Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu.

Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo ambapo tumepata nafasi nyingine nzuri ya kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa.

Msingi wetu wa mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu JAMII INAKUDANGANYA…

Linapokuja swala la mafanikio, kwa sehemu kubwa sana jamii inakudanganya.

Jamii inakuonesha picha ambayo siyo halisi.

Jamii inajaribu kuonesha kwamba mafanikio ni rahisi na hayahitaji juhudi kubwa.

Pia jamii inajaribu kukuonesha kwamba zipo njia za mkato, ambazo ukizijua na kuzitumia utaweza kufanikiwa kwa haraka.

Yote hayo ni uongo na haijalishi nani anayekuambia, ni uongo. Haya kama kila mtu kwenye jamii anaamini na kufanya hayo, bado ni uongo.

Wewe ijue misingi na simama kwenye misingi, hakuna kinachoweza kukuteteresha kwenye misingi.

Chochote unachoambiwa kinafaa, kama kinakwenda kinyume na misingi sahihi, achana nacho, hata kama watu wanakupa ushahidi kwamba kimewafaa. Chochote kinachofanywa nje ya misingi, kina ukomo wake na ukomo huo huwa mbaya sana.

Usikubali kudanganyika na jamii, hata kama unaoneshwa vitu vizuri kiasi gani. Simama kwenye msingi na mafanikio utayapata.

Nakutakia siku njema sana ya leo, uende ukafanye makubwa na kuweza kupata matokeo bora.

Rafiki yako,

Kocha Makirita Amani,

MAFANIKIO NI HAKI YAKO YA KUZALIWA.

www.kisimachamaarifa.co.tz