“If you are defeated once and tell yourself you will overcome, but carry on as before, know in the end you’ll be so ill and weakened that eventually you won’t even notice your mistake and will begin to rationalize your behavior.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.18.31
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari USIWE MWEHU…
Wehu ni kufanya jambo lile lile, kwa namna ile ile halafu utegemee matokeo ya tofauti.
Ni jambo la kushangaza lakini watu wengi ndivyo wanavyoendesha maisha yako.
Mtu anafanya kazi ile ile kwa namna ile ile halafu anategemea kipato chake kiongezeke.
Mwingine anafanya biashara yake kwa mazoea lakini anategemea kipato kitakua sana.
Wengi wanaendesha siku zao kwa mazoea, bila ya mipango wala vipaumbele vyovyote halafu wanashangaa pale siku zinapoisha na hakuna kikubwa wamefanya.
Rafiki, kupata matokeo ya tofauti na unavyopata sasa, lazima ufikiri tofauti na kufanya tofauti na unavyofanya sasa.
Halihitaji iwe na elimu kubwa kujua kwamba ukipanda mahindi huwezi kutegemea kuvuna mtama.
Lakini watu wanamategemeo ya aina hiyo kila siku, na haishangazi kwa nini watu wengi wana maisha magumu.
Usilalamikie matokeo unayopata, bali angalia fikra ulizonazo na hatua unazochukua.
Kama unataka matokeo ya tofauti anza kufikiri tofauti na chukua hatua tofauti.
Kuna ugumu gani hapo?
Ukawenna siku bora sana ya leo, siku ya kufikiri tofauti na kuchukua hatua tofauti ili kupata matokeo tofauti.
#UsiweMwehu #FikiriTofauti #ChukuaHatuaTofauti
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani ,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1