Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo makubwa na kufikia ndoto zetu kubwa.

IMG_20170102_073855
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu DO YOUR WORK, yaani FANYA KAZI YAKO….
Hiki ndiyo kitu pekee muhimu na ambacho unaweza kukisimamia kwenye maisha yako.
Fanya kazi yako, na ifanye kwa usahihi, ifanye kwa juhudi.
Usifanye tu kama unavyotegemewa, bali nenda hatua ya ziada, weka juhudi zaidi.
Ni katika kufanya kazi yako ndipo utakapokutana na watu muhimu kwako.
Ni katika kufanya kazi yako ndipo utakapozifikia ndoto zako.
Ni muhimu mno ufanye kazi yako.

Nikupe tahadhari ya kwamba, katika kufanya kazi yako mambo hayatakuwa rahisi kama utakavyopenda wewe mwenyewe.
Kuna wakati utakutana na magumu na changamoto kubwa.
Kuna wakati utapata matokeo tofauti na uliyotegemea,
Lakini haya yote hayapaswi kukuzuia wewe kufanya kazi yako.

Fanya kazi yako, hicho pekee ndiyo kitakachokubeba kwenye maisha yako.
Siyo kusema kwamba utafanya,
Siyo kujifanya uonekane unafanya,
Na siyo kutoa sababu kwa nini hufanyi,
Bali kufanya, kuleta majibu yanayotokana na kufanya, ndiko kutakubeba wewe.

Kwa msisitizo zaidi rafiki yangu, DO YOUR WORK.

Nakutakia siku njema sana ya leo.
Rafiki na Kocha Wako,
Makirita Amani,
Success Coach, Author and Entrepreneur
Blogs; http://www.amkamtanzania.com and http://www.kisimachamaarifa.co.tz
SUCCESS IS YOUR BIRTHRIGHT.