Rafiki,

Kuna mambo mawili muhimu kuhusu fedha,

Jambo la kwanza ni kuifanyia kazi fedha, hapa ni pale unapofanya kazi ili upate fedha, au kufanya biashara ili upate fedha. Upataji wako wa fedha unategemea uwepo wako kwenye kazi au biashara unayofanya.

Jambo la pili ni fedha kukufanyia kazi wewe, hapa ni pale ambapo fedha yako inafanya kazi na kuzalisha kipato, bila ya wewe kuwepo moja kwa moja.

Katika hali hiyo ya pili, ndipo uwekezaji unapohusika. Hapo ndipo unapopaswa kuiweka fedha yako mahali ambapo inaweza kuzalisha zaidi bila ya wewe kuwepo.

Zipo aina nyingi za uwekezaji, kuanzia kwenye masoko ya mitaji, kwenye ardhi na majengo, kwenye biashara na hata vitu vingine vya thamani.

Katika somo letu la leo, tunakwenda kujifunza uwekezaji kwenye soko la hisa na masoko ya mitaji.

Watu wengi wamekuwa hawauelewi uwekezaji kwenye hisa, wakiona ni kitu kigumu na kisichowafaa wao.

Wengine wamekuwa hawapendi kuchukua muda na kujifunza, badala yake wanachukua ushauri wanaopewa, ambao huwa siyo ushauri mzuri.

Wengine wamekuwa hawawekezi, kwa kusema ni bora hizo fedha wazizalishe kwa njia nyingine, kwa sababu uwekezaji kwenye hisa unalipa kidogo sana.

Wengine wamekuwa wanafikiri unahitaji kuwa na fedha nyingi sana ndiyo uweze kuwekeza kwenye ununuaji wa hisa.

Hayo yote siyo sahihi, mengi ni uongo ambao watu wamekuwa wakiuishi kwa kuamini ni ukweli.

Katika kipindi chetu cha leo cha ONGEA NA COACH nimekushirikisha msingi muhimu sana kwenye uwekezaji wa hisa na masoko ya mitaji.

Chukua muda wako na uangalie kipindi hichi, utauelewa uwekezaji kwenye hisa kwa urahisi na uweze kuchukua hatua.

Na mwisho kabisa, kila mtu anapaswa kuwekeza, bila ya kujali kipato chako ni kidogo au kikubwa kiasi gani. Hii ni kwa sababu uwekezaji unakuja kukusaidia zaidi baadaye kuliko sasa. Hivyo sehemu ya kipato chako unapaswa kuiwekeza.

Angalia kipindi hichi cha leo kujifunza uwekezaji kwa kina. Unaweza kukiangalia kwa kubonyeza maandishi haya. Pia unaweza kubonyeza hapo chini na kuangalia moja kwa moja.

Kwa vyovyote vile, hakikisha unawekeza, kwa sababu kama huwekezi leo, miaka kumi ijayo utajutia sana nafasi uliyoipoteza leo. Jifunze na chukua hatua leo hii.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog