Mbinu Tano Za Kukupa Pesa Na Mafanikio Makubwa.

Mara nyingi ili kufikia mafanikio makubwa zipo mbinu nyingi ambazo unaweza ukazitumia kwa kufikia mafanikio hayo. Ni mbinu ambazo zipo na zimekuwa zikutumiwa na watu wote wenye mafanikio kutimiza mipango na malengo yao siku zote. Leo katika makala hii, naomba nikukumbushe na kukushirikisha mbinu chache ambazo unaweza kuzitumia kukupa mafanikio makubwa:-
1. Jijengee tabia za mafanikio.
Kwa bahati mbaya au nzuri tofauti kubwa inayojitokeza kati ya watu waliofanikiwa na ambao hawajafanikiwa ipo kwenye tabia. Tabia ndizo zinazomfanya mtu akawa na mafanikio au asiwe nayo katika maisha yake. Unapokuwa na tabia nzuri za kimafanikio ni msingi muhimu wa kukupa mafanikio mkubwa tena ya kudumu.
Kwa hiyo kama unatabia kama kupoteza muda, matumizi mabovu ya muda na nyinginezo  hasi, maisha yako yakiwa mabovu usishangae. Hizi ni tabia ambazo kwa vyovyote ni lazima zikurudishe nyuma. Ili uweze kufanikiwa ni muhimu kujijengea tabia za mafanikio ambazo ni lazima zitakupa pesa na mafanikio makubwa katika maisha yako.
2. Jiwekee malengo.
Watu wenye mafanikio siku zote wanaongozwa na malengo. Wanakuwa ni watu wa kujiwekea malengo ya siku, juma, mwezi na hata malengo ya muda mrefu pengine kuanzia miaka mitano na kuendelea. Hii ni tabia ambayo inawafanya wafanikiwe kweye maisha yao na kuufikia uhuru wa kifedha.
Hata wewe ili uweze kufanikiwa na kuwa na mafanikio makubwa ni muhimu kujua upo ulazima wa wewe kujiwekea malengo yako kila siku. Unapojiwekea malengo yanakuwa yanakupa dira, nguvu na hamasa ya kuendelea mbele kwa kile ambacho unakifanya. Hii ndiyo siri mojawapo kubwa ya kupata pesa na mafanikio makubwa.
3. Jifunze kufanya kazi kwa bidii.
Kazi ni msingi wa maendeleo kwa maisha yako yote. Bila kufanya kazi hakuna mafanikio makubwa unayoweza ukayapata. Hiki ndicho kitu unachotakiwa kujua na kujifunza ni lazima kwako kufanya kazi tena kwa bidii zote na siyo kazi ya kitoto. Acha habari ya kujivutavuta linapokuja suala la kazi hilo halifai na litakukwamisha.
Hakikisha unajitoa kikamilifu kwa kile unachokifanya na kukamilisha majukumu yote. Ukiwa utaamua kweli kupiga kazi na kuchana na maneno hakuna mtu ambaye atakuzuia kwenye njia ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa. 
4. Jiwekee utaratibu wa kutunza akiba.
Huwezi kufanikiwa katika maisha yako ikiwa huna tabia ya kujiwekea akiba. Kujiwekea akiba ni kitu cha msingi katika safari ya kuelekea kwenye utajiri. Akiba hiyo unayojiwekea inakuwa ni muhimu sana na itakusaidia sana katika suala zima la kuwekeza. Bila kujiwekea akiba sahau kabisa kufanikiwa, hiyo itakuwa ni sawa na ndoto.
Ukiangalia watu wengi waliofanikiwa wengi wao ni watu ambao wamejiwekea akiba katika maisha yao siku zote. Unaweza ukaanza kujiwekea akiba kuanzia asilimia kumi mpaka hamsini kulingana na kipato ulichonacho. Hiyo itakuwani njia sahihi ya kwako kuelekea kwenye mafanikio makubwa na kukupa pesa za kutosha.
5. Jiwekee utaratibu wa kujifunza.
Njia rahisi ya kuweza kufikia uhuru wa kipesa ni kujifunza kila siku juu ya mafanikio na ni utaratibu ambao tumekuwa tukiuzungumzia mara kwa mara kwenye mtandao huu. Kujifunza ndiyo hitaji la kwanza la msingi ili kufikia mafanikio makubwa. Watu wenye mafanikio ni watu wa kujifunza kila mara bila kuchoka. Hiki ni kitu ambacho kinawafanya wawe na mafanikio makubwa siku hadi siku.
Mara nyingi watu wenye mafanikio wanautumia muda wao wa ziada kujifunza kupitia vitabu, semina au warsha mbalimbali. Ni lazima kwako kuwa maarifa mengi ili uweze kuyatumia kukufanikisha katika mambo yako. Hili ni jambo ambalo unatakiwa kulijua kwa ajili ya kujenga mafanikio makubwa.
Ikiwa utaamua kujijengea tabia hizi chache tu, uwe na uhakika zitakuwezesha kupata pesa na kuwa na mafanikio makubwa kabisa katika maisha yako.
Naomba nikutakie siku njema iwe ya mafanikio kwako na endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kujifunza kila siku.
Kwa makala nyingine nzuri karibu pia katika DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na uhamasika.
 Ni wako rafiki katika mafanikio,
IMANI NGWANGWALU,
0713 04 80 35,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: