Habari za leo rafiki yangu?

Karibu kwenye kipindi chetu cha leo cha ONGEA NA COACH ambapo nimekuwa nakushirikisha mambo muhimu ya kuweza kuwa na maisha bora na yenye mafanikio.

Katika kipindi cha leo nakwenda kukushirikisha kuhusu changamoto ya ajira na hatua za kuchukua kwa wahitimu ambao hawajapata ajira.

Hili liko wazi sasa ya kwamba ajira ni changamoto. Mara zote tunaona nafasi chache za kazi zinazotangazwa, wanaomba watu wengi mno. Wahitimu ni wengi kuliko nafasi za ajira zinazopatikana.

Hali hii imekuwa inawaumiza vijana wengi ambao wameishi maisha yao yote wakiambiwa wasome kwa bidii, wafaulu na watapata ajira nzuri na kuwa na maisha mazuri.

Vijana wanakazana kusoma kweli, wanafaulu na kuhitimu, lakini ajira zinakuwa changamoto.

Katika kipindi cha leo nimezungumzia mambo matatu muhimu sana;

Jambo la kwanza ni kuendelea kuomba kazi kwa wale ambao ndiyo wamehitimu, lakini wakati huo wasiruhusu maisha yao kusimama wakisubiri ajira. Badala yake waendelee kufanya mambo mengine pia.

Jambo la pili ni kufanya maamuzi magumu ya kuachana na harakati za jira, hasa pale ambapo umehitimu zaidi ya miaka miwili na umetafuta ajira bila ya mafanikio.

Jambo la tatu ni hatua za kuchukua, hapa nimekushirikisha ufanye nini sasa pale ambapo umefanya maamuzi magumu ya kuachana na zoezi la kutafuta ajira na kushika hatamu ya maisha yako. Nimekushirikisha maeneo ambayo unaweza kuanzia na ukaweza kupiga hatua kwenye maisha yako.

Angalia somo hili, jifunze na chukua hatua.

Unaweza kuangalia somo hili kwa kubonyeza maandishi haya, au kwa kuangalia moja kwa moja hapo chini.

 

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Makirita Amani,

fb instagram

Kama umejifunza kupitia makala hii karibu tujifunze zaidi kupitia KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utaingia kwenye kundi la wasap na kupata mafunzo kila siku. Bonyeza maandishi haya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kupata vitabu vya biashara na mafanikio tembelea www.kisimachamaarifa.co.tz/vitabu

Kupata blog ya kitaalamu unayoweza kuitumia kutengeneza kipato tembelea www.mtaalamu.net/patablog