Aina Tatu Za Ukomo Uliojiwekea Kwenye Kipato Na Njia Tano Za Kuondoa Ukomo Kwenye Kipato Chako Ili Kufikia Uhuru Wa Kifedha.

Rafiki yangu mpendwa, Sihitaji tena kutumia muda mwingi kukushawishi kwa nini fedha ni muhimu na kwa nini kutengeneza kipato zaidi inapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kwako. Kwa sababu kama mpaka sasa hujalielewa hilo, una tatizo kubwa zaidi ambalo msaada wake hauwezi kupatikana kwenye makala kama hii. Kosa kubwa ambalo watu wengi wamekuwa wanalifanya kwenye fedha... Continue Reading →

Karibu Kwenye Semina Ya KISIMA CHA MAARIFA 2018; Mafanikio, Biashara Na Uhuru Wa Kifedha.

Rafiki yangu mpendwa, Kila mwaka nimekuwa naendesha semina tatu, mbili kwa njia ya mtandao na moja ya kukutana moja kwa moja. Kwa mwaka huu 2018, tayari tumeshapata semina mbili kwa njia ya mtandao, ambapo ya kwanza ilikuwa ya kuanza mwaka, mafunzo yake yako hapa (http://www.kisimachamaarifa.co.tz/semina2018/). Ya pili ilikuwa ya ukuaji wa biashara na kuongeza faida... Continue Reading →

Vitu Hivi Viwili Ndiyo Vinavyokuzuia Usipate Kiasi Cha Fedha Unachotaka Kupata Kwenye Kazi Au Biashara Yako.

Rafiki yangu mpendwa, Moja ya vitu vinavyowafanya wengi wakose usingizi ni fedha. Sehemu kubwa sana ya watu wanaishi kwa mfumo wa mkono kwenda kinywani. Yaani wanafanya kazi au biashara, wanalipwa kiasi kidogo cha fedha, wanaitumia kwenye chakula halafu wanabaki hawana fedha nyingine. Inawabidi wakafanye tena kazi au biashara ndiyo wapate tena fedha ya kula. Wakati... Continue Reading →

Hatua Ya Kwanza Muhimu Sana Ya Kuelekea Kwenye Utajiri, Ambayo Wengi Wanaipuuza Na Inawagharimu Sana.

Kama ukisikia neno utajiri unajisikia vibaya, unapata mawazo ya watu wabaya, watu wanaowanyonya na kuwanyanyasa wengine, basi nina habari mbaya kwako, umejizawadia maisha ya umasikini mpaka kifo chako. Akili yako ni janja sana, haiwezi kamwe kukupa kitu ambacho imani yako inapingana nacho, hivyo kama imani yako inaona matajiri ni watu wabaya, matajiri ni watu wasiofaa,... Continue Reading →

Kauli Hii Unayopenda Kutumia Kuhusu Fedha Ndiyo Inayokuzuia Kupata Fedha Unazostahili Kupata.

Hivi unajua kwamba kila mtu anapaswa kupata kiasi chochote cha fedha anachotaka kupata? Hivi unajua kwamba dunia ina fedha nyingi kiasi cha kumwezesha kila mtu kuwa tajiri? Hivi unajua kwamba kiasi cha fedha duniani kimekuwa kinaongezeka kila mwaka na matajiri wamekuwa wanazidi kuwa wengi? Unaweza kuwa unayajua haya, lakini kwa ndani unajiambia fedha siyo muhimu,... Continue Reading →

Kila Kitu Unachopaswa Kujua Kuhusu Cryptocurrency Na Bitcoin (Fedha Za Kidijitali) Na Kwa Nini Siyo Uwekezaji Mzuri Kwako Kwa Sasa.

Habari kubwa katika kipindi hichi kwa upande wa fedha na uwekezaji ni cryptocurrency au kama inavyofahamika kwa Kiswahili fedha za kidijitali. Aina hii ya fedha imewavutia wengi siyo kwa sababu ya matumizi yake, bali kwa jinsi thamani yake inavyokua kwa kasi na hivyo wengi kuona ni sehemu rahisi ya kupata fedha nyingi bila ya kufanya... Continue Reading →

Mitazamo Hii Mitano (05) Kuhusu Kipato Ndiyo Inakufanya Uingie Kwenye Matatizo Ya Kifedha, Ijue Na Hatua Za Kuchukua Ili Kuondoka Kwenye Umasikini.

Fedha na malipo ndiyo mada nzuri kuliko zote kwenye mijadala yetu ya kila siku. Ninaposema nzuri siyo lazima uwe unaifurahia, lakini hichi ni kitu ambacho kila mtu lazima akifikiria kila siku. Kwa wengine ndiyo kitu wanafikiria siku nzima, hasa pale kipato kinapokuwa kidogo, matumizi makubwa na madeni mengi. Lakini pamoja na kufikiria sana kuhusu fedha,... Continue Reading →

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑