“Lengo la kuanzisha biashara ni kutengeneza na kuuza kitu ambacho watu wanakihitaji na kukiuza kwa faida na kisha kutumia faida hiyo kuajiri timu bora ambayo itatengeneza kilicho bora zaidi.”
Huo ndiyo muhtasari wa biashara kwa sentensi moja. Chochote zaidi ya hapo ni kujisumbua tu.
Sasa rudia hili na mimi, kwa biashara unayoifanya au unayotegemea kuifanya, andika muhtasari wake kwa sentensi moja tu. Ukishafanya hivyo weka nguvu zako zote kwenye kufanyia kazi muhtasari huo, mengine yote achana nayo kwa sasa.
Kama huwezi kuielezea biashara yako kwa muhtasari au kama huwezi kuelekeza nguvu zako kwenye muhtasari huo, basi hujaielewa biashara yako na hilo litakuwa kikwazo kwako kufanikiwa kwenye biashara hiyo.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Asante sana maarifa ya mhitasari huu.
LikeLike