Habari za leo rafiki?
Karibu kwenye kipindi chetu cha leo cha Ongea na Coach ambapo tumekuwa tunashirikishana maarifa sahihi ya kuweza kuwa na maisha ya mafanikio.
Katika kipindi cha leo nakwenda kukushirikisha njia za kuweza kuvuka vikwazo na changamoto kwenye safari yako ya mafanikio.
Nikuambie ukweli mmoja rafiki yangu, pamoja na malengo na mipango mkubwa unayoweza kuwa nayo, pamoja na juhudi kubwa unazoweza kuweka, siyo kila kitu kitaenda kama ulivyopanga.
Labda niweke hilo wazi zaidi, ukiona kila kitu kinaenda kama ulivyopanga basi kuna mawili, moja labda umebahatisha tu, hivyo huwezi kurudia tena na ukapata matokeo hayo hayo. Mbili; umeweka malengo na mipango midogo sana ambayo haina ugumu wowote katika kuifikia.
Kama kweli utaweka malengo na mipango mikubwa, utakutana na changamoto na vikwazo pale unapoanza kuchukua hatua. Na hapa ndipo wengi wanaposhindwa na kuachana na safari waliyoianza.
Sasa kama wewe ni rafiki yangu, sitaki kabisa uishie njiani, sitaki ukimbie changamoto wala vikwazo, bali nataka uvikabili na uweze kutoka ukiwa mshindi.
Ndiyo maana leo nimekuandalia kipindi hichi kizuri sana cha kukuwezesha kuvuka kila aina ya kikwazo na changamoto.
Katika kipindi hichi nimekupa mtazamo sahihi wa kuwa nao pale unapokutana na vikwazo na changamoto. Kitu kikubwa ambacho kinawatofautisha wale wanaoshinda na wanaoshindwa ni mtazamo wanaokuwa nao.
Kupitia kipindi hichi, nimekushirikisha mtazamo sahihi wa kujijengea ambao ukifanya hivyo, changamoto na vikwazo utavifurahia badala ya kuviogopa.
Hii ni kwa sababu;
Changamoto na vikwazo ndiyo njia yenyewe ya mafanikio.
Changamoto na vikwazo ndivyo vinafanya wachache wawe washindi na ushindi kuwa wa maana zaidi.
Changamoto na vikwazo vitaendelea kukufuata popote unapokimbilia, kama hutavitatua.
Nisiseme mengi hapa rafiki yangu, bali nikupe nafasi ya kuangalia kipindi hichi, na ninakusihi sana kiangalie. Wengi wanaoshindwa, wanakosa mtazamo muhimu sana unaokwenda kujifunza kwenye kipindi cha leo.
Kuangalia kipindi hichi kizuri cha leo, bonyeza maandishi haya au kama kifaa chako kinaruhusu angalia moja kwa moja hapo chini.
Baada ya kipindi hichi, unakwenda kuwa shujaa ambaye haangushwi na changamoto au vikwazo. Muhimu ni wewe kuyaweka kwenye vitendo haya uliyojifunza.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Makirita Amani,
Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.
Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu
Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog