AMKA MTANZANIA

Chukua Hatua Juu ya Maisha Yako.

SOMA KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU.

Habari rafiki?

Moja ya mahitaji muhimu sana ya kuwa na maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa ni kujifunza kila siku.

Kujifunza kupo kwa njia nyingi, ila ya msingi kabisa ni kusoma vitabu.

Tafiti nyingi zinaonesha ya kwamba, mtu anayesoma vitabu vitano kwenye jambo lolote, anakuwa kati ya watu bora sana kwenye jambo lile.

Tafiti pia zinaonesha kwamba baada ya kuhitimu masomo, ni watu wachache sana wanaoweza kusoma angalau kitabu kimoja na kukimaliza kwa mwaka.

Na pia upo usemi kwamba, ukitaka kumficha Mwafrika kitu, basi kiweke kwenye maandishi.

Haya yote yanatufanya sisi ambao tuna kiu ya mafanikio kupata hamasa ya kusoma zaidi vitabu na kuyatumia yale ambayo tumejifunza ili maisha yetu yaweze kuwa bora zaidi.

Lakini changamoto kubwa kwa wengi imekuwa kwamba hawana muda wa kusoma vitabu, kwa sababu wapo ‘bize’ na mambo yao mengine.

Na hapa ndipo mimi Kocha wako nataka nikusaidie ili uweze kuondokana na sababu hizo, na angalau kila mwezi uweze kusoma kitabu kimoja.

Hivyo nimekuletea program inayoitwa KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU.

Hii ni program muhimu ya kusoma kurasa kumi tu kila siku za kitabu, hivyo hata ambaye amebanwa kiasi gani, anaweza kutenga muda wa kusoma kurasa kumi tu. Ukiweza zaidi ya hapo sawa, lakini kumi ni muhimu, kila siku, jumatatu mpaka jumatatu.

Katika program hii;

  1. Unaingia kwenye kundi maalumu la wasap la KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU.
  2. Unachagua mwenyewe kitabu gani unasoma kwa mwezi husika, iwe ni nakala tete (softcopy) au nakala ngumu (Hardcopy).
  3. Kila siku unasoma angalau kurasa kumi, unatushirikisha kwenye kundi kurasa ulizosoma na angalau aya moja ya nini umejifunza na unakwendaje kukifanyia kazi.
  4. Muda wa kushirikisha unachagua wewe mwenyewe, ila tu iwe ndani ya siku husika kuanzia saa sita na dakika moja usiku, siku inapoanza, mpaka saa tano na dakika hamsini na tisa siku inapoisha.
  5. Sheria kuu ya program hii ni usome kila siku, ukikosa siku moja unasamehewa, ukikosa siku mbili mfululizo na ukawa huna sababu ya msingi sana utaondolewa kwenye kundi.
  6. Ukiondolewa kwenye kundi, kwa kushindwa kuenda na nidhamu ya kusoma na kushirikisha kurasa kumi ulizosoma kila siku, utaweza kujiunga tena muda wowote kwa kulipa upya ada ya kujiunga.
  7. Nitakuwa nashirikisha baadhi ya vitabu vizuri kusoma, kwa wale ambao hawajui vitabu gani wasome.
  8. Nitakuwa nashauri mtu mmoja mmoja vitabu vipi vizuri kwake kusoma, kulingana na maono na malengo yake.
  9. Kwa wale wenye changamoto ya lugha, nitakuwa nawashauri njia bora za kupata vitabu vinavyowafaa kwa lugha ya Kiswahili.
  10. Itakuwa ni njia nzuri kwako kujijengea nidhamu nyingine pia, ukishaweza kusoma kila siku, unaweza pia kufanya mambo mengine ambayo umekuwa unataka kufanya ila unashindwa.

Kupata nafasi ya kuwa kwenye programu hii ya KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU, unapaswa kulipa ada ya kujiunga na kundi hili ambayo ni tsh 10,000/= . Ada hii inalipwa mara moja pekee, na kama utasoma na kushirikisha kila siku, hutahitajika kulipa tena ada. Ila kama hutasoma kwa siku mbili mfululizo, na bila ya sababu maalumu utaondolewa kwenye kundi na ukitaka kujiunga tena utahitaji kulipa ada upya.

Kuingia kwenye program hii, tuma ada kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe kwa njia ya wasap namba 0717 396 253 wenye majina yako na maneno KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU kisha utaunganishwa.

Karibu sana tusome kwa pamoja KURASA KUMI ZA KITABU KILA SIKU, KITABU KIMOJA KILA MWEZI NA VITABU 12 KILA MWAKA. Program hii itakupa maarifa na kujijengea nidhamu pia.

Rafiki yako na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Wasap; +255 717 396 253.

%d bloggers like this: