Haya Ni Majibu Ya Maswali Kumi Ambayo Bado Yanakutatiza, Pata Mwanga Hapa.

Habari za leo mpenzi msomaji?
Naamini maisha yako yanazidi kuwa bora na imara kadiri siku zinakwenda. Hongera sana na jua kwamba hapo ulipofika bado ni chembe ndogo sana ukilinganisha na kule unakoweza kufika. Lakini huwezi kufika mbali kwa mara moja tu, kuna mchakato wa kwenda mbali zaidi na ndio umekuwa unaupata kupitia mafunzo mbalimbali unayopata kwenye blog zinazoendeshwa na AMKA CONSULTANTS.
Imebaki siku moja tu ili kuweza kujiunga na semina MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu. Kufikia kesho itakuwa ndiyo mwisho wa kujiunga na semina hii nzuri ambayo italeta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako. hivyo natumia nafasi hii kukusisitiza kama bado hujajiunga ufanye hivyo, kwa sababu ukikosa nafasi hii unakosa mambo mazuri sana.

MFANO WA CHETI UTAKACHOPATA KWA KUSHIRIKI SEMINA HII.

 
Kwa nini unanisisitiza sana kuhusu semina hii?
Kama unapata swali hili kwa nini nakusisitiza sana, sio kwa sababu nataka tu ujiunge na semina hii, bali kwa sababu najua ndio kitu unachohitaji sasa kuliko vitu vingine vyote kwenye maisha yako. Ndio, semina hii ni kitu unachohitaji sana.
Nimekuwa napata bahati ya kuongea na watu wengi ambao wamekuwa wanataka ushauri kwenye mambo mbalimbali yanayowapa changamoto kwenye maisha, na mara zote nimekuwa nakutana na kitu hiki kimoja, KUTOKUJIAMINI. Jamii yetu inatujenga katika misingi ambayo tunalazimika kuwa kama watu wengine badala ya kuwa kama sisi tunavyopenda kuwa. Tumejikuta tunalazimika kufanya mambo sio kwa sababu tunapenda ila kwa sababu tunategemewa kufanya vile. Hili limekuwa linafanya maisha ya wengi kuwa magumu sana.
Lakini kwa nini watu wafanye mambo ambayo yanapelekea maisha yao kuwa magumu? Kwa sababu hawajiamini, hawaamini kwamba wana uwezo mkubwa wa kuweza kuendesha maisha yenye furaha kwao na kwa wale wanaowazunguka. Hawaamini kwamba watu wanaweza kuwaheshimu licha ya kutofautiana nao. Hawaamini kwamba wanaweza kusema hapana kwenye vitu ambavyo hawataki. Na hawaamini kwamba mawazo yao na ndoto zao kubwa zinawezekana.
Na ni kazi ngumu sana kuvunja vikwazo hivi, ni kazi ngumu sana kuanza kujijengea imani hii, hasa pale ambapo umezungukwa na watu wale wale ambao wanakulazimisha uwe kama wao. Nimeona wengi wamejaribu ila wakashindwa. Na ndio maana semina hii itakuwa na mchango mkubwa sana kwenye mabadiliko yako kwenye maisha.
NA KITU KIKUBWA SANA AMBACHO SIKUKUSHIRIKISHA.
Katika mafunzo ya semina hii, tofauti na semina nyingine nyingi zilizopita, nitakuwa nakupa mfano hai wa maisha yangu. Kwenye kila somo nitakushirikisha sehemu ya maisha yangu ambapo nimelitumia na limeweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yangu.
Katika semina hii nitakushirikisha jinsi ambavyo nimeweza kuvuka changamoto nyingi huko nyuma kwa kutumia misingi hii na jinsi ambavyo ninaendelea kuzivuka na jinsi ninaishi kwa misingi hii na hivyo kuepuka changamoto nyingi za baadae.
Hii ni nafasi ya kipekee ambayo ni vigumu kuweza kuipata tena, ndio maana nakusisitiza sana ujiunge na mafunzo yako. Nina uhakika, narudia tena, NINA UHAKIKA maisha yako hayatabaki yalivyo baada ya wewe kushiriki semina hii. Nakusisitiza sana, karibu.
Na kumbuka utapata nafasi ya kuniuliza maswali moja kwa moja kupitia kundi la wasap, hivyo hii ni nafasi kubwa sana ya kujifunza na kuboresha maisha yako. huna sababu ya kujaribu kila kitu ndio ujue utafanya nini, unaweza kupunguza muda kwa kukwepa makosa ambayo nimefanya mimi na kuchukua yale ambayo yamenisaidia.
Na habari njema zaidi, unaweza ukapata mafunzo haya BURE KABISA, utawezaje, endelea kusoma.
Kujiunga na semina hii bonyeza haya maandishi na ujaze taarifa zako kisha lipa ada ya kushiriki semina ambayo ni tsh elfu 30. Ada tuma kwenye namba zifuatazo, tigo pesa na airtle money tuma kwenye namba 0717 396 253 mpesa tuma kwenye namba 0755 953 887. Jiunge leo kuhakikisha hukosi nafasi hii ya kipekee.
Natambua bado kuna wasomaji na marafiki wenye wasi wasi ikiwa semina hii inawafaa au la. Kwanza niseme semina hii sio inakufaa tu, bali hutakiwi kuikosa. Huwa siandai semina ambayo haitamsaidia mtu kutoka pale alipo. Ndio maana nakuambia, hii ni yako, usiiache ikupite.
Lakini pia natambua kuna watu wana maswali ambayo sijayajibu kwenye maelezo yote ambayo nimekuwa nayatoa, hivyo hapa naomba nijibu baadhi ya maswali muhimu sana yanayokutatiza.
SWALI; nimebanwa sana, sitakuwa na muda wa kufuatilia semina hii.
JIBU; huhitaji muda mwingi kwa siku ili kuweza kufuatilia, unahitaji kutenga nusu saa asubuhi ya kusoma email ya somo, na nusu saa jioni kwa ajili ya kupitia kwenye kundi la wasap, kuuliza maswali au kuchangia. Hivyo ni saa moja tu kwa siku. Ukiwa hapo ulipo, na ukiwa unaendelea kufanya unachofanya. Na kama kazi au biashara imekubana kiasi kwamba unakosa saa moja kwa ajili yako binafsi, anza kujipanga kuondoka kwenye kazi au biashara hiyo au anza kufanyia kazi vipaumbele vyako. Sio nzuri kwako.
SWALI; mambo mengi utakayofundisha kwenye semina hii ni yale yale ambayo najifunza kila siku.
JIBU; sio kweli, mambo yanaweza kuwa yale yale lakini jinsi utakavyoyapokea ni tofauti kabisa. Kwenye semina hii utayapokea kwa njia ya kuyafanyia kazi tu. Na hapa kila kitu kinakwenda kwa mfano, jinsi ambavyo mimi binafsi nimefanya au nimekuwa nafanya. Pia mafunzo haya yatakuwa yanakupa changamoto ya kuchukua hatua zaidi, sio kusoma tu na kusema nitafanya, bali kufanya hasa.
SWALI; gharama ya mafunzo haya ipo juu sana. Ingekuwa chini kidogo ningeshiriki.
JIBU; gharama ya kushiriki mafunzo haya ni tsh elfu 30. Utatumiwa mafunzo kwa siku 20, ukigawa ni sawa na tsh elfu moja mia tano kila siku (1,500/=). Sio fedha ndogo, lakini thamani utakayoipata ni kubwa sana ukilinganisha na kiasi unacholipia. Angalia gharama unazoweza kupunguza kwenye maisha yako ili usikose mafunzo haya. Kama huwa unakunywa soda, usinywe kabisa kwa mwezi huu wa 10, au kama unakunywa pombe usinywe kabisa kwa mwezi huu, au kama huwa unakula nje, usile kabisa mwezi huu, yaani chagua kitu kimoja ukiondoe kwa mwezi huu tu na utakuwa umepata mara mbili, umejifunza semina, na wakati huo umeondokana na tabia ambayo haikuwa na msaada kwako lakini ulishazoea kufanya. NYONGEZA; Kama utapata changamoto kwenye kuacha vitu hivyo nitakusaidia. Karibu.
SWALI; sina hakika kama hii semina nitapata thamani ya hiyo fedha nitakayotoa.
JIBU; isome bure. Cha kufanya jiunge na semina, lipia ada ya semina, pokea mafunzo yote. Halafu semina itakapoisha niandikie ujumbe, Makirita, nashukuru sana kwa semina yako uliyotoa. Japo kwa upande wangu sijaona msaada wowote au kitu kipya kilichoongezeka. Hivyo naomba unirejeshee ada niliyojiunga nayo. Tuma fedha hiyo kwenye namba yangu hii…….. Asante sana. Fanya hivyo na fedha yako inakuwa imerudi, unakuwa umepata mafunzo haya bure kabisa. Sitanii, ninakuhakikishia hili ninalokuambia, natoa thamani kubwa sana itakayoweza kubadili maisha yako, kama haitaweza una haki ya kudai kile ulicholipia. Na huu ni moja ya misingi utakayojifunza kwenye semina hii.
SWALI; kwa sasa sitajiunga na semina hii, nitajiunga wakati mwingine.
JIBU; hii ndio semina ya mwisho kwa mwaka huu. Halafu haitakuja kurudia tena, tangu tumeanza kutoa semina hatujawahi kurudia hata moja, kwa sababu kuna mambo mengi sana bado unatakiwa kujua na hivyo kurudia ni vigumu. Kuna semina zitakuja kuhusu uwekezaji, kuhusu kazi, kuhusu fedha na nyingine nyingi, kurudi nyuma ni kitu ambacho hakipo. Hivyo unapokosa hii, jua ndio umeikosa kabisa, huipati tena.
SWALI; ningependa kujiunga lakini sina fedha hiyo ya kujiunga.
JIBU; kwanza pole sana. Pili siku nyingine usirudie tena kutoa kauli kama hiyo. Kwa sababu kauli hiyo ndio inakuzuia kupata fedha. Badala ya kusema sina fedha, sema nitapataje fedha kwa ajili ya semina hii. Sasa kama kweli unataka kujiunga na semina hii ila fedha ndio kikwazo, fanya hivi, angalia watu wote ambao ni wa karibu kwako, ndugu, jamaa na marafiki. Na fikiria watu 10 ambao ukiwaambia kitu wanakuelewa, halafu wasiliana nao, waambie unahitaji kubwa sana la shilingi elfu tano tu, hapa unamwambia mmoja mmoja, na kwamba akusaidie elfu tano hiyo na utamrudishia ndani ya mwezi mmoja. Unahitaji watu sita ili upate elfu 30, lakini wasiliana na 10 au hata 20, kwa sababu kuna wengine watakuambia hawana, wengine watakwambia wana changamoto na mengine kama hayo. Ukishapata fedha hii, maana ni leo au kesho, jiunge, halafu niandikie email kwamba nawezaje kutengeneza elfu 50 ya ziada kwenye mwezi huu wa 10. Halafu tutawasiliana, nikushauri, kulingana na mazingira yako unawezaje kutengeneza fedha hiyo ili uwarudishie waliokupa na ubaki na ya ziada pia. Halafu utakuwa umepata njia ya kuongeza kipato pia. Yaani wewe utakuwa umepata vitu vitatu kwa wakati mmoja. Angalizo; uwe tayari kufanya kile ambacho tutashauriana ufanye, na usilete sababu.
SWALI; sijisikii tu kushiriki semina hii kwa sasa.
JIBU; nakuelewa na ninaheshimu hilo, kwa sababu hata ingekuwa bure bado kuna watu wasingetaka kushiriki. Hivyo kuwa na amani na endelea kujifunza kupitia makala mbalimbali. Ila pia nikukumbushe kama umekuwa unasoma makala hizi kwa muda, fikiria mara mbili, maana ni nafasi kubwa na nzuri sana unaiacha ipite.
Kama una swali ambalo sijalijibu hapo juu unaweza kuniandikia email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz na nitakuwa tayari kukujibu. Lengo langu kubwa kwenye maisha ni kuona watu wakiishi maisha yenye mafanikio na wanayoyafurahia kwa kuweka ubora kwenye kile wanachofanya na hata maisha yao kwa ujumla. Ndio maana inapotokea nafasi kama hii sipendi wewe rafiki na msomaji wangu uikose. Hebu chukua hatua sasa, IMEBAKI SIKU MOJA TU.
Kujiunga na semina hii bonyeza haya maandishi na ujaze taarifa zako kisha lipa ada ya kushiriki semina ambayo ni tsh elfu 30. Ada tuma kwenye namba zifuatazo, tigo pesa na airtle money tuma kwenye namba 0717 396 253 mpesa tuma kwenye namba 0755 953 887. Jiunge leo kuhakikisha hukosi nafasi hii ya kipekee.
Kama hukupata taarifa za mwanzo kuhusu semina hii haya ndio yatakayofundishwa;
SEMINA; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.
1. Nilizaliwa kushinda.
2. Maisha yangu ni jukumu langu.
3. Ninaamini ninaweza kushinda.
4. Ninapima ushindi wangu kwa malengo.
5. Mimi kama mshindi ni mwaminifu.
6. Nimejitoa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa.
7. Muda ni mali ya thamani kwangu.
8. Nimezishinda hofu zote.
9. Kujifunza kila siku ndiyo nguzo yangu.
10. Nimeacha kutafuta sababu.
11. Wakatishaji tamaa hawaniyumbishi.
12. Ninafanya kile nilichopanga kufanya leo.
13. Kukosea ni sehemu ya ushindi wangu.
14. Ninakazana kuwa bora na sio kuwashinda wengine.
15. Ninajua hakuna njia ya mkato.
16. Kulaumu na kulalamika ni mwiko kwangu.
17. Mimi ni king’ang’anizi, sikubali kukata tamaa.
18. Ninashukuru kwa maisha haya ya ushindi.
19. Ninashirikiana na washindi wenzangu.
20. Ninachukua hatua mara moja.
Masomo haya 20 yameandaliwa vizuri sana kiasi kwamba kadiri unavyokwenda unaendelea kuvunja minyororo yote ambayo inakuzuia kufikia mafanikio. Kumbuka mabadiliko ya kweli kwenye maisha yako yanaanza na wewe mwenyewe, na ndio maana mafunzo haya yameandaliwa ili kukuwezesha wewe mwenyewe kubadilika, kujiahidi kwamba utashinda na baadae utashinda kweli.
Ili kuhakikisha washiriki wanapata mafunzo bora, nafasi za ushiriki huwa zinakuwa chache. Hivyo ni vyema ukachukua hatua haraka.
Kujaza taarifa zako
bonyeza maandishi haya na malipo fanya kwa namba zifuatazo; M PESA 0755 953 887, TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253.
Chukua hatua haraka kabla nafasi hii ya kipekee haijakupita.
Nakukaribisha sana kwenye mafunzo haya ambayo ninaamini bila ya kusita kwamba yatabadili maisha yako. Nimejitoa kuweka kila ninachojua kwenye mafunzo haya ili yawe msaada mkubwa sana kwenye maisha yako, usijaribu kabisa kuyakosa.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
makirita@kisimachamaarifa.co.tz
P.S Kama bado hujajaza fomu ya kujiunga bonyeza maandishi haya sasa na ujiunge na mafunzo haya mazuri.
N;B Kumbuka IMEBAKI SIKU MOJA TU kujiunga na mafunzo haya, BONYEZA HAPA kujaza fomu sasa ili usikose mafunzo haya muhimu.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: