“God tests everyone, one with wealth, another with poverty. A rich man is tested in whether he would extend an arm of support to those who need it; a poor man in whether he would bear all his sufferings without discontent and with obedience.” —The TALMUD
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii mpya tuliyoiona leo,
Tunapaswa kwenda kuitumia siku hii vyema ili kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yetu.
Kitu kimoja muhimu sana ambacho huenda hukijui ni kwamba hapo ulipo sasa, upo kwenye majaribu.
Unajaribiwa ili kuweza kujulikana kama kweli unaweza kukabiliana na hali fulani kwenye maisha yako.
Mungu anamjaribu kila mmoja wetu kupitia kile anachompatia na hali anayopitia.
Tajiri anajaribiwa kama anaweza kuutumia utajiri wake kwa manufaa ya wengine pia, kama anaweza kuwa msaada kwa wale wenye uhitaji.
Na masikini anajaribiwa kama anaweza kuwa na uvumilivu katika wakati mgumu anaopitia na kutokukata tamaa.
Watu wengi hawapigi hatua kwenye maisha yao, kwa sababu wanashindwa majaribu madogo madogo wanayopitia.
Jua wazi ya kwamba kila unachopitia sasa kwenye maisha yako, kiwe kizuri au kibaya ni majaribu unapewa.
Lengo lako ni kuhakikisha unavuka kila aina ya majaribu unayopitia sasa ukiwa imara na kwa kufanya kile kilicho sahihi.
Usijizuie kupata makubwa na mazuri zaidi baadaye kwa kushindwa kukabiliana na madogo unayopitia sasa.
Jua kila unachopitia ni majaribu na hivyo simama imara, ukiwa na msimamo wa kufanya kile kilicho sahihi kwenye kila hali unayopitia.
Tafakari hili leo, jua ni majaribu gani unayopitia na kisha hakikisha unavuka majaribu hayo vizuri kwa sababu upande wa pili wa majaribu hayo ndiyo kuna mafanikio makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania