mtoto ana kitu kizuri ambacho kipo ndani yake. Hata kama darasani anakuwa wa mwisho, kipo kitu ambacho anaweza kukifanya vizuri. Hapo ndipo mzazi unapotakiwa kuanzia katika kumlea mtoto mwenye mtazamo chanya na atakayefanikiwa.

Unapokazana kuangalia kitu kizuri ambacho kipo ndani ya mtoto, unaziona fursa nyingi za kumsaidia kuwa bora zaidi. Na hilo linampelekea yeye kuwa hasi, kuona kuna vitu anaweza na hata kufanikiwa kwenye maisha.

SOMA; Barua Ya Wazi Kwa Wazazi Wa Kizazi Kipya (Kama Una Miaka Chini Ya 40 Soma Hapa).

 1. Kumpuuza mtoto kuna matokeo mabaya kuliko kumkatisha tamaa.

Mwaka 1984 utafiti uliofanywa na Family Concern, ulihusisha watoto wa shule 60, ambao waligawanywa kwenye makundi matatu na kupewa majaribio ya mtihani wa hesabu kula siku kwa siku tano. Kundi la kwanza walikuwa wanasifiwa kila siku kwamba wana akili na wanafanya vizuri. Kundi la pili walikuwa wanakatishwa tamaa na kukosolewa kila siku. Na kundi la tatu waliachwa tu, hawakuambiwa chochote.

Matokeo sasa, wale waliosifiwa kila siku, matokeo yao yalikuwa yanakuwa bora zaidi kila siku. Wale waliokuwa wanakosolewa walionesha kuwa bora, lakini siyo sana ukilinganisha na waliosifiwa. Ila wale ambao hawakuambiwa chochote, matokeo yao hayakuwa na mabadiliko yoyote.

Utafiti huu unaonesha namna gani kuwapuuza watoto kunawafanya wakate tamaa na wasione uhitaji wa kuwa bora zaidi. Na hili ndilo linafanywa na wazazi walio wengi. Watoto wanakazana kufanya yao na wazazi wanafanya yao, hakuna msaada wa karibu watoto wanapata kutoka kwa wazazi, hasa kwenye masomo na changamoto nyingine.

 1. Kuwa chanya ni kazi ya kila siku, kama kuoga.

Inashangaza namna ambavyo watu wanachukulia kirahisi swala la kuwa chanya. Watu wanafikiri kwa kusoma kitabu kimoja, au kuhudhuria semina moja, basi wanatosha kuwa chanya na kufanikiwa.

Hivi ukioga mara moja ndiyo umetakata milele, au ukila mara moja basi umeshiba milele? Kama ambavyo tunaoga na kula kila siku, tunapaswa kujifunza kuwa chanya kila siku, kwa kusoma na kusikiliza vitu chanya kila siku. Kwa sababu kila siku dunia inatulazimisha kuwa hasi.

Tengeneza msingi huu kwa watoto wako pia, wawe tayari kujifunza kila siku na kuwa chanya.

 1. Njia ya uhakika ya kuwafanya watoto wako wasikose kazi.

Wajengee msingi wa kufanya zaidi ya wanavyolipwa. Dunia nzima inafanya kazi kwa uvivu, watu wanataka kupata zaidi ya kile wanachowekwa, na hili limesababisha wengi kukosa kazi, na hata wakianzisha biashara zinakufa. Ukitaka watoto wako wapate kazi wakati wote, na hata wakijiajiri wafanikiwe, basi wajengee msingi wa kufanya zaidi ya wanavyolipwa. Wawe tayari kwenda hatua ya ziada. Wakazane kutoa thamani zaidi badala ya kuangalia wanalipwa nini kwanza.

Ni sheria ya asili kwamba, pale mtu anapofanya zaidi ya anavyolipwa, wanafikia hatua ya kulipwa zaidi ya wanavyofanya. Dunia inaenda kinyume na sheria hii, wajenge watoto wako waende nayo vizuri.

 1. Malezi ya mtoto hayana kuchelewa.

Wakati sahihi wa kutoa malezi bora kwa mtoto wako ni wakati wowote ambao upo na mtoto wako. Na kama mtoto bado yupo chini yako, hujachelewa kwenye kumjengea misingi ya maisha ya mafanikio.

Japo kama watoto wameshakua na kujenga misingi tofauti, zoezi litakuwa gumu, lakini linawezekana. Hata kama hutafanikiwa kwa asilimia 100, kipo kitu ambacho utakijenga kwa watoto wako.

Hivyo usijiambie umechelewa, tumia nafasi uliyonayo kuhakikisha watoto wako wanakuwa chanya na kufanikiwa kwenye maisha yako.

 1. Utatu katika malezi ya mtoto.

Sisi binadamu tumegawanyika kwenye utatu wa mwili, akili na roho. Wazazi wengi wamekuwa wakikazana na maeneo mawili, moja zaidi la akili, na kidogo kwenye mwili lakini kusahau kabisa kwenye roho.

Kwenye akili, hakikisha mtoto anapata elimu bora kabisa kwake, anajifunza mambo chanya na yenye msaada.

Kwenye mwili hakikisha mtoto anapata chakula chenye afya na kufanya mazoezi ya viungo, pia msaidie kujikinga na magonjwa.

Kwenye roho, msaidie mtoto kukua kiimani, Sali naye pamoja, nenda naye nyumba ya ibada na pia msaidie kujua maana ya maisha na kusudi lake hapa duniani.

Mtoto akikua katika utatu huu, lazima atakuwa na mafanikio makubwa.

 1. Muda wa wazazi unahitajika kwa malezi bora ya watoto.

Kwa zama tunazoishi, ambapo asilimia kubwa ya wazazi wote wawili wanafanya kazi, jukumu la malezi ni kama limekodishwa kwa vituo vya kulelea watoto, wasaidizi wa ndani au shule za bweni.

Kwa aina hii ya maisha tunawanyima watoto wetu fursa ya kuwa na misingi mizuri ya maisha, kwa sababu yeyote tunayemkodishia kazi hiyo, kwa sababu sisi tupo bize, hana muda wa kutosha kwa watoto wetu.

Ni vyema pamoja na ubize wa zama hizi, kila mzazi atenge na kulinda muda wa malezi kwa watoto. Hili ni jukumu ambalo linapaswa kupewa kipaumbele cha kwanza.

 1. Watoto wanaolelewa na wazazi wawili wana nafasi ya kufanikiwa kuliko wanaolelewa na mzazi mmoja.

Tafiti nyingi zimekuwa zinaonesha kwamba watoto wanaolelewa na mzazi mmoja, hasa mama, wamekuwa wakidhurika zaidi kuliko wanaolelewa na wazazi wawili. Watoto wengi wa mtaani utakuta wamelelewa na mzazi mmoja au mzazi alipewa ujauzito na kutekelezwa. Watoto wengi wanaoishia kwenye ulevi, matumizi ya madawa, wizi na hata ukahaba, wanatoka kwenye familia ya kulelewa na mzazi mmoja.

Ni muhimu sana kwa wazazi kuhakikisha wanashirikiana kuwalea watoto wao ili kupata msingi mzuri wa maisha ya mafanikio.

 1. Mtazamo wa mtoto unajengwa na mambo makuu matatu;

Moja; imani, watoto wengi wanaanza kujenga imani kwa wazazi wao. Lazima uwawezeshe kujenga imani nzuri ya kiroho na kwao binafsi.

Mbili; matumaini, chochote ambacho tunafanya kwenye maisha, ni kwa matumaini, mjengee mtoto uwezo wa kutumaini kwenye lolote wanalofanya.

Tatu; upendo, upendo ndiyo unatawala kila kitu, mtoto anapokuwa na upendo, maisha yanakuwa bora sana kwake.

 1. Malezi ya watoto ni kazi, tena ambayo ni muhimu mno.

Wapo wazazi ambao wanafanya kazi na kukosa muda wa kulea watoto wao, ambapo ukipiga mahesabu vizuri, unakuta wanapoteza fedha nyingi kuliko wanazopata kupitia kazi wanazofanya. Lakini wazazi wa aina hii, wanaona kazi ni muhimu kwa sababu wakiacha na kuelea watoto, watadharaulika.

Zoezi la kulea watoto linadharaulika kwenye jamii na kuonekana ni la watu ambao hawana elimu au hawawezi kupata kazi. Na hii imechangia kuharibika sana kwa maadili ya watoto. Wewe kama mzazi, kama unaona ni muhimu kwa watoto wako kupata malezi bora kutoka kwako, na hivyo kupunguza kazi unazofanya au  hata kuacha kama yupo mwingine anayefanya kazi, usiogope na kuona utachukuliwa ni mtu wa chini. Zoezi la kulea watoto ni kubwa na muhimu. Uwekezaji unaofanya sasa, utakulipa sana mbeleni kwa kuwa na familia bora ya watoto wenye mafanikio.

Kama ambavyo tumejifunza kwenye uchambuzi huu mfupi, zoezi la malezi kwa watoto siyo rahisi, lakini linawezekana hasa pale wazazi wanapojitoa na kushirikiana. Kama wewe ni mazazi au unapanga kuwa na watoto baadaye, soma kitabu hichi. Kupata kitabu hichi bure kabisa, jiunge na kundi la AMKA MTANZANIA telegram. Bonyeza maandishi haya kujiunga.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz

 

UCHAMBUZI WA KITABU; Uongozi Wetu Na Hatima Ya Tanzania.

Nchi ya Tanzania imepitia vipindi tofauti mpaka kufika hapa tulipo sasa. Tukianza na harakati za uhuru mpaka kuupata uhuru, muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kufutwa kwa mfumo wa vyama vingi na hatimaye kuja kurejeshwa tena. Yote haya ni matukio ambayo yameleta mabadiliko makubwa kwenye nchi yetu.

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, baba wa taifa la Tanzania ni mtu mwenye mchango mkubwa sana kwa hapa nchi yetu ilipofika. Alikuwa raisi wa kwanza wa Tanzania kuanzia uhuru na muungano mpaka mwaka 1985 ambapo aliamua kung’atuka kwenye uongozi.

Baada ya kung’atuka kwake, raisi aliyefuata alikuwa ni Ali Hassan Mwinyi, ambaye kwa wakati wake, yapo mambo yaliyofanyika, ambayo hayakumfurahisha Nyerere. Nyerere kwa uchungu aliokuwa nao kwa nchi hii, aliona kukaa kimya ni hatari kubwa, ndipo alipoandika kitabu hichi cha Uongozi Wetu Na Hatima Ya Tanzania.

uongozi wetu

Kitabu hichi ni kama maonyo, ushauri na wosia wa Nyerere kwa viongozi wa Tanzania na maendeleo ya Tanzania kwa ujumla.

Karibu kwenye uchambuzi wa kitabu hichi, nikushirikishe yale niliyojifunza, ambayo yanatuwezesha kuijua vizuri nchi yetu na kuweza kupiga hatua.

 1. Changamoto ya ukomo wa uongozi.

Wakati Mwalimu anaandika kitabu hichi mwaka 1994, ulikuwa umebaki mwaka mmoja kufika ukomo wa raisi  Mwinyi. Kulikuwa kumeanza kuwa na minong’ono kwamba raisi Mwinyi aendelee kuwa raisi. Hili lilimkera mwalimu na kuona iwapo halitasemwa waziwazi na kuandikwa kwenye katiba kwamba ukomo wa raisi ni vipindi viwili, basi litakuja kuleta shida mbeleni.

Tumekuwa tunaendelea kuona hili, tangu uongozi wa Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli, kila uongozi, kumekuwa na minong’ono ya raisi kuongezewa muda.

Mwalimu anatukumbusha kwamba lazima pawepo na ukomo wa uongozi, kwa sababu ndivyo katiba yetu inavyotaka. Kwenda kinyume na hilo, ni kutengeneza matatizo baadaye.

 1. Tishio la kuvunjika kwa muungano wa Tanzania.

Katika kitabu hichi, Mwalimu amejadili matukio mawili makubwa ambayo yalikuwa yanatishia muungano wa Tanzania.

Tukio la kwanza ni Zanzibar kujiunga na umoja wa nchi za kiisilamu. Hili lilikuwa kinyume na katiba na kupelekea watu kuona Zanzibar ina uhuru mkubwa ndani ya muungano.

Tukio la pili lilikuwa vuguvugu lililoanzishwa na kundi la wabunge 55 maarufu kama G55 kutaka muundo wa muungano utengenezwe upya na kuwe na muungano wa shirikisho la serikali tatu. Kitu ambacho Mwalimu alikikemea sana na kusema kuifufua Tanganyika ni kuua Muungano.

 1. Vuguvugu la kubadili muungano lilikuwa ni ajenda ya vingozi.

Katika kitabu hichi, Mwalimu anatuonesha namna gani vuguvugu la kudai serikali ya Tanganyika lilikuwa ajenda ya viongozi na siyo ya wananchi. Anatuonesha kwamba hakukuwa na uhitaji mkubwa wa wananchi kuhusiana na muundo wa muungano. Badala yake ilikuwa ni ajenda ya baadhi ya viongozi ambao walikuwa wanataka madaraka zaidi.

 1. Utaratibu mpya wa kumpata makamu wa raisi.

Wakati wa utawala wa Mwalimu, na hata utawala wa Mwinyi, uongozi wa juu ulikuwa ni raisi wa Muungano, waziri mkuu ambaye pia alikuwa makamu wa kwanza wa raisi na raisi wa Zanzibar ambaye alikuwa makamu wa pili wa raisi wa Muungano.

Nyerere alishauri hili libadilishwe kwa sababu nchi ilikuwa imeingia kwenye mfumo wa vyama vingi. Hivyo iwapo chama kimoja kitaongoza serikali ya muungano na chama kingine serikali ya Zanzibar, ingetokea changamoto ya uongozi.

Hapa ndipo ulipopendekezwa mfumo wa kuwa na mgombea mwenza ambaye anatoka upande wa pili wa muungano, tofauti na ule anaotoka mgombea uraisi.

 1. Wanafalsafa ni viongozi wazuri, ila hawapendi uongozi.

Mwalimu anatuandikia kwamba, changamoto kubwa tunazopata kwenye uongozi, ni kwa sababu tunaowachagua kuwa viongozi ni wanasiasa. Mwalimu akimnukuu Plato anasema kwamba wanafalsafa ni viongozi wazuri, kwa sababu kwanza hawapendi kuongoza, hivyo wakipewa uongozi, watafurahia pale unapofikia ukomo. Tofauti na wanasiasa ambao hawataki uongozi wao ufikie ukomo.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; On Becoming A Leader (Mambo Muhimu Ya Kuzingatia Ili Kuwa Kiongozi Bora Kwa Zama Hizi).

 1. Suluhisho ni kuwabana viongozi na siyo kuvunja muungano.

Mwalimu anatushirikisha mkutano wake na kundi la wabunge ambao walitaka mfumo wa muungano kutengenezwa upya. Walimpa sababu nyingi za kutaka hivyo, na Mwalimu alikubaliana nazo, lakini aliwaambia zote ni matatizo ya uongozi, ambayo yangeweza kutatuliwa kwa wabunge kuwabana viongozi na siyo kukimbilia kubadili muundo wa muungano.

Mwalimu aliamini kwa changamoto zilizokuwepo kwenye muungano wa serikali mbili, kwenda kwenye serikali tatu kungetengeneza changamoto kubwa zaidi na muungano huu usingepona.

 1. Kuongoza ni kuonesha njia.

Jambo moja kubwa lililomkera Mwalimu kwa wakati ule ni uongozi kukosa nafasi ya kuonesha njia na badala yake ukawa unafuata njia. Yaani viongozi hawakuwa watengeneza ajenda ambazo zinaleta mijadala, badala yake mijadala ilikuwa inaanzishwa na wengine na uongozi kulazimika kujitetea au kujinasua.

Mwalimu aliona huu ni udhaifu mkubwa ambao unaipeleka nchi kwenye matatizo makubwa.

 1. Mara ya kwanza Mwalimu Kulizwa na mambo ya siasa.

Vuguvugu la kubadili muundo wa muungano lilijadiliwa ndani ya chama, na chama kikakubali kwamba lipingwe. Mwalimu aliombwa kuwapa semina viongozi wa chama na serikali kuhusu madhara ya kubadili mfumo wa muungano.

Lakini muda mfupi baada ya makubaliano hayo, katika vikao vya chama, Mwalimu alisikitishwa sana pale aliposikia kwamba swala la muundo wa muungano limerudi tena na wakati huo chama ilibidi kifanye maamuzi mengine.

Mwalimu alishindwa kujizuia na kujikuta akilia, kwa sababu hakuelewa iweje jambo ambalo limeshakubaliwa na vikao vya juu vya chama linarudishwa tena kwa maamuzi tofauti.

 1. Kwa nini serikali tatu pekee?

Baada ya swala la kubadili mfumo wa muungano kuonekana kuendelea zaidi ya ilivyotegemewa, Mwalimu alihoji kwa nini wanaotaka muungano ubadilishwe wanataja serikali tatu tu?

Alieleza ipo miundo mbalimbali ya muungano, serikali moja, mbili na hata serikali tatu. Je kwa nini wananchi wasipewe nafasi ya kujua aina hizo mbalimbali za muungano, faida na hasara zake kisha wachague ipi inafaa?

Hapa ndipo Mwalimu alishawishika zaidi kwamba ajenda ya muundo wa muungano ilikuwa ya watu wachache wenye maslahi yao binafsi.

 1. Dhana ya uwajibikaji.

Moja ya mambo yaliyomkera zaidi Mwalimu ni kukosekana kwa dhana ya uwajibikaji. Kwa mfano kwenye swala la muungano, waziri mkuu alimshauri raisi akatae mapendekezo ya kujadili muungano, na raisi akafanya hivyo. Lakini miezi miwili baadaye, waziri mkuu yule yule alimshauri tena raisi kukubali mapendekezo ya kujadili muungano.

Mwalimu anasema hapa kunakosekana uwajibikaji, ni labda waziri mkuu angepaswa kujiuzulu yeye mwenyewe, au raisi alipaswa kumfukuza waziri mkuu. Lakini hayo yote hayakufanyika, na iliashiria udhaifu mkubwa kwenye uongozi.

SOMA; Hii Ndiyo Changamoto Kubwa Ya Kuwa Kiongozi, Ambayo Lazima Uijue Na Ujiandae Nayo.

 1. Raisi kukokotwa.

Moja ya vitu ambavyo Mwalimu aliviona ni hatari kwenye uongozi wa nchi, ni hali ya raisi kukokotwa na viongozi aliowachagua yeye mwenyewe. Ilionekana kama raisi hana kauli kwenye swala la muungano, na hivyo alikuwa akifanya kila anachoshauriwa kufanya.

Hii ilitokana na viongozi wale kujua udhaifu wa raisi na kuutumia vizuri. Walijua makosa aliyoyafanya kwa kufumbia macho swala la Zanziba kujiunga na umoja wa nchi za kiislamu. Hivyo walitumia mwanya huo kulazimisha hoja ya muungano.

 1. Raisi anawajibika kwa maamuzi yoyote anayofanya, hata kama ameshauriwa.

Mwalimu anatukumbusha kwamba kwa uongozi wa nchi yetu, raisi ni kiongozi ambaye ana mamlaka ya juu kabisa ya utendaji. Raisi anaweza kushauriwa, lakini halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote. Anapaswa kufanya maamuzi sahihi na maamuzi yoyote anayofanya yeye ndiyo anawajibika nayo.

Alieleza kwamba hata kama raisi ameshauriwa na mtu, na akafanyia kazi ushauri huo na ukawa ni makosa, anayelaumiwa ni raisi na siyo aliyemshauri. Hivyo raisi anapaswa kufikiri kila jambo kwa kina, hata kama ameshauriwa na mtu gani.

 1. Kumtikisa raisi ni kuitikisa nchi.

Mwalimu aliona kilichokuwa kinaendelea kwa wakati ule ni kama raisi alikuwa anataka kutikiswa na watu, na hilo lingekuwa hatari sana kwa nchi.

Ilionekana kama viongozi waliokuwa chini yake, hasa waziri mkuu na mawaziri wengine, walikataa kuwajibika kwa makosa yao. Na raisi aliogopa kuwafukuza kazi.

Mwalimu alisema kumbadili waziri hata waziri mkuu siyo jambo la ajabu, anaweza kujiuzulu au kufukuzwa na nchi isitikisike. Lakini huwezi kumtikisa raisi wa nchi bila kuitikisa nchi yenyewe.

 1. Raisi Mwinyi kama kiongozi dhaifu.

Mwalimu alisema kwamba, raisi mwingi alikuwa mtu mwema na mpole, lakini akasema wazi kwamba alikuwa kiongozi dhaifu. Alionya kwamba upole na udhaifu wake ulikuwa unatumiwa na watu ambao si wema wala wapole kuhatarisha umoja na amani ya nchi yetu.

Aliona mipango ya watu hawa kutengeneza uongozi utakaofuata baada yake, na hapo alitaka utengenezwe mchakato mzuri la sivyo kuna watu watajijengea njia ya uongozi kwa hila.

 1. Mchakato mpya wa kumpata mgombea uraisi ndani ya chama.

Wakati wa chama kimoja, kamati kuu ya chama cha mapinduzi ilipendekeza jina moja la nani atagomea uraisi na hilo kupitishwa na halmashauri kuu na mkutano mkuu.

Mwalimu alitilia shaka mchakato huo wakati wa mfumo wa vyama vingi. Hivyo alipendekeza mchakato wa kura za maoni katika kupata mgombea wa chama kwa ngazi ya uraisi.

SOMA; UCHAMBUZI WA KITABU; LEADING QUIETLY (Jinsi Watu Wanavyofanya Makubwa Bila Ya Kuwa Na Majina Makubwa).

 1. Muungano wa Tanzania ni wa kipekee duniani.

Mwalimu aliandika kwamba muungano wa Tanzania ni wa kipekee kabisa duniani. Alieleza kwamba huu ulikuwa muungano wa nchi mbili huru, kwa ridhaa yao wenyewe tofauti na ilivyokuwa awali kwamba muungano ulilazimishwa na mipaka ya wakoloni.

Mwalimu aliwahoji wale waliokuwa wanahoji uhalali wa muungano, kwa nini hawahoji uhalali wa mipaka ya nchi mbalimbali iliyotengenezwa na wakoloni?

 1. Lawama ni kwa Chama Cha Mapinduzi.

Mwalimu aliamini kwamba, chama imara kinazalisha serikali imara, hivyo iwapo serikali itashindwa kusimama vizuri, lawama zote ni kwa chama cha mapinduzi. Alionesha namna ambavyo chama kimekosa uongozi mzuri wa kuweza kuisimamia serikali katika sera za chama.

Kwa mfano mchakato wa kubadili muungano, ulikuwa kinyume na sera za chama, kitendo cha jambo hilo kuruhusiwa, ilikuwa udhaifu kwa chama.

 1. Uhitaji wa chama cha upinzani imara.

Mwalimu aliamini kwamba, bila ya upinzani imara, chama cha mapinduzi kitaendelea kuwa kibovu. Alieleza chama kinahitaji upinzani ambao utawaamsha viongozi na kusimamia misingi ya chama.

Yeye mwenyewe pamoja na kuwa mwasisi wa chama, alisema chama siyo baba wala mama yake, iwapo kitakuja chama kingine chenye misingi mizuri na uongozi imara, angeondoka ccm na kujiunga nacho.

 1. Woga unajenga udikteta.

Mwalimu alionesha namna ambavyo watu wanashindwa kusimamia viongozi kwa kuwa na woga. Mwalimu alisema woga siyo heshima, bali woga unazaa udikteta.

Pale watu wanapoanza kumwogopa kiongozi badala ya kumheshimu, hapo wanazalisha dikteta ambaye atawatawala atakavyo na asihojiwe kwa namna yoyote ile.

 1. Uhuru una gharama zake.

Mwalimu aliandika kwamba, uhuru hauji wala haudumishwi ila kwa kuwa tayari kulipa gharama zake. Vitu vyote vyenye thamani kubwa, gharama yake ni kubwa. Lazima watu wawe tayari kuingia gharama katika kutengeneza na kulinda uhuru wao kama wananchi wanaowasimamia viongozi waliowachagua.

Kitabu hichi cha Mwalimu Nyerere, kinatupa taswira ya changamoto kubwa ya uongozi iliyokuwepo wakati anaandika kitabu hichi. Ni changamoto ambayo imezalisha matatizo mengi kwa nchi yetu ambayo bado inaendelea kuwepo katika ngazi mbalimbali za uongozi wa vyama na serikali.

Kupitia kitabu hichi cha Mwalimu, tunaona hatua muhimu za kuchukua kama viongozi, wananchi na hata wanachama wa vyama mbalimbali katika kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama na kuwa na maendeleo. Ni kitabu muhimu kwa kila Mtanzania kusoma ili kuelewa jitihada za kuitengeneza Tanzania bora zilipotokea.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza kwenye uchambuzi wa kitabu hiki ili uweze kuona matokeo bora kwenye maisha yako.

Kupata vitabu vya Kiswahili vya kujisomea ili kuweza kufanikiwa kwenye kazi, biashara na maisha kwa ujumla, tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

www.kisimachamaarifa.co.tz

fb instagram

Hii Ndiyo Nyumba Adimu Sana Kupatikana Katika Zama Hizi Za Taarifa.

Habari mpendwa Rafiki na Msomaji wa mtandao wa AMKA MTANZANIA? Natumaini hujambo na unaendelea vyema katika shughuli zako za kila siku za kukupatia kipato na kugusa maisha ya watu wengine, yaani kuishi maisha ya maana hapa duniani.  Karibu mpendwa rafiki katika makala yetu ya leo tuweze kujifunza kwa pamoja. Natumaini rafiki yangu unajua kuwa kwa sasa tunaishi katika karni ya ishirini na moja (21) na tupo katika zama za taarifa ili ufanikiwe kwa sasa unahitaji taarifa sahihi na kwa wakati sahihi.  Na zama hizi za taarifa zinahitaji kila mtu awe na maarifa sahihi ili yaweze kumsaidia kuishi maisha ambayo ni sahihi na yenye maana kwa ujumla.

Mpendwa rafiki na msomaji wa AMKA MTANZANIA, karibu katika makala yetu ya leo ambapo tutajifunza falsafa moja kutoka kwa mwanafalsafa mkubwa aliyeishi na kuzaliwa kabla ya Yesu kuzaliwa na siyo mwingine bali ni mwanafalsafa Plato. Mwanafalsafa Plato aliwahi kusema, ‘’ a house that has a library in, it has a soul’’ akiwa na maana ya kwamba nyumba ambayo ina maktaba ndani ni nyumba ambayo ina roho. Kila mtu anaishi katika nyumba iwe ni nyumba yako uliojenga au uliopanga lakini unaishi katika nyumba. Je falsafa hii inagusa namna gani?

SOMA; Sehemu Kumi (10) Unazoweza Kupata Muda Wa Kujiongezea Maarifa Kupitia Kusoma Vitabu.

Ukweli ni kwamba nyumba nyingi wanazoishi watu hazina maktaba ndani. Nyumba nyingi ni mabingwa wa kuwa na makochi makubwa, flat screen tv nk. Jaribu kupita nyumba kumi katika jamii unayoishi halafu angalia ni nyumba gani wana maktaba au wana vitabu ndani. Wengi wanapenda kununua vitu kama cd za nyimbo, tamthilia mbalimbali na kukaa nazo kuliko kununua vitabu. Nyumba nyingi ni maskini wa vitabu na nyumba nyingi hazina roho na roho ya nyumba ni vitabu. Katika vitabu tunapata maarifa ambayo yanatusaidia kuishi maisha sahihi.

Maisha ya wanafalsafa wengi ni maisha mazuri sana yenye furaha, amani na mafanikio na kama ukifuatilia maisha ya mwanafalsafa hakika utaujua ukweli nayo kweli itakuweka huru. Yatupasa tuanze kuamka katika majumba yetu badala ya mgeni kuja kwako na kumfungulia tv aangalie mpe kitabu asome aonje roho ya nyumba yako. Akisoma hata ukurasa mmoja atakua ameongeza thamani katika maisha yake. Anza kununua vitabu na kuweka maktaba yako ndogo nyumbani. Katika nyumba yako hakikisha unaishi weka sehemu ya maktaba ambayo ndio roho ya nyumba yako.

Haitoshi kuwa na maktaba tu bali uhai wa maktaba ni wasomaji wa vitabu. Vitabu vinunuliwe na visomwe. Tukiwa tunajenga utamaduni wa kusoma vitabu kwa kila familia tutajenga jamii bora sana na tutafanya dunia kuwa sehemu salama ya kuuishi kwa kila mmoja wetu. Tuanze kwa kila familia kuwa na maktaba za vitabu kwetu. Tuache mambo ambayo hayana faida kubwa katika maisha yetu bali tujenge kizazi imara na jamii imara. Kila mtoto alelewe katika utamaduni wa kusoma vitabu kwani ndio njia sahihi ya kumfundisha mtoto kuvua samaki na siyo kumpa samaki.  Kama unaona ni fahari kumwachia mtoto aangalie sana tv bila kusoma vitabu ujue unamharibu mwenyewe mtoto wako.

SOMA; KITABU CHA APRIL; THE SEVEN HABITS OF HIGHLY EFFECTIVE PEOPLE (Tabia Saba Za Watu Wenye Ufanisi Wa Hali Ya Juu).

Mpendwa rafiki, mwanafalsafa na mwandishi  Jim rohn aliyezaliwa karni ya ishirini (20) na kufariki dunia karni ya ishirini NA moja ( Septemba 17,1930- Desemba 5, 2009) naye aliwahi kusema, ‘’ successful people have  big libraries. The rest have big flat screen Tvs in their home’’ akiwa na maana ya kwamba watu waliofanikiwa wamekuwa na maktaba katika nyumba zao na wengine waliobakia wamekuwa na tv kubwa za kisasa.  Hivyo basi, unaona mwanafalsafa huyu anavyotuambia ukweli kama alivyotuambia mwanafalsafa Plato. Plato yeye aliishi na kuzaliwa kabla hata ya Yesu lakini leo maneno yake yanadhihirika na mwanafalsafa aliyefariki katika karni hii 21 naye anatuambia ukweli huo huo.

Siku hizi katika nyumba nyingi fasheni ni kuweka flat screen ili naye aende na wakati kama wenzake wanavyoenda. Lakini ukiangalia katika upande wa roho ya nyumba hakuna kitu. Ukiwa na  maktaba ndani ndio unaonesha uhai wa nyumba yako kuliko kuwa na tv kubwa nyumbani. Tunatakiwa kuishi maisha ya kifalsafa yaani falsafa ni msingi wa maisha ya binadamu ambayo unaelezea ukweli kupitia uhalisia wa dunia. Jinsi unavyofikiria na unavyoishi unatumia falsafa bila ya wewe mwenyewe kujua.
Kila nyumba inatakiwa ianze leo kuwa na maktaba na kuanza kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu kila siku na kuachana na kutumia muda mwingi katika kuangalia luninga. Kuangalia luninga sana na kwa muda mrefu ni faida hasi kiafya lakini ukisoma vitabu sana ni faida chanya kiafya.  Kuwa balozi wa kuhamasisha jambo hili sehemu yoyote uliyopo. Tuna kazi kubwa kwa kila mmoja wetu kusaidiana ili kufuta ujinga. Taifa haliwezi kukua kama tukikaa na kushinda katika makochi na kuangalia tv taifa litakuwa kama watu wakifanya kazi kwa juhudi na maarifa.

SOMA; Hivi Ndivyo Tabia Ya Kupenda Kujisomea Ilivyoboresha Maisha Yangu. Inawezekana Hata Kwako Pia.

Sasa katika kufanya kazi kwa juhudi haitoshi bila kuwa na maarifa ya kutosha. Maarifa tunayapata katika vitabu vyetu vinavyopatikana katika maktaba zetu. Habari njema ni kwamba katika zama za taarifa unaweza kuwa na maktaba yako ndani ya simu yako imejaa vitabu, kompyuta, na nk. Unatakiwa kutembea na maktaba sehemu yoyote unayokwenda kuanzia leo.

Hatua ya kuchukua; anza leo kutembea na kitabu ukipata muda sehemu yoyote ile chukua kitabu soma. Katika simu yako kama umejaza vitabu ambavyo havina faida chanya futa weka vitabu, kama kwenye kompyuta yako umejaza nyimbo, movie za aina mbalimbali na sirizi (mpangilio wa matukio) mbalimbali futa na weka vitabu. Kama familia yako haina kitabu anza leo kutenga eneo la maktaba na muanze desturi ya kusoma kitabu. Karibu pia katika klabu yetu ya kusoma vitabu viwili kwa wiki. Katika kundi hili tunapokea watu makini ambao hawana sababu yaani excuses. Kujiunga na kikundi hiki tuma ujumbe kwa njia ya telegram kwenda namba +255717101505 ili uweze kujifunza kwa hamasa na kwa nidhamu bila kuahirisha.

Makala hii imeandikwa na Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali, unaweza kuwasiliana naye kupitia namba 0717101505/0767101504 au kwa barua pepe deokessy.dk@gmail.com, kessydeo@mtaalamu.net  au unaweza kutembelea tovuti yake, www.mtaalamu.net/kessydeo ,www.actualizeyourdream.blogspot.com


Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Kinachoitwa LETTERS From A SELF-MADE MERCHANT To His SON.

Wiki hii tunajifunza kwenye kitabu kinachoitwa LETTERS from a SELF-MADE MERCHANT to his SON. Kitabu hiki kimeandikwa na George Horace. Kitabu hiki kinahusu barua za Mfanyabiashara ambazo alikua akiziandika kwenda kwa mwanae. Tajiri huyu alikua akimwandikia mwanae toka akiwa chuoni hadi alipokua anafanya kazi na hata alipokua akipitia mambo kadha wa kadha. Barua hizo zilikua zina mafunzo mengi sana na zimegusa maeneo mengi sana ya maisha.

BARUA ZA MFANYABIASHARA TAJIRI KWA KIJANA WAKE.

 
Karibu sana tujifunze machache katika barua hizo.
1. Njia pekee ya uhakika ya mtu kupata utajiri wa haraka, ni kuupewa au utajiri wa kurithi toka kwa wazazi au ndugu. Mbali na hapo hakuna njia nyingine ya halali ya kupata utajiri wa haraka. Lazima ujiandae kufanya kazi kwa bidii, na ukubali kuanzia chini au pale ulipo. Matajiri kama kina Billgate, Warren Buffet, Mengi, Bharesa na wengine, imewachukua miaka zaidi ya 20 kufikia hapo walipo toka walipoanza kuwaza kwa habari ya kua matajiri. Utakavyoanza mapema kuweka mipango na kuitekeleza, usipofanya hivyo mwenzako anafanya hivyo na baada ya muda kutakua na tofauti kubwa na mwishowe utaanza kumuonea wivu.
2. Kuna sehemu mbili ya elimu ya chuo mtu anapata. Sehemu ya kwanza ni ile unayopata darasani kutoka kwa maprofesa, na nyingine ni ile unayopata kutoka kwa watu wanaokuzunguka, ambayo ndiyo ya muhimu zaidi. For the first can only make you a scholar, while the second can make you a man.
3. Ni rahisi kuonekana mwenye hekima kuliko kuongea hekima. Sikiliza zaidi kuliko kua mwongeaji, waache wengine wawe waongeaji zaidi, wewe sikiliza zaidi. Unapomuonyesha mtu kua unamsikiliza kwa makini, ni rahisi kukwambia kila kitu anachokijua.
4. Pesa inaongea ila tu kama mmiliki wake atakua na ulimi mlegevu wa kuongea ongea na mara zote matokeo yake hua sio mazuri. Umasikini pia unaongea japo hakuna mtu anayetaka kuusikia unasema nini.
5. Njia rahisi ya kutengeneza maadui hapa duniani ni kuajiri marafiki. Aidha kwenye biashara au hata kwenye uongozi wa kisiasa. Usiingize urafiki kwenye biashara, bishara ibaki biashara na urafiki ubakie urafiki. Usimwajiri mtu kwa kumuonea haya kamba ni rafiki yako, hii itakua ni kujitengenezea uadui. Maana kwa kawaida marafiki wanatamani wawe kwenye level sawa, na pale unapoanza kupiga hatua mbele, urafiki wenu unaanza kushika dosari. Na kwa vile anakujua ataleta kujuana kwingi kwenye kazi, na ukitaka awajibike kazini kama wengine ataanza kukuona mbaya.
SOMA; Kama Utashindwa Kufanya Chochote Utakachojifunza, Basi Fanya Hiki Kimoja Tu, Na Maisha Yako Yatagusa Wengine.
6. Usioe binti maskini aliyekuzwa kama tajiri. Mabinti kama hawa ni wale wanaotaka maisha ya matanuzi bila kujua zinatafutwa namna gani. Mfano binti anajua kipato chako, anaanza kukwambia hicho ni kidogo hakinitoshi, akipata mwenye kipato cha juu, ndio hutamuona tena. Wanataka kuishi maisha Fulani hivi, ili waonekane, fedha za kununulia cheni za dhahabu, kununulia mapambo ya dhamani, aende saluni za ghali ili tu awazidi wenziwe. Kwa ufupi ni kwamba hawana nidhamu ya matumizi ya fedha
7. Chuo hakitengenezi wajinga bali kinawaendeleza, pia chuo hakitengezi watu makini, bali kinawaendeleza tu. Mjinga atabaki kua mjinga hata akienda shule, japo akitoka atakua aina nyingine ya mjinga. Shule zinaendeleza kile ulichonacho. Lakini kukosekana kwa elimu ya chuo hakupunguzi wajinga, ila kuwepo kwa elimu kwa elimu ya chuo kunainua pia watu makini.
8. Wauzaji wazuri ni wale wenye uwezo wa kutengeneza hamu ya kula kwa wanunuzi hata kama hawana njaa. Umeshawahi kujiuliza kwa nini hua unanunua vitu hata kama ulikua huna ratiba ya kununua? Wafanya biashara wazuri wanajua jinsi ya kutengeneza hamu ya kununua hata kama ulikua huna mpango wa kununua.
9. Njia mpya ni nzuri kuliko za zamani. Katika nyanja yoyote teknolojia mpya zinarahisisha utendaji wa kazi na ufanisi, nakupelekea matokeo makubwa na ya uhakika. Mfano kwenye kilimo mkulima anayetumia jembe la mkono hawezi kupata sawa na anayetumia zana za kisasa kama trekta, na vifaa vya umwagiliaji. Ukiendelea kufanya kitu kwa njia ile ile miaka nenda rudi, utapata matokeo yaleyale. Wanaotumia njia za zamani mara zote huwatumikia wanaotumia njia mpya.
10. Mwonekano wa nje hudanganya, Shati chafu laweza kuficha moyo safi, lakini ni nadra sana kufunika ngozi safi. Ukiwa umevaa nguo zenye dosari, watu wengi wanakwenda kwenye hitimisho, kwamba hata akili yako haiwezi kua na mawazo mazuri. Watu wanaangalia smartness ya akili ya mtu kwa kuangalia amevaaje. Wakati mwingine sio kweli, mavazi ya nje hayana uhusiano na akili. Mfano tajiri wa Facebook Mr. Mark mara nyingi anavaa T-shirt, kwa mtazamo wa jamii ya sasa tungetegemea awe anapiga suti kali kila siku maana hela anayo.
11. Ulimi unaweza kusema uongo lakini macho yatasema ukweli. Mara nyingi mtu anayesema uongo ukimwangalia machoni utagundua, maana anakosa ujasiri wa kukutazama usoni.
12. Ajiri kwa taratibu na fukuza haraka (Be slow to hire and quick to fire. Katika kuajiri usifanye haraka, tumia muda kuchunguza sifa za mtu unayemtaka. Unapogundua kwamba umeajiri mtu ambaye sio sahihi fukuza mara moja. Kama sheria ya kazi inavyotaka, mlipe mshahara wake wa mwezi mmoja zaidi na haki zake nyingine kulingana na matakwa ya sheria, halafu aondoke. There are no exceptions to this rule, because there are no exceptions to human nature.
SOMA; Hiki Ndio Kinachokuzuia Wewe Kupata Kile Unachotaka Kwenye Maisha Yako.
13. Katika shughuli zako zote, kumbuka LEO ndio fursa yako, na kesho ni fursa ya mwenzako. Ukiwa na mtazamo huo utatumia vizuri muda ulionao kwa wakati huo Maana ni rahisi kuahirisha shughuli kwamba utafanya kesho. Weka juhudi katika kufanikisha shughuli zako leo bila kusubiri kesho, maana kesho sio fursa yako tena bali ni ya mwingine.
14. Mtu anakua mzuri au bora kutokana na anavyojiboresha, lakini hakuna mtu anakua bora kwa sababu babu yake alikua bora. Kwa vile baba au babu yako alifanikiwa katika maisha haina maana na wewe utafikiwa tu. Lazima uchukue jukumu la kuboresha maisha yako wewe mwenyewe.
15. Ukifanikiwa watu watasema ni bahati au umefanikiwa kama ajali (accident) ila pia ukishindwa watu watatoa unabii kwamba tulijua atashindwa tu, yaani sisi tulimwambia akajifanya mjuaji. Kwa hiyo ufanikiwe au ushindwe lazima watu watazungumza mabaya tu. Hakuna mtu atakayetambua juhudi ambazo unazifanya kufikia mafanikio.
16. Njia nzuri ya kutosheleza ladha ya mandhari ni kupanda mlima. Unapopanda mlima hua kuna njia ndefu na njia za mkato. Njia ndefu huchukua muda kufika kileleni lakini ndio salama. Ila njia ya mkato mara nyingi zinapita sehemu za hatari zenye maporomoko, kuna uwezekano ukaanguka na kufika chini mara moja. Vivyohivyo Njia ya kufika kilele cha mafanikio sio fupi lakini ndio njia salama. Hufiki juu kwa haraka, lakini pia haushuki kwa haraka. Pita njia sahihi achana na njia za mkato.
17. Usiishi leo kwa kipato/mshahara wa kesho, bali ishi leo kwa mshahara/kipato cha jana. Unapokua na matumizi makubwa kuliko kipato chako ina maana unatumia kipato cha kesho, mwishowe unajikuta unalimbikiza madeni kibao, kwa hiyo kipato cha kesho utatumia kulipa madeni ya gharama ulizotumia kuishi leo.
18. Ukikosea kuoa, itakugharimu maisha yako yote. Hili ni kosa ambalo utaishi nalo kwa kipindi chote cha maisha yako.
SOMA; Ukiendelea Na Maisha Haya Watu Watakunyanyasa Sana…
19. Mke ana nguvu kubwa sana ya kumtengeneza mwanaume kuliko hata wazazi. Mwanaume anapokua mdogo wazazi wanakua na nguvu kubwa kwake katika kum-shape, lakini akishakua mtu mzima inakua ngumu sana wazazi kumrekebisha, ila mwanaume huyo akipata mke mwema its easier keep him in order.
20. Unapokua mfanyakazi, fanya kazi vizuri sana, kiasi kwamba bosi wako ashindwe kufanya kazi bila wewe, ila wewe uwe na uwezo wa kufanya kazi hata yeye asipokuwepo. Mfano kama wewe ni meneja msaidizi, fanya kazi vizuri kiasi kwamba meneja wako atashindwa kuongoza idara yenu pasipo wewe, lakini wewe utakua unaweza kuongoza idara hata pasipo yeye. Hii ni kwakufanya kazi zako vizuri, lakini pia zile anazofanya yeye unajifunza na kuzifanya vizuri pia. Tahadhari ni kwamba usifanye kwa kuonesha unataka kushindana naye. Fanya kwa kuonyesha unataka kumsaidia ili asiwe na majukumu mengi.
Asanteni sana
Tukutane wiki ijayo
Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana naye kwa simu 0763 071007 au barua pepe
daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com

Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu The One Thing.

Habari rafiki, ni matumaini yangu waendelea vizuri. Wiki hii tunaendelea na utaratibu wetu wa kushirikishana mambo 20 nilijifunza kwenye kitabu. Leo tunajifunza kutoka kwenye kitabu kinaitwa The ONE THING- the surprisingly truth behind the extraordinary results. Kitabu kimeandikwa na Gary Keller pamaoja na Jay Papasan.

Kwa ufupi kitabu hiki ni kizuri sana. Hupaswi kukosa mambo ya wiki hii. Karibu tujifunze.

1. Muda hausubiri mtu. Muda hauna cha VIP , maskini au tajiri hauna wa kumuogopa wala wa kumuonea huruma. Kwahiyo tunapaswa kuuthamini sana muda maana ni bidhaa hadimu sana na tumepewa bidhaa hii sawa kwa watu wote. Tofauti zetu zinatokana na jinsi tunavyotumia muda tulionao. Muda haukusubiri ufanikiwe kwanza ndio uzeeke, au hausubiri kwanza ustaafu ndo ukaanze biashara. Hata ukilala na usifanye chochote muda unayoyoma. Time waits for no one.

SOMA; Fanya Mambo haya matatu kuwa na maisha bora na yenye furaha.

2. Unapomuoana mtu ana maarifa mengi ujue imemchukua muda kujifunza kufikia hapo. Ukiona mtu amefanya vitu vingi au amefanikisha vitu vingi ujue kwamba alitumia muda fulani kuvifanikisha, na vilevile Ukiona mtu mwenye fedha nyingi ujue imemchukua muda kuzipata. Suala kubwa hapa ni muda. Kila kitu kinahitaji muda, hakuna kitu cha kulala usiku na kuamka asubuhi umekua tajiri hakuna kitu kama hicho. Mafanikio yeyote yanahitaji muda. Unaowaona wamefanikiwa iliwachukua miaka kadhaa kufika hapo walipo. Walikua na upeo wa mbali wa miaka kuanzia 20 mbele.. wakati wengi wetu hata mwakani hatujui tutakua wapi tunaishi maisha ya pata potea, kutafuta na kula kuoa au kuolewa na kujenga kanyumba kamoja na kagari kwisha kazi.. Halafu tunajiona vidume kweli.. na kukaa na kusema usiwaone wale kina Bill gates ni Freemason wale mali zao ni za kishetani… Tuna sahau kwamba wenzetu walikua na Malengo na mipango ya muda mrefu na kila siku walikua hawapotezi muda kuyafanyia kazi malengo yao. It’s just a matter of time

3. Kampuni nyingi zilizofanikiwa zinakua na bidhaa moja au huduma moja ambayo ndiyo inawafanya wajulikane na kuwatengezea fedha nyingi. Issue sio kua na bidhaa nyingi kama utitiri. Chagua kitu kimoja weka nguvu zako zote hapo lazma utaona mafanikio. Sasa kwetu unataka uuze mchele wewe, spear za pikipiki, duka la vyombo, sijui kibanda cha mpesa unataka. Fanya kitu kimoja kwanza kikishafanikiwa anza kingine. Success is sequential, not simultaneous.

4. Hakuna mtu anayefanikiwa peke yake. Kila mtu aliyefanikiwa katika Nyanja yeyote atakwambia kuna mtu aliyemshawishi, alimhamasisha au alimfunza hadi imepelekea kufika hapo alipo. Hata Albert Einstein mwanasayansi maarufu duniani, alikua akipata uongozi na maelekezo kutoka kwa bwana Max Talmud kwa muda wa miaka sita. Na ndio maana utasikia watu wakisema mentor wangu ni fulani, mentor wangu, mentor wangu.. je na wewe unayo mentor? Tafuta kocha na kaa chini ya kocha. Kumbuka No one is self-made. No one succeeds alone. No one.

5. Waliofanikiwa hawafanyi vitu tofauti la hasha wanafanya kwa utofauti. Wana jicho la umuhimu. Wanatulia na kuamua kipi ni cha muhimu katika maisha yao na ndicho wanachokipa nafasi kiendeshe maisha yao. Wanaofanikiwa Wanafanya kwanza vile vitu ambavyo wengine wanapanga kufanya baadaye, na ubaya ni kwamba hiyo baadaye hua haifiki inabaki tu baadaye. Achievers always work from a clear sense of priority.

SOMA; Kijana Punguza Mambo Haya Ili Uweze Kupata Mtaji Wa Kuanza Biashara -1

6. Orodha ya vitu vya kufanya (To do list) usipokua makini inaweza ikakupleka nje ya kuafanikiwa. Kwanza orodha ya mambo ya kufanya ni vitu vile tunavyodhani tunahitajika kufanya. Jambo la kwanza linalotokea kwenye orodha mara nyingi ni lile lililoanza kukujia kichwani. To do list nyingi ni kwa ajili ya kutufanya tuwepo tu(Survival list) , ni orodha ya kukufanya umalize siku yako na kujiona kwamba umefanya kazi..yani umeweza kufanya yote ulopanga kwenye orodha unajihisi umefanikisha mambo sana. Instead of a to-do list, you need a success list – a list that is purposefully created around extra ordinary results. Success list au orodha ya mafanikio ni ile inayojikita kwenye shughuli zenye matokeo makubwa na shughuli zenyewe ni chache tu. The majority of what you want will come from the minority of what you do. Kwisha habari

7. Kuwa bize au kua na mambo mengi ya kufanya hakumaanishi kufanikiwa. Mara nyingi tunapenda watu watuone kwamba tuko bize, tuna mabo mengi ya kufanya. Je umewahi kujiuliza toka uwe bize umepiga hatua gani ya maana kulingana na ubize wako? Don’t focus on being busy; focus on being productive. Allow what matters most to drive your day.

8. Jifunze kusema Hapana. Sio kila kitu unakubali tu, sio kila wakati unaawambiwa fanya hivi au vile na wewe unakubali tu. Mara nyingi vitu vya namna hiyo vinakujia ili kutimiza ndoto au mafanikio ya wengine. Jifunze kusema hapana, mpaka pale umemaliza kufanya jambo la muhumi kwanza. Mara nyingi hasa wafanyakazi walio ajiriwa wanadhani kukubali kila kitu kinachotoka kwa boss ndo unakua mfanyakazi bora au ndo utaambiwa uko flexible. Flexible wapi … wakati unajimaliza mwenyewe. utajikuta ni mtu wa kufanya vitu vya emergency tu… Usikimbilie kupata sifa za muda tu..ukaja kujutia maisha yako. Jifunze kusema hapana hata kwa boss wako. Mwanzoni ataweza asikuelewe lakin ipo siku utakua mfano, kwamba ni mtu unayejua kuweka vipaumbele mtu unayejua kusimimamia jambo lenye kipaumbele bila kujalisha ni dharura gani imetokea.

9. Kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja (Multitasking) ni uongo. Hii imekua dhana kila sehemu, utasikia watu wakijivunia mimi nafanya multitasks. Imefika mahali mpaka kwa waajiri multitasking imekua ni moja ya sifa ya mtu anatakiwa awe nayo ili kuajiriwa. Yaani wakati unaandika ripoti muda huhuo uwe unamhudumia mteja na tena uwe unaongea na simu. Ukifanya hivyo lazima utashindwa kimoja wapo au vyote, au utaishia kuapata matokeo ya kawaida sana. Katika ulimwengu wa leo ambapo unapimwa kwa matokeo (results/impacts) na sio kwa kazi uliyofanya Multitasking inawazika wengi sana. Ili uwe na matokeo makubwa fanya jambo la muhimui kuliko yote weka nguvu na umakini wako hapo. Hakikisha umemaliza alafu nenda kwenye jambo lingine. It’s not that we have too little time to do all the things we need to do, it’s that we feel the need to do too many things in the time we have.

10. Hatupaswi kuogopa mambo makubwa. Kwa kujua au kutokujua wengi wetu tumekua tunaogopa mambo makubwa tukidhani ni mabaya kumbe sio kweli. Mfano mtu anaogopa kuwa na mawazo ya kumiliki ndege, kumiliki makampuni makubwa duniani, akidhani kwamba ni mbaya au atapata madhara mabaya. Utasikia mtu anasema sasa pesa zote hizo nipeleke wapi? Mimi nataka tu za kunitosha sitaki presha mimi. Ukiwa na mawazo hayo ujue wewe ni mbinafsi (selfish) maana unajifikiria wewe tu. Huwazi kupata zaidi ya unachohitaji ili kuwasaidia wengine, mwisho wa upeo wako ni wewe kupata tu. Angalia kina Bill gate fedha walizonazo asilimia kubwa wala hatumii yeye. Anatumia kuwasaidia wengine katika sekta ya afya, kilimo n.k Ana malengo ya kufuta kabisa baadhi magonjwa yaliyoitesa dunia kama polio, malaria, ebola n.k. Ipo miradi mingi sana ya kilimo inayofadhiliwa na Bill Gate, na kiu yake kubwa nikuona wakulima wadogo wakiongeza vipato vyao kaika hali endelevu, mimi mwenyewe nimekua nikisimamia moja ya miradi ya kilimo inayofadhiliwa na Bill Gate. Don’t fear big. Fear mediocrity. Fear waste. Fear the lack of living to your fullest. “People who are crazy enough to think they can change the world are the only ones who do.”

SOMA; Huu Ndio Ukomo Unaojiwekea Wewe Mwenyewe.

11. Usiogope kushindwa maana ni sehemu ya safari yako ya kufanikiwa . Tazama kushindwa kwako kama shule ya kujifunzia alafu songa mbele. Mtu mmoja aliwahi sema hivi “ if you want to double your success, then you have to double your failures”. Akimaanisha kwamba kama unataka kupata mafanikio mara dufu, uwe tayari kushindwa maradufu. Maana katika kushindwa ndio unajua ipi sio njia sahihi na kuanza kutafuta njia sahihi.

12. Ubora wa maisha yako utatokana na maswali unayojiuliza. Unaweza jiuliza kwanini tujikite kwenye maswali wakati kwa kawaida hua tunahangaikia kupata majibu. Ni kweli Wengi tunawaza kupata majibu. Na mimi nakuuliza majibu ya kitu gani? Kama huna mawasli? Ukweli ni kwamba ubora wa majibu unatokana na ubora wa maswali. Hata waliobadilisha maisha yao, au waliobadilisha ulimwengu walianza kwanza kwa kujiuliza maswali makubwa na wakaanza kuyatafutia majibu. Je hapo ulipo ndipo ulipaswa uwepo? Maisha unayoishi ni ya kwako? Je kusudi la wewe kuwepo hapa duniani ni nini? Je unafikiri kama pangekua hakuna kikwazo chochote, na una kila kitu ili kufanya chochote au kupata chochote ungefanya nini? Au Ungetamani kua na maisha gani? Anza kujiuliza maswali hayo na mengine. Ukiona umekerwa ujue somo limeingia na uwezo wa kupata majibu unao. Fanyia kazi uone kama maisha yako yatabaki kama ulivyo. Great questions are the path to great answers.

13. Maisha ndio mwajiri wako mkuu, utakachopatana nae ndicho atakachokupa.. Unapopatana mshahara na mwajiri wako ndicho atakachokupa. Sasa cha ajabu umepatana mshahara na mwajiri baada ya muda unalalama mshahara mdogo. Kwani hukulijua hilo wakati wa mapatano? Bahati nzuri nimewafanyia watu wengi mahojiano ya kazi (job interview), na mara nyingi swali la mshahara linaulizwa mwishoni, na lengo lake kubwa ni kutaka kujua huyu mtu anajitathimini vipi. Yeye mwenyewe anajithaminisha je? Sasa wengi wakiulizwa swali la mshahara anajibu kwamba nitakua tayari au nitaridhika kwa mtakachonipa. Au anataja kiwango cha chini sana. Mimi mwenyewe niliwahi kukosa kazi kwa kutaja mshahara mdogo. Nikidhani ndo nitaonekana ninafaa au nitakua nimeangukia kweny bajeti yao. Duuh kwa masikitiko ndo nikawa nimejimaliza mwenyewe. Sasa wanachojiuliza waajiri ni kwamba kama mtu huyu haoni thamani yake sisi je tutawezaje? Sasa turudi kwenye pointi yetu ya msingi, Maisha ndio mwajiri wako, utakachopatana nae ndicho atakachokupa. Usiyaambie maisha nitakubaliana na chochote utakachonipa. Tambua thamani yako patana na mwajiri wako (maisha) ubora wa vitu unavyotaka.

14. Maisha yenye kusudi (Life with purpose) ndio maisha yenye furaha. Kama hujui kusudi lako hata ufanikiwe vipi huwezi furahia. Live with purpose and you know where you want to go.

15. Kuishi Maisha yenye vipaumbele (Live by priority). Tunaweza kuwa na kusudi la maisha, lakini tukikosa vipaumbele itakua ni pata potea. Kipaumbele au priority ina tafsiri kadhaa kama “kitu cha muhimu zaidi”, “kitu cha msingi”, “kitu cha kwanza”, “kitu cha juu” kitu kikuu” n.k Unaweza kua na tafsiri nyingi lakin zote zitalenga kaitka kitu kimoja kinachopaswa kutangulia ili kurahisisha vingine au hata kufanya hivyo vingne visiwe vya muhimu kivile. Kua na ndoto au malengo makubwa mengi sio kwamba ndo kufanikiwa, la hasha. Wengine wanajiuliza sasa mbona nina vipaumbele vingi, lakin unasahau kwamba katika vipaumbele ulivyonavyo ikichimba ndani zaidi una kimoja ni cha muhimu zaidi. Anza nacho hicho. The purpose without priority is powerless

SOMA; Kama Hutaki Kuwa Na Maadui Fanya Kitu Hiki Kimoja.

16. Kusudi la furaha. Ukweli ni kwamba kila tunachofanya kwenye maisha ni ili tupate furaha. Furaha ndio bidhaa ambayo imekua ukitafutwa na watu wengi sana, lakin ndio bidhaa ambayo wachache sana wanafanikiwa. Tatizo ni kwamba tunafikri furaha ni jambo la kufikia, yaani pale tunapopata kitu fulani,( kama mke, mume, mototo, nyumba, gari au kufaulu) ndo tunatakiwa kufurahi. Ndio maana ukipata kitu kile unafurahia kwa muda kidogo tu halafu unaanza kutafuta kingine ili upate furaha tena. Unapaswa kufurahia kila hatua unayopita kuelekea mafaniko. Kuna mtu aliwahi kusema hakuna njia ya mafanikio, bali mafanikio ndio njia. Kama mafanikio ni njia, basi tunapaswa kuwa na furaha kwenye njia hiyo. Happiness happens on the way to fulfillment.

17. Weka malengo yako kwenye kataratasi na uyaweke karibu na wewe. Watu wengi hatuna utaratibu wakuandika malengo yetu, yaani malengo yanakua kichwani tu, tena malengo mengi yanawekwa kipindi cha mwaka mpya, mwezi January ukiisha ulishasahau ulipanga nini. Swali la kujiuliza ni vitu ngani viko karibu na wewe zaidi? Wengi wetu simu ndo vitu vya karibu, simu ndo kitu cha mwisho kua nacho kabla ya kulala na cha kwanza kukishika kabla ya kuanza siku. Malengo yako ndo yanapaswa kua karibu na wewe kuliko unavyodhani. Kabla ya kulala yasome, kabla ya kuanza shughuli nyingne yasome. Kufanya hivyo kunaweka akili yako kua kwenye mstari sahihi wa kuhakikisha unajikita kwenye vitu vyenye mchango kwenye malengo husika. Pia utavutia watu au mazingira ambayo yanaendana na malengo yako hata yale ulodhani ni magumu utashangaa fursa zinafunguka hatua kwa hatua. Fanya hivyo ujionee mwenyewe

18. Dereva wa maisha yako ni wewe chukua umiliki wa matokeo yako (Take ownership of your outcomes). Wengi wetu tunaishi kama abiria kwenye maisha, halafu tunashangaa tunakoelekea, au tunalaumu kwa yanayotokea. Sasa acha kua abiria wa maisha yako, nenda kwenye kiti cha dereva chukua usukani wa masiha yako. Wajibika kwa matokeo unayopata.

19. Vitu vinavyozuia mafaniko ya mtu mara nyingi sio vile asivyovijua bali ni vile anavyovijua ambavyo sio kweli. Cha ajabu tunafahamu vingi sana. Ila vingi kati ya hivyo ni vya uongo na ndivyo vilivyotufikisha hapa tulipo. Halafu cha ajabu kingine vile vya uongo ndo tumeweka imani yetu huko, na ndivyo vinaamua maisha yetu. Kabla hujangundua usijokijua, anza kugundua unachokijua ambacho sio sahihi.

20. Jitahidi kuzungukwa na watu watakao kunyanyua juu zaidi. Ukweli ni Wengi tunapenda kukaa na watu tunaowazidi ili watuone vichwa kwelikweli. Tunapenda makundi ambayo sisi ndo tunakua wazungumzaji wa kuu tunaomiliki mazungumzo, kila ukisema uantaka watu waseme ndio mzee. Sasa kuna habari sio nzuri kama unatabia kama hiyo. Maana wewe ni wastani wa watu 5 wanaokuzunguka. Kama umezungukwa na vilaza 9 wewe utakua wa 10. Njia pekee ya kutoka hapo ulipo ni kuzungukwa na watu waliofanikiwa kukuzidi wewe ambapo utajifunza mbinu walizotumia kufika waliko. Sio lazima ukamtafute Bill gate au Buffet, vipo vitabu vizuri vinavyoelezea walivyoanza mpaka waliko fika. Zungukwa na vitabu vya watu wakubwa waliofanikiwa. Chimbua maarifa ya watu hao na tendea kazi unachojifunza, uone kama utabaki ulipokua .

Asanteni sana tukutane wiki ijayo. Kama utapenda kupata kitabu hiki cha The ONE THING wasiliana nami. Nitakupatia bure kabisa.

Makala hii imeandikwa na Ndugu Daudi Mwakalinga mwandishi, mhamasishaji na mshauri katika masuala ya kilimo. Unaweza kuwasiliana nae kwa simu 0763 071007 au 0658 587029 au email daudimwakalinga@yahoo.com au dd.mwakalinga@gmail.com

SOMA; Karibu Kwenye Semina Ya Mafanikio Kwenye Biashara Mwaka 2015.

KITABU; Kwa Nini Wewe Ni Mjinga, Masikini Na Mgonjwa(Why You’re Dumb, Sick And Broke)

Rafiki yangu na msomaji mzuri wa AMKA MTANZANIA bwana Jiduma Luhende kitambo kidogo alinitumia kitabu hiki kinachoitwa Why You’re Dumb, Sick And Broke kilichoandikwa na Randy Gage.

Baada ya kukisoma kitabu hiki nimejifunza mambo mengi sana kwa nini ujinga, maradhi na umasikini tunavikaribisha sisi wenyewe. Ujinga, umasikini na hata maradhi yanayokusumbua wewe umeyakaribisha wewe mwenyewe kwa mawazo uliyoweka au uliyowekewa kwenye kichwa chako.

Kitabu hiki kinaelezea ni jinsi gani jamii imejenga picha hasi kuhusu utajiri, vyombo vya habari na hata tamthilia mbalimbali zinaonesha utajiri kama kitu kibaya sana na matajiri kama watu ambao maisha yao hayana furaha na wabinafsi wenye roho mbaya. Picha hii tunayoingiziwa kila siku inatufanya tuone umasikini ndio wenye furaha na roho nzuri.

dumb

Kitabu hiki pia kimeeleza ni jinsi gani dini mbalimbali tunazoamini zinatutengeneza kuwa masikini. Ameeleza kwa mifano mizuri sana mambo yanayofanyika kwenye dini kwa kujua au kutojua lakini yanakufanya wewe uone ni vizuri kuwa masikini kuliko kuwa tajiri.

Kitabu hiki hakikuacha nyuma mchango wa serikali kwenye kukufanya wewe uwe mjinga na masikini. Serikali ina mpango mzuri sana wa kuhakikisha wewe unaendelea kuwa mjinga na masikini ili uendelee kuitegemea kwa kila kitu na usiwe na nguvu ya kuihoji. Kwa njia hii serikali nyingi duniani zinaadhibu wenye fedha nyingi na utajiri na kubembeleza wale ambao ni masikini.

Kuna mambo mengi sana kwenye kitabu hiki ambayo ukiyasoma utabadili kabisa mtazamo wako juu ya maisha yako kuhusu utajiri na umasikini.

Katika kitabu hiki mwandishi ameshauri biashara tatu ambazo mtu anaweza kuzifanya na akawa na uhuru wa kifedha. Tatizo kubwa la biashara nyingi ambazo watu wanafanya ni kwamba inakuwa vigumu sana biashara kujiendesha zenyewe bila ya uwepo wa mmiliki kwa asilimia kubwa. Hii inakufanya wewe mmiliki wa biashara kupoteza umiliki wako, badala ya wewe kumiliki biashara, biashara inakumiliki wewe.

Mwandishi ameshauri biashara tatu ambazo kati ya hizo mbili unaweza kuzianza ukiwa na mtaji kidogo ila baadae ukajenga biashara kubwa sana ambayo haitakumiliki. Sitakuambia biashara hizi hapa, soma kitabu hiki halafu ukishafikia ambapo mwandishi ameshauri kuhusu biashara hizi niandikie email kwenye amakirita@gmail.com kuniambia ulivyozielewa biashara hizo kisha nitakushauri na kukupa mwanga zaidi kuhusu biashara moja au mbili kati ya hizo ambayo ndio nafanya kila siku na inaonesha mafanikio makubwa. Kwa kusoma kitabu hiki na kupata ushauri huo juu ya biashara unaweza kupata fursa kubwa sana kwenye maisha yako ambayo itayabadili kabisa maisha yako.

kitabu kava tangazo

Nakusihi sana usome kitabu hiki, ni kitabu kifupi ambacho kinaeleweka haraka sana. Kitabu hiki kina kurasa zisizozidi 190 zenye maandishi, kama ukiamua kukisoma kwa nusu saa kila siku, baada ya wiki moja utakuwa umekimaliza na umejifunza mengi sana.

Kama utakisoma kitabu hiki mpaka mwisho utajua kwa nini wewe ni MJINGA, MASIKINI NA MGONJWA na utajua ni jinsi gani ya kuwa MJANJA, TAJIRI na AFYA NJEMA.

Angalizo, wakati unasoma kitabu hiki inabidi uwe na uwezo wa kuhoji kila unachokisoma, ndivyo mwandishi alivyokiweka kitabu hiki. Kinakuchochea uwe na uwezo wa kuhoji kila kitu kwenye maisha yako, kuanzia kazi unayofanya, wanaokuzunguka, dini yako, habari unazopata na hata serikali yako. Hivyo kama wewe ni mvivu wa kuhoji unaweza kuona kitabu hiki kinakufundisha uasi hasa linapokuja swala la dini au watu wanaokuzunguka.

Kitabu hiki kimetumwa kwa wanachama wa mtandao huu. Kama bado hujawa mwanachama na ungependa kupata kitabu hiki bonyeza maandishi haya na uweke email yako na uweke email yako kisha ujiunge na utatumiwa email yenye link ya kitabu hiki pamoja na vitabu vingine viwili.

Nakusihi tena soma kitabu hiki, hakuna utakachopoteza ila utakuwa na kila kitu cha kujifunza.

Nakutakia kila la kheri kwenye safari yako ya kuboresha maisha yako.

TUKO PAMOJA.

Tafadhali endelea kuwaalika marafiki zako kulike page yetu ya facebook. Bonyeza maandishi haya na kisha like halafu nenda sehemu ya invite friends kisha waalike nao walike ukurasa huu ili tuweze kuwafikia wengi zaidi. Asanye sana kwa ushirikiano wako.