“Men, the philosopher’s lecture-hall is a hospital—you shouldn’t walk out of it feeling pleasure, but pain, for you aren’t well when you enter it.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.23.30
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ambayo tumeiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari FALSAFA KAMA TIBA…
Ukienda hospitali ukiwa unaumwa na ukaondoka ukiwa na raha kuna tatizo,
Matibabu hayana raha, utachomwa sindano ambazo zinauma, utapasuliwa mwili ambapo kuna maumivu au utapewa dawa za kunywa ambazo siyo tamu kama vitu unavyopenda kula.
Pamoja na hayo tunayopaswa kufanya ili tupone kutokuwa ya kufurahisha, hatuna budi kuyafanya ili tuweze kuwa na afya bora.
Hivyo pia ndivyo falsafa ilivyo.
Kama unaisoma falsafa au kukutana na mwanafalsafa na kuondoka ukiwa unajisikia vizuri basi kuna tatizo.
Maana falsafa haipo kwa ajili ya kumfanya mtu ajisikie vizuri, bali ipo kumfanya mtu ajue na kufanya kile kilicho sahihi, ambacho mara nyingi siyo kitu tubachopenda kufanya, lakini inatubidi tufanye.
Kazinya falsafa ni kuimarisha akili, hisia na tabia, na ili kifanya hivyo, lazima ikuoneshe wazi kwamba kwa sasa unakosea. Sasa kwa kuwa wengi hatupendi ukweli, kuoneshwa kwamba tunakosea huwa kunatuumiza sana.
Na falsafa haijali kama unaumia au la, falsafa inajali wewe kufanya kilicho sahihi.
Tuitumie falsafa yetu ya ustoa kufanya yale ambayo ni sahihi, kuishi kwa misingi yetu na kusikamia ukweli hata kama unakuja na maumivu kwetu.
Kadhalika kwenye kuomba ushauri au mwongozo.
Kama mtu unayemwomba ushauri anakuambia kile ambacho unataka kukisikia, huyo mtu siyo mshauri mzuri kwako.
Anayekushauri anapaswa kukueleza ukweli kama ulivyo, haijalishi unakuumiza au la, na hataki kukufurahisha, anataka kukuonesha ukweli.
Na wewe pia unapopata nafasi ya kuwashauri au kuwaongoza wengine, epuka sana kutaka kuwaambia kile wanachopenda kusikia kwa kutaka wakupende. Badala yake waeleze ukweli hata kama hilo litakugharimu kwa watu kuchukia.
Ndiyo maana wamekuja kwako kwa ushauri, ingekuwa rahisi wangefanya wenyewe na wasingetaka ushauri. Wamekuja kwako kwa sababu mambo ni magumu, wape ukweli kama ulivyo.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kupokea na kutoa ukweli kama ulivyo bila ya kuhofia kuumia sisi wenyewe au kuwaumiza wengine. Ukweli unapaswa kusimama kama ulivyo, hauna haja ya kurembwa rembwa.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1