Habari za leo rafiki yangu?

Hakuna kitu kimekuwa mzigo kwa wengi na kuwazuia kufanikiwa kama mikopo na madeni. Japo wengi wamekuwa wakidanganyika mikopo ina manufaa kwao, wengi wamekuwa wanauona ukweli halisi wa mikopo pale wanapoichukua.

Sasa changamoto kubwa sana kwenye madeni ni kwamba, watu wanadanganywa sana. Wamekuwa wanadanganywa na kauli kuu mbili;

Kauli ya kwanza ni kwamba huwezi kufanikiwa bila ya kukopa, au matajiri wengi wanakopa na ndiyo maana wamefikia utajiri.

Kauli ya pili ni ile kwamba mtu anakopesheka.

Hili ni kauli mbili ambazo zimewapoteza wengi, kwa kuwaingiza kwenye madeni ambayo hayana msaada kwao na kuishia kuteseka.

Kwenye kipindi chetu cha ONGEA NA COACH leo nimezungumzia na kuchambua aina kuu mbili za madeni ambazo unapaswa kuzijua kabla hujaingia kwenye madeni.

Pia nimekushirikisha madeni gani uyaepuke sana kwenye maisha yako, na madeni yapi ambayo yana msaada kwako. Kabla hata hujaanza kukadiria ni madeni gani mazuri kwako, nikuambie tu, madeni unayofikiria kwako ni mazuri ni mabaya mno.

Kwa mfano, kuchukua mkopo wa kujenga nyumba, kununua gari au hata kuanza biashara, ni madeni mabaya kwako na yatakurudisha nyuma. Kabla hujaanza kubisha hili, nakusihi uangalie kipindi hichi cha leo, ili uweze kupata maarifa sahihi na kuweza kuchukua hatua sahihi.

Kuangalia kipindi hichi kizuri cha leo kuhusu aina za madeni na madeni ya kuepuka, bonyeza maandishi haya.

Pia unaweza kuangalia kipindi hichi moja kwa moja hapo chini iwapo kifaa chako kinaruhusu.

Angalia kipindi hichi cha madeni, kisha chukua hatua ya kuepuka madeni ambayo hayana msaada kwako.

Pia karibu upate kitabu KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, ili uweze kujifunza mbinu za kuweza kuondoka kwenye umasikini. Kupata kitabu hichi angalia maelekezo ya picha hapo chini.


Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,


Kupata blog yako ya kitaalamu, unayoweza kuitumia kutengeneza kipato, BONYEZA maandishi haya.

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Pata kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ujifunze jinsi unavyoweza kuanzisha na kukuza biashara yako, pia utajifunza mifereji nane(08) ya kipato unayopaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha. Bonyeza maandishi haya kupata kitabu.