Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari FANYA TENA…
Rafiki yangu,
Baada ya kushindwa,
Baada ya kuanguka,
Baada ya kukutana na magumu na changamoto,
Kinachofuata ni kufanya tena.
Haijalishi umekutana na ugumu kiasi gani, haijalishi umeshindwa kiasi gani, hakuna kitakachokusaidia bali kufanya tena.
Umeanzisha biashara na imekufa? Vizuri, sasa fanya tena, fanya ukiwa na funzo kwa nini biashara uliyoanzisha ilikufa, ili unayoanzisha sasa isife.
Umefanya kilimo na hujapata mafunzo mazuri? Hiyo ni safi, sasa rudi shamba ukiwa na funzo kwa nini kilimo ulichofanya awali hakikukupa matokeo mazuri, na sasa upambane mpaka upate mavuno mazuri.
Kuna kitu chochote ambacho ulijitoa sana kufanya, ukaweka kila aina ya juhudi, lakini umepata matokeo ambayo hukitegemea? Vizuri, sasa fanya fanya ukiwa na funzo zuri, ili usirudie makosa uliyofanya mwanzo.
Rafiki yangu mpendwa, kitu pekee kitakachokusaidia kwenye haya maisha ni KUFANYA.
Unaweza kuongea utakavyo, unaweza kueleza kila aina ya sababu, unaweza kulalamika na kulaumu utakavyo,
Lakini kumbuka, maneno ni sawa na upepo, yanapita tu.
Kitakachokusaidia wewe ni kifanyam kuchukua hatua.
Usitumie muda mwingi kutuambia kwa nini umeshindwa, au kitafuta aliyefanya ushindwe.
Peleka muda wako wote kwenye kufanya.
Ukishindwa, kaa chini na pitia kila ulichofanya, na jiulize wapi nimekosea, na ni wewe umekosea, wala usitafute nani kakosea.
Ukishajua ulipokosea, fanya tena, ila sasa epuka makosa uliyofanya awali.
Umeshindwa, vizuri, fanya tena. Kuna ugumu gani hapo rafiki yangu? Maana utapata kama utafanya. Na hakuna atakayekupa unachotaka kwa huruma kwamba umeshindwa, ni kwa kufanya.
Hivyp usipoteze muda wako kutoa sababu kwamba umeshindwa, bali jifunze uliposhindwa na fanya tena.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, leo nenda kafanye tena kile ulichoshindwa.
#Fanya #FanyaTena #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha