ONGEA NA COACH; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuishinda Hofu Ya Kushindwa Na Kuweza Kufanikiwa.

Habari rafiki?

Karibu kwenye makala yetu ya ONGEA NA COACH ambapo nimekuwa nakushirikisha mambo mbalimbali kuhusu maisha ya mafanikio kwa njia ya video.

Kwenye kipindi chetu cha leo nakwenda kukushirikisha kuhusu kuishinda hofu ya kushindwa.

Ukweli ni kwamba kila mtu anapenda kuwa na maisha bora na yenye mafanikio. Kila mtu anapenda kupiga hatua kwenye maisha yake, anapenda kutoka pale alipo sasa na kupiga hatua zaidi.

Watu wengi hupanga kabisa namna ya kutoka pale walipo sasa, huweka malengo na mipango mikubwa, ambayo ukiisikia, unajua kabisa ya kwamba mtu huyo atakuwa mbali zaidi siku zijazo.

Lakini changamoto kubwa sana inajitokeza pale mtu anapoanza kufanya, pale mtu anapochukua hatua. Hapa ndipo anakutana na vitu vingi vinavyompa kikwazo au sababu ya kwa nini asianze au kuendelea kwa sasa.

Pamoja na sababu nyingi ambazo mtu anaweza kujipa au kukubaliana nao, mzizi mkuu upo sehemu moja; HOFU.

Watu wengi wanashindwa kuanza kutokana na kuwa na hofu. Wengi wanakuwa na hofu kwamba huenda watashindwa, na wakishindwa mambo yatakuwa mabaya zaidi ya yalivyo sasa. Hivyo wanaacha kabisa kuchukua hatua.

Kwenye kipindi cha leo, nimekupa njia tatu muhimu za kuweza kuishinda hofu hii ya kushindwa. Kwa kufanyia kazi njia hizo tatu, kamwe hutoshindwa kuchukua hatua kwenye maisha yako kwa sababu ya hofu. Badala yake hofu itakuwa hamasa kubwa kwako kuchukua hatua.

Angalia kipindi hichi cha leo, ujifunze mambo haya matatu, uanze kuyafanyia kazi na maisha yako yabadilike.

Kuangalia kipindi hichi cha leo, bonyeza maandishi haya. Pia unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini kama kifaa chako kinaruhusu.

Usikubali kabisa hofu ya kushindwa iwe sababu ya wewe kushindwa. Hakuna kushindwa kwenye maisha mpaka pale wewe mwenyewe unapoamua kwamba umeshindwa. Vinginevyo, chukua hatua, jifunze na kuwa bora zaidi.

KWA NINI SIYO TAJIRI

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

ONGEA NA COACH; Hii Ndiyo Biashara Bora Kwako Kufanya Na Yenye Mafanikio Makubwa Sana.

Habari za leo rafiki yangu?

Karibu kwenye kipindi chetu cha leo cha ONGEA NA COACH ambapo nimekuwa nakushirikisha video zenye mafunzo mbalimbali ya kukuwezesha kuwa bora zaidi na kuweza kufanikiwa. Nimekuwa nakusisitiza mara zote kwamba MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA, hakuna yeyote anayeweza kuichukua haki hiyo kwako.

Kwenye kipindi cha leo nimekushirikisha jambo muhimu sana kuhusu biashara.

Watu wengi ambao wamekuwa wanapanga kuingia kwenye biashara, wamekuwa wanauliza swali ambalo siyo sahihi. Swali lao ni je biashara ipi yenye mafanikio makubwa naweza kufanya?

Swali hili lina ndugu zake kama; wapi nikiweka fedha zangu baada ya miezi sita nakuwa nimetengeneza mara mbili?

Maswali yote hayo siyo sahihi na yamewapotosha wengi. Yamewafanya wengi kukimbizana na vitu ambavyo siyo sahihi kwao, kupoteza fedha na hata muda pia. Huku wakiacha biashara nzuri ambazo wangeweza kufanya na kufanikiwa sana.

Kwenye kipindi hichi nimekuonesha kwa kina aina ya biashara ambayo unaweza kuifanya na ukafanikiwa sana.

Kwenye kipindi hichi nimekueleza mambo mawili muhimu sana kuhusu biashara ambayo wengi hawajawahi kuambiwa na hawapendi kusikia. Kwa kujua hayo mawili tu, kunakutosha kufanya biashara yako kwa utofauti mkubwa.

Pia nimekupa hatua tatu muhimu za kuanza biashara yoyote ile unayoanza ambazo zitakuwezesha kuanza biashara sahihi na kufanikiwa pia.

Kupitia kipindi hichi cha leo, nimekuonesha wapi pa kuanzia na uanzeje, hata kama upo chini kabisa. nimekupa hatua kwa hatua uanzie wapi na ukueje zaidi.

Mwisho kabisa sijaacha kuzungumzia kuhusu mikopo kwenye biashara. Kwa sababu hii imewasumbua wengi na kuwaangusha. Hapa nimekupa tahadhari kubwa sana kuhusu mikopo na namna gani unapaswa kuwa makini nayo.

Kama upo kwenye biashara, au unapanga kuingia kwenye biashara, basi hichi ni kipindi kimoja ambacho unapaswa kukiangalia, na tena kukiangalia kwa umakini mkubwa. Kwa sababu yapo mambo mengi madogo madogo ambayo hutayasoma kwenye vitabu wala kuyapata kwenye ushauri wa biashara unaopewa na wengine.

Angalia kipindi hichi cha leo kwa kubonyeza maandishi haya, au kwa kuangalia moja kwa moja hapo chini iwapo kifaa chako kina uwezo huo.

Neno langu kwako ni moja tu, kila biashara ni nzuri kama tayari upo kwenye biashara. Acha kupoteza muda kujiuliza biashara ipi nzuri, ingia kwenye biashara na utaona namna ya kutengeneza biashara nzuri kwako.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

BIASHARA NDANI YA AJIRA SOFT

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

Changamoto ya Ajira Na Hatua Za Kuchukua Kwa Wahitimu Ambao Bado Hawajapata Ajira.

Habari za leo rafiki yangu?

Karibu kwenye kipindi chetu cha leo cha ONGEA NA COACH ambapo nimekuwa nakushirikisha mambo muhimu ya kuweza kuwa na maisha bora na yenye mafanikio.

Katika kipindi cha leo nakwenda kukushirikisha kuhusu changamoto ya ajira na hatua za kuchukua kwa wahitimu ambao hawajapata ajira.

Hili liko wazi sasa ya kwamba ajira ni changamoto. Mara zote tunaona nafasi chache za kazi zinazotangazwa, wanaomba watu wengi mno. Wahitimu ni wengi kuliko nafasi za ajira zinazopatikana.

Hali hii imekuwa inawaumiza vijana wengi ambao wameishi maisha yao yote wakiambiwa wasome kwa bidii, wafaulu na watapata ajira nzuri na kuwa na maisha mazuri.

Vijana wanakazana kusoma kweli, wanafaulu na kuhitimu, lakini ajira zinakuwa changamoto.

Katika kipindi cha leo nimezungumzia mambo matatu muhimu sana;

Jambo la kwanza ni kuendelea kuomba kazi kwa wale ambao ndiyo wamehitimu, lakini wakati huo wasiruhusu maisha yao kusimama wakisubiri ajira. Badala yake waendelee kufanya mambo mengine pia.

Jambo la pili ni kufanya maamuzi magumu ya kuachana na harakati za jira, hasa pale ambapo umehitimu zaidi ya miaka miwili na umetafuta ajira bila ya mafanikio.

Jambo la tatu ni hatua za kuchukua, hapa nimekushirikisha ufanye nini sasa pale ambapo umefanya maamuzi magumu ya kuachana na zoezi la kutafuta ajira na kushika hatamu ya maisha yako. Nimekushirikisha maeneo ambayo unaweza kuanzia na ukaweza kupiga hatua kwenye maisha yako.

Angalia somo hili, jifunze na chukua hatua.

Unaweza kuangalia somo hili kwa kubonyeza maandishi haya, au kwa kuangalia moja kwa moja hapo chini.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

fb instagram

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog

ONGEA NA COACH; Aina Kuu Mbili Za Kipato Na Jinsi Ya Kuzitumia Kufika Kwenye Utajiri.

Habari za leo rafiki yangu?

Karibu tena kwenye kipengele hichi cha makala za ongea na coach ambapo nimekuwa nakuandalia masomo kwa njia ya video. Kupitia masomo haya, nimekuwa nakushirikisha maarifa muhimu sana ya kukuwezesha kupiga hatua kwenye maisha, kuzivuka changamoto na hata kufikia utajiri.

Katika kipindi chetu cha leo tunakwenda kujifunza kuhusu aina kuu mbili za kipato na jinsi ya kuzitumia kufika kwenye utajiri.

Kila mtu huwa anaongelea kuhusu kipato,

Wapo wanaosema kipato hakitoshi, wengine kipato kigumu, wengine wanafikiria kuongeza kipato.

Lakini wote hawa wanazungumzia aina moja pekee ya kipato, ambayo kwa vyovyote vile haiwezi kukufikisha kwenye utajiri na uhuru wa kifedha.

Zipo aina kuu mbili za kipato, aina ya kwanza ni ya kufanya maisha yaende, na aina ya pili ni ya kutengeneza utajiri mkubwa kwenye maisha yako.

Hizi ni aina mbili za kipato ambazo kila mtu ambaye yupo makini na maisha yake anapaswa kuzijua, kuzifanyia kazi na kupata matokeo mazuri.

Kwenye kipindi cha leo nimekushirikisha aina hizi, na kwa mifano kabisa pamoja na namna ya kutumia aina hizo kutengeneza utajiri na uhuru wa kifedha kwenye maisha yako.

Kuzijua aina hizi mbili za kipato na jinsi ya kuzitumia kufikia utajiri, angalia kipindi hichi cha leo.

Unaweza kuangalia kipindi hichi kwa kubonyeza maandishi haya na ukaenda kuangalia. Au kama kifaa chako kinaruhusu, unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini.

Ni imani yangu kwamba utaelewa vizuri aina hizi mbili za kipato na jinsi ya kuzitumia, na kama hutaelewa kwa namna yoyote, niwekee maoni yako chini ya somo hili la leo na nitakupa majibu sahihi.

Jifunze na chukua hatua, kuyaweka yale uliyojifunza kwenye matendo ili maisha yako yaweze kubadilika.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Hii Ndiyo Siri Kubwa Ya Waandishi Wenye Mafanikio Makubwa.

Rafiki,

Wahenga walisema ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Dunia inapenda kuona matokeo, lakini haipendi kuona ule mchakato wa matokeo hayo, namna gani yamefikiwa.

Huwa tunaona habari za watu waliotoka chini kabisa na kufanikiwa sana, lakini hatupati ile picha halisi ya njia walizopita mpaka wakafanikiwa. Utasikia maneno kwamba alikazana sana na hakukata tamaa, mwishowe amefanikiwa.

Lakini huenda huko katikati mtu alikata tamaa kwenye mambo mengi. Huenda mpango aliokuwa nao mwanzo siyo huo ambao amefanikiwa nao. Huenda kuna mahali alivunja sheria, alikiuka taratibu na alifanya mambo ambayo kikawaida hayawezi kukubalika, lakini yakamwezesha kuvuka hatua moja kwenda nyingine.

Ninachotaka kukuambia ni kwamba, kuna safari ndefu na ngumu ya kufika popote ambapo mtu anataka kufika.

Kwenye uandishi napo mambo yako hivyo hivyo. Wapo waandishi wenye mafanikio makubwa, walioandika vitabu vingi ambavyo vimegusa maisha ya wengi. Lakini wengi wamekuwa wanaviona vitabu pekee, hawaoni maisha nyuma ya vitabu hivyo.

Wengi wamekuwa wanafurahia mafanikio ya waandishi wenye mafanikio, na wao kukimbilia kuandika, bila ya kujua kazi kubwa iliyopo nyuma ya uandishi wenye mafanikio.

Mmoja wa waandishi ninaowakubali sana, alikuwa anahojiwa, akaulizwa mchakato wake wa uandishi wa vitabu ukoje. Akajibu bila ya kusita kwamba kabla hajaandika kitabu kimoja, basi anasoma vitabu 250, ndiyo vitabu mia mbili na hamsini. Unaweza kuona namna gani hiyo kazi siyo ndogo wala rahisi, hapo ni kusoma na hata hajaanza kuandika.

Kwenye kipindi cha leo nimekuandalia somo kuhusu siri kubwa ya waandishi wenye mafanikio makubwa. Angalia kipindi hichi kujifunza kitu muhimu unachopaswa kukipa kipaumbele kama unataka kufanikiwa kwenye uandishi.

Na hata kama wewe siyo mwandishi, angalia kipindi hichi, kitakupa funzo kubwa la namna unavyopaswa kujitoa kwa ajili ya mafanikio.

Unaweza kuangalia kipindi hichi kwa kubonyeza maandishi haya. Au ukaangalia moja kwa moja hapo chini kama kifaa chako kina uwezo huo.

Jifunze na chukua hatua ili kuweza kufanikiwa kupitia chochote ambacho unafanya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Aina Mbili Za Madeni Na Madeni Ya Kuepuka Kwenye Maisha Yako.

Habari za leo rafiki yangu?

Hakuna kitu kimekuwa mzigo kwa wengi na kuwazuia kufanikiwa kama mikopo na madeni. Japo wengi wamekuwa wakidanganyika mikopo ina manufaa kwao, wengi wamekuwa wanauona ukweli halisi wa mikopo pale wanapoichukua.

Sasa changamoto kubwa sana kwenye madeni ni kwamba, watu wanadanganywa sana. Wamekuwa wanadanganywa na kauli kuu mbili;

Kauli ya kwanza ni kwamba huwezi kufanikiwa bila ya kukopa, au matajiri wengi wanakopa na ndiyo maana wamefikia utajiri.

Kauli ya pili ni ile kwamba mtu anakopesheka.

Hili ni kauli mbili ambazo zimewapoteza wengi, kwa kuwaingiza kwenye madeni ambayo hayana msaada kwao na kuishia kuteseka.

Kwenye kipindi chetu cha ONGEA NA COACH leo nimezungumzia na kuchambua aina kuu mbili za madeni ambazo unapaswa kuzijua kabla hujaingia kwenye madeni.

Pia nimekushirikisha madeni gani uyaepuke sana kwenye maisha yako, na madeni yapi ambayo yana msaada kwako. Kabla hata hujaanza kukadiria ni madeni gani mazuri kwako, nikuambie tu, madeni unayofikiria kwako ni mazuri ni mabaya mno.

Kwa mfano, kuchukua mkopo wa kujenga nyumba, kununua gari au hata kuanza biashara, ni madeni mabaya kwako na yatakurudisha nyuma. Kabla hujaanza kubisha hili, nakusihi uangalie kipindi hichi cha leo, ili uweze kupata maarifa sahihi na kuweza kuchukua hatua sahihi.

Kuangalia kipindi hichi kizuri cha leo kuhusu aina za madeni na madeni ya kuepuka, bonyeza maandishi haya.

Pia unaweza kuangalia kipindi hichi moja kwa moja hapo chini iwapo kifaa chako kinaruhusu.

Angalia kipindi hichi cha madeni, kisha chukua hatua ya kuepuka madeni ambayo hayana msaada kwako.

Pia karibu upate kitabu KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, ili uweze kujifunza mbinu za kuweza kuondoka kwenye umasikini. Kupata kitabu hichi angalia maelekezo ya picha hapo chini.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Je Inawezekana Kutengeneza Zaidi Ya Milioni Tano Kila Wiki Kupitia Intaneti? Ukweli Uko Hapa.

Habari za leo rafiki?

Kama wewe ni mtumiaji wa mtandao wa intaneti, utakuwa umeshawahi kupokea ujumbe unaokuambia kwamba kuna njia unaweza kutengeneza mamilioni ya fedha kupitia mtandao wa intaneti, bila ya kufanya kazi kubwa. Jumbe hizi zinakuwa na ushawishi sana wa kutaka kujaribu kile ambacho watu wamekuwa wanaambiwa.

Na ushawishi zaidi unatolewa na watu wanaodai kwamba wameshatengeneza kipato cha aina hiyo na kuonesha mchakato mzima wanaotumia wao na kipato walichotengeneza. Watu wamekuwa wakitamani kuchukua hatua hizo ili na wao waweze kutengeneza kipato hicho, lakini wanakutana na jukumu moja wanalopaswa kufanya. Na jukumu hilo ni kusambaza ujumbe wa kwamba mtu anaweza kutengeneza kipato kikubwa kwenye mtandao.

Kwa kuwa watu wana tamaa ya fedha, wanatuma ujumbe ule ili wapate fedha hizo, na hilo ndiyo linapelekea wewe kupokea ujumbe kwa watu wako wa karibu, wakikuambia fungua link fulani na utaweza kutengeneza mamilioni ya fedha. Ukifungua na wewe unaambiwa utume kwa wengi na mchezo unaendelea hivyo.

Kwenye kipindi cha leo nimelijadili hili kwa kina, uwezekano wa kutengeneza mamilioni kwenye intaneti na nini unapaswa kufanya ili kuweza kutengeneza kipato hicho.

Kabla hujakimbilia kutafuta hizo link za kutengeneza mamilioni kwenye intaneti, nakushauri sana uangalie kipindi hichi, kitakupa mwanga na hatua za kuchukua.

Kuangalia kipindi hichi cha leo bonyeza maandishi haya. Pia unaweza kukiangalia kipindi hichi moja kwa moja hapo chini.

Usikubali kudanganyika kwa namba yoyote ile, ijue misingi sahihi ya kutengeneza fedha kwenye intaneti kisha chukua hatua sahihi.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Sababu Moja Kubwa Inayopelekea Watu Wengi Kuendelea Kuwa Masikini Licha Ya Kufanya Kazi Sana.

Habari rafiki?

Fedha ni moja ya maeneo muhimu sana ya maisha yetu, ukiondoa hewa ambayo tunaipata bure bila ya kulipia chochote, kitu cha pili kwa umuhimu zaidi ni fedha, kwa sababu bila fedha, huwezi kupata chochote kwenye maisha. Najua unajua hata kupata maji safi na salama ya kunywa, unahitaji kuwa na fedha. Hivyo hilo halina ubishi.

Pamoja na umuhimu huu mkubwa wa fedha kwenye maisha yetu, bado watu wengi wanateseka sana kwenye swala la fedha. Wapo watu ambao wanafanya kazi sana lakini bado fedha ni changamoto kubwa kwao. Wapo ambao wanatengeneza kipato kikubwa lakini baada ya muda maisha yao yanakuwa magumu sana. Na wapo wale ambao wamekazana kwenye kazi zao, wakaweka juhudi za kutosha, lakini siku moja wakaambiwa kazi hakuna tena na maisha yao yakawa magumu mno.

Yote haya yanasababishwa na kosa moja kubwa sana ambalo watu wengi wanafanya, kuwa na mfereji mmoja wa kipato. Mtu anakuwa na njia moja pekee ya kumtengenezea kipato. Anaizoea njia hiyo na kuitegemea, pale unapotokea changamoto na kipato kwenye njia hiyo kikakauka, ndipo matatizo makubwa yanapoanza.

Katika somo letu la video leo, nakwenda kukushirikisha umuhimu wa kuwa na mifereji mingi ya kipato. Popote pale ulipo kwenye maisha yako, ni muhimu sana uwe na mifereji mingi ya kipato, uwe na njia nyingi za kukuingizia kipato. Hii ndiyo njia pekee unayoweza kujitengenezea uhuru wa maisha yako.

Kujifunza kwa kina kuhusu hili, angalia somo hili zuri la leo. Unaweza kuangalia somo hili kwa kubonyeza maandishi haya, au ukaangalia moja kwa moja hapo chini.

Karibu sana ujifunze na uweze kuchukua hatua ili uweze kujijengea uhuru wa kifedha.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Changamoto Ya Kutegemea Matangazo Kama Njia Ya Kutengeneza Kipato Kwenye Mtandao.

Habari rafiki?

Karibu kwenye kipindi chetu cha leo cha video ambapo tunakwenda kujifunza mambo muhimu ya kuzingatia katika kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti.

Zipo njia nyingi za kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti, lakini watu wengi wamekuwa wanakimbilia njia moja, ambayo inaonekana ni rahisi, lakini siyo njia bora.

Njia ambayo wengi wamekuwa wanapenda kuitumia ni matangazo. Wengi wamekuwa wakianzisha blog au kukuza mitandao yao kwa lengo la kuvutia watu wa kutangaza kupitia wao. Japo ni njia ambayo ukiweza kuifanyia kazi vizuri ina kipato kikubwa, ni njia isiyo na uhakika.

Kama unaendesha blogu za kujifunza kama ambavyo nimekuwa nakushauri, hutafikia hatua ya kuwa na wasomaji wengi ndani ya muda mfupi. Ni jambo lililo wazi kwamba watu wanapenda habari kuliko kujifunza, hivyo itakuhitaji muda mrefu.

Lakini zipo njia ambazo unaweza kuzitumia vizuri na kuanza kutengeneza kipato kwenye mtandao wa intaneti hata kama una wasomaji wachache. Njia hizo ndiyo unakwenda kujifunza kupitia somo letu la leo.

Karibu sana tujifunze pamoja maarifa sahihi ya kutengeneza kipato kupitia mtandao wa intaneti.

Unaweza kuangalia somo hili zuri la leo kwa kubonyeza maandishi haya. Pia unaweza kuangalia moja kwa moja hapo chini kama kifaa chako kinaruhusu.

Pata kitabu; JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, kitakuwezesha kuanzisha na kukuza blog yako na hatimaye kuweza kuitumia kutengeneza kipato.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.

Sababu Moja Kubwa Inayopelekea Biashara Nyingi Kufa.

Habari rafiki?

Watu wengi wamekuwa wakikazana kuanzisha biashara, wanajinyima kupata mitaji ili kuongeza vipato vyao kupitia biashara. Lakini cha kusikitisha, biashara hizo hufa na watu kupoteza fedha walizowekeza. Hii inawapelekea watu hao kukata tamaa na kuona biashara ni kitu kibaya sana.

Lipo kosa moja kubwa sana ambalo watu wengi wamekuwa wanalifanya kwenye biashara. Kosa hilo linapelekea biashara zao kufa haraka sana.

Kwenye somo letu hili la leo nimejadili kosa hili kubwa na namna ya kuliepuka ili biashara yako iweze kupona.

Naomba nisikueleze mengi hapa, bali uangalie somo hili mwenyewe na uweze kujifunza. Unaweza kuangalia somo hili kwa kubonyeza maandishi haya. Pia unaweza kuliangalia moja kwa moja hapo chini iwapo kifaa chako kinaruhusu.

Fanyia kazi haya ambayo umejifunza, ili uweze kuendesha biashara yenye mafanikio makubwa.