Rafiki,

Wahenga walisema ukiona vyaelea ujue vimeundwa. Dunia inapenda kuona matokeo, lakini haipendi kuona ule mchakato wa matokeo hayo, namna gani yamefikiwa.

Huwa tunaona habari za watu waliotoka chini kabisa na kufanikiwa sana, lakini hatupati ile picha halisi ya njia walizopita mpaka wakafanikiwa. Utasikia maneno kwamba alikazana sana na hakukata tamaa, mwishowe amefanikiwa.

Lakini huenda huko katikati mtu alikata tamaa kwenye mambo mengi. Huenda mpango aliokuwa nao mwanzo siyo huo ambao amefanikiwa nao. Huenda kuna mahali alivunja sheria, alikiuka taratibu na alifanya mambo ambayo kikawaida hayawezi kukubalika, lakini yakamwezesha kuvuka hatua moja kwenda nyingine.

Ninachotaka kukuambia ni kwamba, kuna safari ndefu na ngumu ya kufika popote ambapo mtu anataka kufika.

Kwenye uandishi napo mambo yako hivyo hivyo. Wapo waandishi wenye mafanikio makubwa, walioandika vitabu vingi ambavyo vimegusa maisha ya wengi. Lakini wengi wamekuwa wanaviona vitabu pekee, hawaoni maisha nyuma ya vitabu hivyo.

Wengi wamekuwa wanafurahia mafanikio ya waandishi wenye mafanikio, na wao kukimbilia kuandika, bila ya kujua kazi kubwa iliyopo nyuma ya uandishi wenye mafanikio.

Mmoja wa waandishi ninaowakubali sana, alikuwa anahojiwa, akaulizwa mchakato wake wa uandishi wa vitabu ukoje. Akajibu bila ya kusita kwamba kabla hajaandika kitabu kimoja, basi anasoma vitabu 250, ndiyo vitabu mia mbili na hamsini. Unaweza kuona namna gani hiyo kazi siyo ndogo wala rahisi, hapo ni kusoma na hata hajaanza kuandika.

Kwenye kipindi cha leo nimekuandalia somo kuhusu siri kubwa ya waandishi wenye mafanikio makubwa. Angalia kipindi hichi kujifunza kitu muhimu unachopaswa kukipa kipaumbele kama unataka kufanikiwa kwenye uandishi.

Na hata kama wewe siyo mwandishi, angalia kipindi hichi, kitakupa funzo kubwa la namna unavyopaswa kujitoa kwa ajili ya mafanikio.

Unaweza kuangalia kipindi hichi kwa kubonyeza maandishi haya. Au ukaangalia moja kwa moja hapo chini kama kifaa chako kina uwezo huo.

Jifunze na chukua hatua ili kuweza kufanikiwa kupitia chochote ambacho unafanya.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.