“Circumstances are what deceive us—you must be discerning in them. We embrace evil before good. We desire the opposite of what we once desired. Our prayers are at war with our prayers, our plans with our plans.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 45.6

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KUDANGANYIKA NA KUGAWANYIKA..
Hatufikii malengo na mipango mikubwa tunayokuwa tumejiwekea kwa sababu tumedanganyika na kugawanyika.
Tunajidanganya kuhusu uhalisia wa jambo, hatujiambii ukweli kama ulivyo, hatuwezi maandalizi ya kutosha na hata juhudi tunazoweka siyo kwa uwezo wetu wote.
Tunajidanganya na kutegemea tupate matokeo bora, tusipoyapata tunatoa lawama kwa kila mtu kasoro sisi wenyewe.

Lakini pia kinachotuzuia kupata tunachotaka ni kujigawa kwenye mambo mengi na yasiyo na maana. Tunataka kufanya kila kitu, hatuna kipaumbele. Hivyo mipango inakuwa mingi na inakuwa inashindana yenyewe. Kwa kugawanyika huku, unashindwa kuweka nguvu zako zote kwenye kitu kimoja na kukifanya kwa ufanisi wa hali ya juu.
Kadiri unavyofanya vitu vingi kwa pamoja, ndivyo unavyoshindwa kwenye vyote.

Hivyo tuwe makinim tusijidangaye, tujiambie ukweli kama ulivyo, tuwe na maandalizi sahihi na tuweke juhudi kubwa sana kadiri inavyohitajika. Tusiende tu kwa kubahatisha tukifikiri mambo yatakuwa mazuri yenyewe.
Na pia tusijigawe sana, kuwa na mpango mmoja mkubwa ambao ndiyo unaweka akili yako yote, muda wako wote na nguvu zako zote. Unapoweka kila ulichonacho kwenye kitu kimoja kikubwa unajipa nafasi ya kukifikia zaidi kuliko kujigawa kwenye vitu vingi.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuacha kujidsnganya na kujigawa, ukabili ukweli na fanyia kazi kitu kimoja kwa wakati.
#Usijidanganye, #UsijigaweKwenyeMengi, #WekaJuhudiKubwaKwaMachache

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha