Rafiki yangu mpendwa,
Aliyewahi kuwa raisi wa Marekani Harry Truman, aliwahi kunukuliwa akisema; “Siyo wasomaji wote ni viongozi, lakini viongozi wote ni wasomaji.”
Hilo linaweza kusemwa kwenye maeneo mengine yote ya maisha, kuanzia mafanikio, fedha, mahusiano na hata furaha.
Kwa kifupi ni kwamba japo siyo wasomaji wote ni watu waliofanikiwa, lakini watu wote waliofanikiwa ni wasomaji.
Swali kwako rafiki yangu mpendwa, je umejiweka upande gani?
Je umejiweka upande wa wasomaji ambapo unakuwa na nafasi kubwa ya kufanikiwa kwenye maisha?
Au umejiweka upande ambao siyo wa wasomaji na hivyo kujizuia kabisa kufanikiwa?
Rafiki, unasoma hapa kwa sababu unataka mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Na neno moja nililo nalo kwako kama rafiki yako ni hili, kuwa msomaji.
Na siyo tu msomaji, bali msomaji wa vitabu.
Iko hivi rafiki, chochote unachotaka kujua ili uweze kufanikiwa, tayari kimeandikwa kwenye kitabu fulani.
Kitu kimoja ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba hakuna chochote unachohitaji kujua ili ufanikiwe ambacho huwezi kukipata kwenye vitabu.
Sikuambii hayo kwa kubahatisha, bali kwa uhakika na kwa uzoefu.
Kwa sababu kwa hatua zote nilizopiga kwenye maisha yangu mpaka hapa nilipofika sasa, mchango mkubwa kabisa umetokana na usomaji wa vitabu.
Najua unakubaliana na mimi kwenye haya, lakini ndani yako unajikumbusha jinsi ambavyo umekuwa unadhamiria sana kusoma vitabu ila unakwama.
Unapanga kabisa kwamba usome kitabu, unaanza na kukisoma, lakini hufiki mbali. Unaishia kupotezwa na usumbufu mbalimbali unaokuzunguka.
Mimi kama rafiki yako naijua sana hiyo changamoto, nimeipitia na kuweza kuivuka.
Na kwa sababu nakujali sana kama rafiki yangu, nimekuandalia njia bora ya kuweza kuvuka changamoto hiyo pia.
Nimekuandalia njia ambayo itakuwezesha kusoma vitabu, kuvielewa kwa kina na kuyafanyia kazi yale unayojifunza.
Njia hiyo ni programu maalumu ya usomaji inayoitwa TUSOME PAMOJA DAILY.

Hii ni programu ya kundi la wasap ambapo wanachama kwa pamoja wanashirikiana kusoma.
Kila mmoja anashirikisha kile alichosoma kwenye siku yake na aliyojifunza.
Programu hiyo ya kipekee ina nguvu kubwa mbili;
Nguvu ya kwanza ni kuzungukwa na watu sahihi.
Unakuwa kwenye kundi la wasomaji wenzako kitu ambacho kinakupa msukumo wa kusoma zaidi.
Unapoona wenzako wanasoma na kushirikisha, wewe pia utasukumwa kusoma na kushirikisha.
Nguvu ya pili ni ya kuwepo kwa mtu anayekufuatilia kwa karibu katika usomaji wako.
Kuna nyakati utakutana na changamoto na vikwazo mbalimbali vinavyoathiri usomaji wako.
Katika nyakati kama hizo ndipo hatari kubwa ya kuacha kusoma ilipo.
Lakini kwa kuwa kwenye programu hii, unafuatiliwa kwa karibu na Kocha ili uweze kuendelea na safari ya usomaji.
Rafiki, sijui nikuambieje lakini ukweli ni kwamba mwarobaini wa tatizo lako la usomaji sasa umepatikana.
Chagua sasa kujiunga na programu ya TUSOME PAMOJA DAILY ili ujijengee tabia ya kujisomea kila siku na uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Manufaa makubwa ya kuwa kwenye programu ya TUSOME PAMOJA DAILY.
Kuna manufaa mengi sana ya kuwa kwenye programu mpya ya TUSOME PAMOJA DAILY.
Haya 10 ni ya uhakika kabisa ambayo unakwenda kunufaika nayo;
1. Kuweza kusoma na kukamilisha angalau kitabu kimoja kwa mwezi. Hapo ni zaidi ya vitabu 10 kwa mwaka, idadi ambayo wengi sana hawaifikii.
2. Kushauriwa na kuchaguliwa vitabu vizuri vya kusoma kulingana na hali yako.
3. Kujifunza kupitia usomaji wa wengine, hivyo wakati unasoma kitabu ulichochagua, unaendelea kujifunza kupitia vitabu wanavyosoma wengine.
4. Kusimamiwa kwa karibu kwenye usomaji wako ili chochote kisikurudishe nyuma.
5. Kuendelea kupata mafunzo na hamasa ya umuhimu wa kusoma na jinsi ya kusoma kwa manufaa.
6. Kupata chambuzi za vitabu vingi na vizuri kwa lugha rahisi ya Kiswahili.
7. Kutafutiwa na kutumiwa kitabu chochote kile unachotaka. Hapa utachangia gharama ya kununua na kutumiwa kitabu ulipo.
8. Kupata ufumbuzi na suluhisho la changamoto zozote zinazoathiri usomaji wako.
9. Maarifa unayopata kupitia usomaji yatakufanya uwe bora kabisa wewe binafsi.
10. Maarifa hayo pia yatakuwezesha kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Rafiki yangu mpendwa, manufaa hayo makubwa, pamoja na mengine mengi unakwenda kuyapata ndani ya programu ya TUSOME PAMOJA DAILY.
Na habari njema kabisa kwako wewe rafiki yangu ni kwamba, unakwenda kuyapata manufaa hayo makubwa kwa kuchangia kiasi cha TSHS 9,900/= TU Kwa Mwezi.
Yaani kwa siku 30 za mwezi ambazo unanufaika na programu hiyo nzuri, unachangia kiasi cha shilingi elfu tisa na mia tisa.
Hiyo ni sawa na kuchangia shilingi mia tatu na thelathini kwa siku.
Swali kwako rafiki yangu, je utakubali ukose manufaa hayo makubwa sana ya programu ya TUSOME PAMOJA DAILY kwa kuepuka gharama ndogo ya mia tatu?
Siamini hilo linaweza kutokea kwako.
Hivyo basi, fungua kiungo hiki kinachofuata hapa na moja kwa moja ujiunge kwenye kundi la programu ya TUSOME PAMOJA DAILY.
Kiungo; https://bit.ly/tusomepamoja
Kwa maelezo zaidi wasiliana na namba 0752 977 170 sasa.
Rafiki, programu inakwenda kuanza rasmi tarehe 01/06/2022.
Lakini unapaswa kujiunga mapema ili kujihakikishia nafasi yako.
Kutokana na ufuatiliaji mkubwa tunaokwenda kufanya kwa washiriki wa programu hii, nafasi zitakuwa chache sana.
Hivyo chukua hatua sasa ili usikose nafasi hii adimu.
Fungua sasa link; https://bit.ly/tusomepamoja na ujiunge kwenye kundi la programu ya TUSOME PAMOJA DAILY.
Rafiki, nikimalizia na kauli nyingine ya aliyekuwa raisi mwingine wa Marekani, Richard Nixon aliyewahi kusema; “Tabia moja ambayo viongozi wote wanayo ni usomaji. Usomaji siyo tu unakuza akili, bali pia unaupa ubongo mazoezi. Vijana wa leo ambao wanatumia muda wao mwingi kuangalia TV hawawezi kuwa viongozi wazuri wa kesho.”
Unazidi kuona msisitizo hapo rafiki yangu, kama unataka kufanya makubwa, hakuna namna unaweza kukwepa usomaji.
Na ndiyo maana nakukaribisha sana kwenye programu ya TUSOME PAMOJA DAILY.
Ungana na viongozi wenzako tusome kwa pamoja.
Fungua hapa kujiunga; https://bit.ly/tusomepamoja
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani.