UCHAMBUZI WA KITABU; Winning The Loser’s Game (Mbinu Zisizopitwa Na Wakati Za Kufanikiwa Kwenye Uwekezaji).

Tangu uwekezaji kwenye masoko ya mitaji umeanza kufanywa kitaalamu, yaani kuwepo kwa taasisi zinazoajiri watu wenye uelewa mkubwa kwenye uwekezaji, uwekezaji umekuwa mgumu sana. Uwekezaji kwenye masoko ya mitaji umekuwa mchezo wa kushindwa kwa sababu watu wanaoshiriki mchezo huu wote wana uwezo mkubwa na ili mmoja afanikiwe, lazima mwingine ashindwe. Na hii yote imetokana na... Continue Reading →

UCHAMBUZI WA KITABU; The Craving Mind (Jinsi Tunavyonasa Kwenye Uraibu Na Jinsi Ya Kuvunja Tabia Mbaya.)

Akili zetu sisi binadamu ni kitu cha ajabu sana, ni kitu ambacho kina nguvu ya kufanya makubwa kuliko tunavyoweza kutegemea. Lakini cha kushangaza ni kwamba, mtu anaweza kuitawala akili yake akafanya makubwa, au akatawaliwa na akili yake na kuwa mtumwa maisha yake yote. Tumekuwa tunaona watu wengi wakiingia kwenye uraibu (addiction) wa madawa ya kulevya,... Continue Reading →

UCHAMBUZI WA KITABU; Stories For Work (Mwongozo Wa Kutumia Hadithi Kwenye Kazi Na Biashara).

Kuna aina kuu mbili za fasihi, fasihi simulizi na fasihi andishi. Kwa asili, sisi binadamu tumeishi kwa kipindi kirefu kwenye fasihi simulizi kuliko fasihi andishi. Tangu enzi na enzi, watu walikuwa wakifundishana na kurithishana maarifa kwa njia ya hadithi na masimulizi. Kumekuwepo na hadithi nzuri za kufundisha na hata kuburudisha. Watu wanaelewa sana kitu kinapoelezwa... Continue Reading →

UCHAMBUZI WA KITABU; Right Risk (Misingi Kumi Ya Kupiga Hatua Kubwa Kwenye Maisha Yako Kwa Kuchukua Hatari Sahihi).

Kitu pekee ambacho tuna uhakika nacho kwenye maisha ni kwamba hakuna kitu chenye uhakika. Yale maisha ambayo tumekuwa tunadanganywa kwamba ukifanya vitu fulani basi utakuwa na uhakika wa maisha, hayana uhalisia katika zama hizi. Tunaamini kwamba kuna watu wenye majibu yote na majibu sahihi, lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu mwenye majibu yote na majibu... Continue Reading →

UCHAMBUZI WA KITABU; The 80/20 Principle (Siri Ya Kupata Matokeo Makubwa Kwa Kutumia Rasilimali Chache).

Mwaka 1869 mchumi Vilfredo Pareto alitoa andiko lake la kiuchumi ambapo alionesha kwamba asilimia 80 ya ardhi ya Italia ilikuwa inamilikiwa na asilimia 20 ya watu. Hakuishia hapo, alionesha hata kwenye shamba, asilimia 20 ya mimea ndiyo ilitoa asilimia 80 ya mazao. Dhana hii imefuatiliwa kwa muda mrefu na kuonekana inakubali kwenye kila eneo, kuanzia... Continue Reading →

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑